Lakini eti tunasali makanisani na misikitini kumueleza Mungu aiangalie TZ kwa huruma. Vyuo vikuu vyote tulivyonavyo navyo wamefunga badala ya kufanya tafiti za kuokoa watu. Bado watu wanadhani Korani na Biblia ni vitabu vya medicine. Inatia shaka sana!
Kila ukiangalia ulaya na America zinavyovurugwa, na jinsi watumishi wa afya wanavyohangaikia wagonjwa na bado wengine wanapoteza maisha, basi naamini hapa kwetu, COVID-19 inapiga inavyotaka.
Sekta yetu ya afya haina kujituma bali ni kutafuta kuhusudiwa tu! Kuna wanaojiita maprofesa pale Muhimbili najua sasa wako bize kuandika wapate pesa za miradi kama walivyopiga za UKIMWI bila lolote la maana, Hawawezi hata kubuni mbimu za kitabibu kuwasaidia wagonjwa! Kila mtu anapenda kupumzika na kula migahawani huku wagonjwa wakiteseka. Mtu si anaamua kusepa tu!