Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Vipaumbele:
1. Elimu
2. Afya
3. Kilimo
4. Miundombinu
5. Utawala bora
6. Mawasiliano

Swali: Je, kwa takribani miaka 54 ya kuwa madarakani wametekeleza hayo kwa kiwango gani cha kuridhisha wananchi?!

Je, kwa sasa kuna miujiza gani watakayotumia kutekeleza ilani hiyo?

Kama kwa zaidi ya nusu karne wameshindwa kutekeleza haya, badi pengine hawatufai kabisa(Hawakutufaa toka mwanzo).

1.ELIMU:

Nchi hii watu wanasomea chini ya mti(Kongwa Dodoma), Bunge liko Dodoma.

Nchi hii kule Geita wanafunzi wanasoma katika madarasa ambayo hayajaezekwa(Geita atokako Mh. Magufuli).

Elimu hii inayochezewa kwa wanafunzi kujihangaikia masomoni(kwa shida) na kushindwa kuajiriwa na wakimaliza wanashindwa hata kuajiriwa.

Elimu hii yenye kubadilishwa mitaala karibu kila baada ya mwaka hadi miaka miwili na kufanya wanafunzi kutokujielewa.


2. AFYA.

Sehemu ambapo hata Hospitali ya Taifa wataalamu wako tele lakini wenye kutoleana macho tu mgonjwa anapofika kwasababu ya kutokuwa na vifaa tiba, dawa.

Sehemu ambapo Serikali inahadaa wananchi huduma bure, lakini hakuna hospitali yenye kutoa huduma bure hata kwa makundi maalum(wazee, wajawazito, watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano).

Nchi ambayo mwananchi asiye mtumishi wa Serikali hapati fursa/kuhimizwa kutumia BIMA, na yule aliye mtumishi ingawa anapata huduma za kitabibu bado huduma ya dawa ni changamoto.


Nchi ambayo Wananchi wanalala chini...chini katika/kwenye sakafu wakiwa hospitalini kwa uhaba wa vitanda lakini viongozi wa nchi wakitibiwa nje kila leo, in the name of ' ni pesa yake, kama anamudu kwanini asiemde'


3. KILIMO:

Migogoro kushindwa kutatuliwa kati ya wafugaji na wakulima.

Kushindwa kumjali mkulima mdogo(small scale) katika uuzaji, kuwapangia bei watakazo katika masoko.

4. MIUNDOMBINU.

Hivi si Nchi hii yenye kukumbwa na Mafuriko kila mwaka, anticipation kushindwa kufanyika kila mwaka?

Nchi ambayo baada ya mafuriko tunalia tunakosa maji tukishindwa ku_harvest haya maji kwa matumizi ya baadae.

Nchi ambayo Umeme unakosekana despite vyanzo kadhaa vya umeme(Maporomoko, Makaa ya mawe, Vyura wa Kihansi, Mabwawa, Nishati ya jua, Gesi) sehemu ambapo tu hata kwa Nishati ya jua kila kijiji kina uwezo wa kuwa na Solar (Wananchi wakichangia na Serikali ikiwawezesha).

Nchi ambayo barabara zake zahitaji ukarabati kila mwaka( na sehemu nyingine utanuzi).


UTAWALA BORA:

Nchi ambayo Serikali(Mhimili mmoja wa dola una nguvu na kandamizi kushinda mwingine, lakini pamoja na jitihada za kuboresha hili kupitia Katiba mpya Serikali hiyo hiyo(Kupitia watu wale wale waliodanganya umma kywa watahakikisha Katiba inapatikana kabla ya kumaliza hatamu ya uongozi kuhafifisha suala hili.

Nchi ambayo Watawala ni watu wenye kuwaweka ndugu na jamaa zao katika ngazi za juu(na chini pia) hata kama hawana uwezo/vigezo vya kuwepo huko na wenye kufanya maamuzi yasiyo na tija kwa Taifa.


6. MAWASILIANO.

Mawasiliano kutunza nyaraka za Serikali. Hili ni jambo zuri, lakini hebu tujiulize kama katika kipindi cha miaka kumi iliyopita Siri na nyaraka kupitia njia nyingi za mawasiliano ya Setikali vimefichuliwa hivi na bado Serikali haioni haya/aibu kwa uozo ulio ndani yake wala hakuna jitihada kurekebisha, itakuwaje pale ambapo tutazuiliwa na sheria kandamizi kupata hata hicho kidogo(uozo) Serikalini.


Kama wameshindwa haya kwa zaidi ya nusu Karne hawataweza hata kama tukiwapatia Nchi kwa Karne nzima. Failure has been proved by CCM.
 
Vipaumbele:
1. Elimu
2. Afya
3. Kilimo
4. Miundombinu
5. Utawala bora
6. Mawasiliano

Swali: Je, kwa takribani miaka 54 ya kuwa madarakani wametekeleza hayo kwa kiwango gani cha kuridhisha wananchi?!

Je, kwa sasa kuna miujiza gani watakayotumia kutekeleza ilani hiyo?


Ilani kuu ya uchaguzi 2005 na 2010: Kasi mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya iliishia wapi? Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Nadhani ccm wanawaona watanzania kama mazuzu hivi, maana wanabadilisha biti tu lakini wimbo ni uleule!

[
 
Hichi chama kinakurupuka sana,its a shame kabisa,mnataka twende kwenye uchumi wakati maviwanda yamekua magofu?
 
ah! kwani hawa si walikuwepo miaka yote 54+ au uchaguzi huu ndio wanategemea iwe mara yao ya kwanza? lkn ni mara nyingi nimekuwa nikisikia ilani ilan lkn sioni lolote labda umaskini.
 
Umesahau ahadi laplop kwa kila mwalimu.
1-Ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania iko wapi?
2-Ahadi kigoma kuwa dubai imeishia wapi?
3-Huduma bora za afya mpaka leo mama zetu wanajifungulia chini?
4-Tatizo la umeme kuisha Arusha mbona kila siku hamna umeme?
Ccm mmeshachoka na sisi tumewachoka hatugemei mabadabiliko yote chini ya chama kile kile,sera zile zile,mfumo ule ule ,watu wale wale na ahadi hewa zile zile huu mwaka wa mabadiliko .watanzania wanaotaka maendeleo kuanzia kura za udiwani,ubunge na uraisi pigia viongozi wa UKAWA.
POMBE MWISHO KAUNTA MTAANI NA IKULU NI LOWASA.
 
Hizi ni porojo toka miaka 40 iliyopita. Hivi vitu walitaka kufanya miaka mingi imefika. Kila siku the same irani. Matekelezo hamna. Utasikia 2025 watakuja na the same vibwagizo .
 
Hao wanatudanganya na Ilani yao. Mbona maisha bora kwa Mtanzania hatuioni ila maisha duni sana kwa mtanzania ndiyo tunaiona. Msidanganyike enyi Watanzania wenzangu.
 
CCM kwa mara nyingine wametoa ilani ya hovyohovyo! Vipaumbele vyake eti watajenga Zahanati kwa kila kijiji! Hivi hawajui tatizo hasa ni nini? Ukienda Muhimbili hospital (hospitali ya taifa) hakuna vitanda vya kutosha achilia mbali uchafu uliokithiri na madawa! Huko vijijini itakuwaje? Siyo kujenga tu maghofu na kuyaacha huko?

Kipaumbele kingine eti wanakuja leo na ngonjera za kujenga reli Dar es Salaam na mikoani huku wakiwa hawajatoa mchanganuo wowote!

Kipaumbele kingine ni kujenga uwanja wa ndege Dodoma! Vipi vile ilivyoahidi mwaka 2010 vya Mwanza, Kagera na Songwe?

Leo wanakuja na sera ileile ya kilimo? Hawajatoa ufumbuzi wowote ule wa tatizo la ajira na umasikini!

Mimi nilidhani kuwa CCM wangetumia huu ushindani uliopo kutoa ilani bora walau kuleta matumaini kwa wanachama wao ila ndo wameharibu kabisa!!

"Jiwe walilokataa CCM sasa limekuwa jiwe kuu la nchi, atakayeangukiwa na jiwe hilo atasagwasagwa"
 
VIPAUMBELE VYA ILANI YA MAGUFULI NA CCM 2015-2020
1. Kulinda wizi wa Watangulizi wake
2. Kuendelea kuchakachua maoni ya watanzania. Kuhusu katiba mpya
3. Kulinda wauza madawa ya kulevya
4. Kulinda majangili na wahalifu wote nchini
5. Kulinda na kusitawisha wageni dhidi ya wazawa: wachina NK .
 
Wanajaza vipaumbele lukuki ili wapige mpunga.

Mwakahuu walewanao wadharau na kuwaita wanywa viroba ndio wataonyesha hasirazao kwenye sanduku la kura kwa magamba kwakuwa wao ccm ndio walio sababisha kutokea kwa hao wanao waita wanywa viloba kwa kuwanyima elimu bora sasa wameshazinduka shida wanazopata wamesha jua magamba ndio tatizo.
 
Hawawezi tena, kiwango chao cha kufikiria kimefika mwisho. Kama Mwenyekiti wa kamati ya ilani ni wassira unategemea nini?
 
Wanasema habari za kuboresha huduma za afya. Cha kusikitisha ni kwamba ukifika kwenye vituo vya afya leo hii utaambiwa dawa za magonjwa ya kawaida kabisa kama vile malaria, homa za matumbo, mafua n.k hazipo, ila CONDOM zipo kwa wingi sana. Hivi jamani condom ni dawa ya ugonjwa gani? Afya bora ya ccm hiyo.

Niliwahi kuwa mtafiti kupitia USAID na tulikuwa tunafuatilia uwepo wa huduma za kinga , ushauri nasaha pamoja na utoajiwa wa dawa za HIV. Yafuatayo ni baadhi ya mambo niliyoyaona field.

1. Katika village dispensaries za serikali kuna uhaba mkubwa wa matabibu, Nesi aliyesoma mwaka mmoja yeye ndo anafanya dressing, prescriptions, anatoa dawa, kuzarisha, ushauri nasaha n.k

2. Vituo vina nesi mmoja tu au wawili walivishwa dhamana ya udaktari.

3. Manesi wana maisha magumu na wamefanana na wanavijiji kwa kila kitu.

4. Hawana morale ya kazi.

N.k

Serikali ya CCM. Nazani huwa hawafiki huko.
 
Wameongeza beti tu na vibwagizo. Sawa na wasira aliesema ataleta maendeleo in coming 5 years
 
Ni wale wanaofaidika na mfumo huu gandamizi, na serikali ya CCM tu, ndio ambao wanaendelea kutetea CCM. Vinginevyo, unahitaji upungufu wa akili, kuendelea kudanganywa kwa miaka 54.

Rejea "UKIONA MTU KANG'ANG'ANIA KWENYE GARI BOVU, JUA KUNA MZIGO WAKE"

Kwaheri CCM.
 
Wanamtegemea mungu coz ndiyo anayewachagulia kiongozi wa kusimamia yote hayo
 
Viwanda na mashirika hamna tena,sasa hili bomu la ajira mtalitatua vp?na huo uchumi wa kati tutafikaje?au mnataka vijana waendelee kuendesha bodaboda?

CCM bomu la kulipuka muda wowote kuanzia sasa!
 
[video]https://m.youtube.com/watch?v=LXS2szrrX7E[/video]
 
CCM imezindua ilani yake ya uchaguzi wa 2015 - 2020.Katika ilani hiyo imeanisha kuwa vipaumbele ni Kupambana na umaskini,kupambana na rushwa,Ajira kwa vijana,Ulinzi na Usalama.Aidha CCM ina ahidi upya kuborsha miundombinu,kukuza uchumi,kuboresha viwanda,nishati,kilimo sanaa na michezo. Kabla ya kuamini na kuikubali ILANI hii ya CCM naomba tuchambue kwa ufupi ahadi hizo kwa miaka 54 ya Uhuru na Utawala wa TANU - CCM.
1. Kupambana na umaskini - CCM imeshindwa kabisa kupambana na umaskini kwa miaka yote 54.Umaskini umefikia hatua ya kutisha kiasi kwamba hata mlo mmoja umekuwa ni shida vijijini na mijini.Mgombea wa UKAWA naeleweka kidogo kwa kuwa amekuwa akisema kila wakati kwamba anauchukia umaskini na atapambana nao kwa nguvu zake zote.Unaweza vipi kukiamini chama kilichouwepo madarakani kwa miaka 54 na kikashindwa kabisa kuuondoa umaskini huo?MKUKUTA na MKURABITA imebaki kuwa katika makabrasha tu.Wachache ndio wanaonufaika na rasilimali za nchi.
2. Ajira kwa vijana - Hali ya ajira kwa vijana wa Tanzania ni janga ambalo linakaribia kuleta madhara. Mifano ni mingi.Vijana maelfu kwa mamia hawana ajira za kuaminika na wamekuwa wakihaha kujipatia ridhiki zao ili hali watoto wa vigogo wakichukua ajira muhimu za nchi.Kwa kijana maskini asiye na wa kumshika mkono hawezi kupata ajira kamwe.Uhamiaji walitangaza ajira kama 70 walijitokeza vijana zaidi ya 10,000 kuomba ajira ambazo pia walipatiwa watoto wa vigogo japo vyombo vya habari viliingila kati.Mh. Lowassa aliwahi kusema mara kwa mara kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka.Yeye yupo tayari kutatua kwa dhati tatizo la ajira kwa vjana wa Kitanzania wakauaga umaskini kwa rasilimali za nchi yetu.
3. Ulinzi na usalama - Hali ya usalama wa nchi ni mzuri.Hali ya usalama wa wananchi ipo matatani. Wananchi wa kanda ya Ziwa wanauawa kwa kukatwa makoromeo na serikali imekaa kimya hakuna hata tamko. Albino wanauawa na wengine wanakatwa viungo vyao.Jeshi la Polisi limekuwa likipambana naraia wasiokuwa na silaha kwa nguvu kubwa. Viongozi wa vyama upinzani na waandishi wa habari wamekuwa wakishambuliwa na idara nyeti za ulinzi na usalama.Matumizi ya mabavu kwa majeshi yetu yameondoa dhana nzima ya ulinzi na usalama kwa wananchi wa Tanzania ndani ya taifa lao. Wageni kutoka nchi jirani wamekuwa wakiingia Tanzania na kufanya shughuli zao huku wakihatarisha usalama wan chi na wanaohusika wakiaminika kupokea chochote.
4. Rushwa – Hali ya rushwa ( Matumizi mabaya ya mali/Ofisi za umma kwa manufaa binafsi) ni tete nay a kutisha. Magali na vyombo vya usafiri vya Taifa vimekuwa vikitumika na Viongozi wa CCM nje ya utaratibu.Watumishi wa umma wamekuwa wakifanya kazi za chama ama zao binafsi na hivyo kuisababishia Nchi hasara kubwa katika muda ama Ofisi za Serikali.Hongo katika CCM imekuwa ya kupitiliza nay a kutisha.Viongozi wengi waliobwaga manyanga wanalalamikia hongo na rushwa katika kuwapitisha Viongozi katika uchaguzi. CCM itawezaje kutatua taizo la rushwa nchini ilihali imeshindwa kutatua ndani ya chama chake? Wala rushwa wengi na wakubwa wapo CCM.Mikataba ya kiulaghai imesainiwa na Viongozi wa Serikali chini ya CCM.Viongozi waandamizi wanatetea upuuzi huo.Hii ni hatari kubwa.
5. Ujenzi wa Miundombinu – Pamoja na jitihada zinazoelezwa barabara nyingi zimejengwa chini ya kiwango kwa gharama kubwa.Paul Makonda amekaririwa akilalamika ujenzi duni katika Wilaya yake tu ndani ya Dar es salaam. Kwingine kukoje? Mkoa kama wa Morogoro bado haujaunganishwa na Ruvuma kwa barabara hata ya vumbi ukiacha ile ya wafugaji wa Kisukuma. Kwa chama kilichokaa mdarakani kwa miaka 54 haitoshi.Kinahitaji PUMZIKO.
6. Kukuza uchumi – Uchumi wan chi umeporomoka kwa kasi ya ajabu. Bei ya mazao ya biashara nje imeshuka sana. Fedha za kigeni zimepanda na Shilingi imeshika kwa kasi ya ajabu. Shughuli za Kiuchumi kama Kilimo kimedidimia kutokana na kukosa pembejeo.Wawekezaji wa ndani na nje hawana habari kuwekeza katika kilimo kwa kuwa maeneo yanayolipa kwa haraka kama madini na gesi yapo nje nje. Bidhaa za ndani hazina soko kabisa na sasa tunatumia njiti za meno,sabuni,viberiti,nyembe,mishumaa,madodoki,soksi,chupi,leso,sidiria,njiti za masikioni nk kutoka nje.Viwanda vyetu havina thamani na vingine vimefungwa kabisa.Lowassa ameahidi kufufua viwanda kama General Tyre na vingine vingi.
7. Nishati – Ni janga la Taifa kama majanga mengine. Mkoa unaopata umeme muda wote ni Kagera tu kwa kuwa unachukua nishaiti hii kutoka Uganda.Vyanzo vya kuzalisha umeme wa kutosha tunavyo shida ni uzembe na rushwa za Viongozi wetu.Vyanzo vinavyotajwa sasa vya gesi tayari vimetekwa na wawekezaji na wananchi hawataambulia lolote.Vijana wanaotegemea umeme kwa ajili ya saloon,uchomeleaji,usindikaji wa bidhaa,viwanda vidogo na vikubwa ni kero.
8. Kilimo – Ukosefu wa pembejeo na matumizi ya jembe la mkono ambalo liltakiwa kuwa Makumbusho ya Taifa ni shida. Mkulima anahangaika mwaka mzima anachopata hakikidhi hata kwa miezi mitatu. Mkulima anaconda,mifugo inakonda na mfugaji anaconda pia. Masoko imekuwa ni kero nyingine. Viongozi wapo radhi kuleta mchele wa Thailand na kuuzwa kwa bei ya chini huku mchele wa Tanzania ukikosa soko. Sukari ya Tanzania inakosa soko nay a nje inauzwa kwa bei poa huku wafanyabiashara wakikwepa kodi.
9. Sanaa na michezo – Kama kuna mahali serikali ya CCM imeshindwa kuendana na wakati ni katika Nyanja hii.Imeshindwa kuweka misingi bora na imeishia kuwekeza katika ushindi wa kubahatisha wa Timu za Taifa.Ni lazima uwekezaji uanzie chini na kwa usimamizi bora. Sanaa za maonesho zimeingiliwa.Tunu za Taifa hazijulikani.Wasanii na wanamichezo wameshaulika. Wanaokumbukwa ni wakina Diamond na Mrisho Mpoto lakini sio wakina Jangala na Pembe.Wengine wameishia kufa vifo vya aibu kutokana na kukosekana kwa misingi na sheria zakuwalinda. Kilichopo ni kuwapa kwa mkono huu na kuwanyang’anya kwa mkono ule.
HITIMISHO
CCM haina jambo jipya la kutudanganya Watanzania kuwa tukiweke tena madarakani. Wakati umefika CCM ipumzike ili ijitafakari na kujipanga kwa wakati mwingine. Viongozi wamepoteza dira na chama kimepoteza mwelekeo. Hawazungumzi lugha moja tena na walio wengi wamekwama kwenye tope kubwa na hawawezi kujikwamua. Wanahitaji MABADILIKO ya UHAKIKA.Na UKAWA ndio mwisho wa MABADILIKO.
 
Back
Top Bottom