Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Halafu ili ujue hawa ccm wanadharau na ni wakati wao kupumzika,watuhumiwa wale wale wa escrow ndio wameteuliwa na chama tena kugombea ubunge.
 
Hapaeleweki hatua kidogo pale TAMISEMI. Wakurugenzi Wengi wameondolewa kwa chuki na bila sababu za kueleweka. Inashangaza mtumishi wa serikali kuondolewa bila kufuata sheria ya utumishi wa umma na kanuni zake. Mimi nadhani huyu Katibu Mkuu atakaa pale TAMISEMI Milele.
:amen::amen:
 
Huyu magufuli hana jipya wizara yake ya ujenzi imefeli, wakandarasi wanaidai serikali mpaka wengine wamekufa kwa presha kwa madeni kwenye mabenki halafu eti ndio jembe? Huyu ndio mchapakazi wa ccm wizara imemshinda nchi ataiwezaje? Magufuli angejitazama kwanza ndio aanze kampeni hafai hafiti ni janga lingine nchi hii.
 
Wakuu salaam sana!
Kama mjuavyo ccm imezindua ilani ya uchaguzi inayoonyesha namna ya kuwadanganya tena watanzania kwa kupindi kungine cha miaka mitano! Kiukweli hii sio ilan ila ni laana kwa watz. Mfano kuna kipengele kinazungumzia kujenga hospital tatu kubwa za rufaa kanda ya kusini, kuboresha kilimo kupitia sera ta kilimo kwanza. Hizi ni baadhi tu ya mambo ya kusadikika yaliyoanishwa kwenye hii ilani. Bila kuwa shabiki, hizi porojo kwa watanzania. Hakuna mahali popote pameandikwa mtanzania atamiliki rasilimali zaidi ya kusema kuwa itafufua viwanda.

Sijaweza kuiattach hapa, ila wataalam wanaweza kuipakuwa ili wadau wote waisome na wajipime kisha wafanye maamuzi.
 
Wewe ndio umepiga porojo kwa kutoeleweka unachosema. Ilani ya CCM imejitoshekeza na tingatinga lipo la kuitekeleza. Mzee aliyedhoofika kiafya hatumtaki.
 
Wanazindua Campaign Na Ilani Mpya Kwani Ile ya 2010-215 Wametekeleza zile Ahadi za Kisanii Zipatazo zao 450;Ebu Mwenye

Kumbukumbu Nazo Hatuwekee Hapa tupige Asilimia ya Utekelezaji kama sio tu Chini ya 2o%.
 
Dar es Salaam. Wasomi na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na uchumi nchini wamekuwa na maoni tofauti juu ya Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Maoni hayo yaliyotolewa jana baada ya gazeti hili kuchapisha habari iliyotaja vipaumbele vya chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo vilivyo katika ilani yake ya 2015-2020.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Profesa Gaudence Mpangala alisema ilani hiyo imetoa mpango mzuri lakini akatahadharisha kuwa ahadi zilizotolewa zimejirudia kwa kuwa zilikuwamo pia katika awamu mbili zilizopita.
Alisema kitu cha msingi kwa chama hicho ni kubainisha mazingira na kuyafanya kuwa rafiki kwa utekelezaji ya mipango hiyo na kuzifanya rasilimali zilizopo ziwanufaishe wananchi badala ya mataifa ya nje ambayo yananeemeka zaidi kwa wakati tulionao. “Tusipobadili mfumo, bado hatuwezi kunufaika na vyote tulivyonavyo. Uchumi hauwezi kuimarika kama hatuna viwanda, Serikali na wajasiriamali wajikite huko ili kuongeza thamani ya bidhaa zetu. Miaka 50 baada ya uhuru bado jembe la mkono linatumika licha ya ahadi nyingi zilizotolewa katika chaguzi zilizopita,” alisema Profesa Mpangala na kuongeza kuwa: “Ahadi ya kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia rushwa na uhujumu uchumi bado siyo hitaji kwa sasa. Rais (Benjamin) Mkapa wakati anaingia madarakani mwaka 1995 alitoa ahadi kama hiyo na akaunda tume iliyoelezea kiwango cha rushwa nchini na kuishauri Serikali juu ya hatua stahiki za kuchukua.”
Profesa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Peter Kopoka aliisifu Ilani ya CCM kuwa akisema imekaa vizuri kwani imegusa maeneo yote muhimu kwa wananchi na Taifa kwa ujumla ila akasisitiza usimamizi wa dhati wa mipango yote iliyobainishwa ili kupata matokeo yanayohitajika.
Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa Hakielimu, Godfrey Bonaventure alisema kwenye kipengele cha elimu, CCM haijawa makini kwani haijajikita kwenye mahitaji yaliyopo, badala yake imerudia kilichosemwa kwenye Sera Mpya ya Elimu iliyozinduliwa hivi karibuni.
“Nimesikitishwa kuona kuwa mpaka leo bado CCM wanajikita kwenye udahili na ufaulu wakati hoja ya sasa ni ubora wa elimu inayotolewa kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu. BRN na hata Sera Mpya ya Elimu imezungumzia juu ya masuala hayo mawili, tunachohitaji kuona ni mikakati ya kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia,” alisema Bonaventure. Alitaka suala la ubora liangaliwe pia kwenye maeneo mengine akitolea mfano wa ujenzi wa zahanati kila kijiji: “Ni aibu kuwa miaka 50 baada ya uhuru bado tunahangaika na kipindupindu, ugonjwa ambao hauzungumzwi kwingineko duniani. Ingekuwa vyema kama wangetueleza zahanati hizo zitajengwa kwa viwango gani. Afya na elimu ni mambo magumu tofauti na ujenzi wa miundombinu ambayo ukiwa na fedha za kutosha basi mradi unakamilika.”
Ilani hiyo imetoa takwimu ambazo kwa kipindi cha miaka mitano ni lazima zifanyiwe kazi, mfano kuongeza udahili wa kidato cha kwanza kutoka asilimia 60 mpaka 80 huku ufaulu wa kidato cha nne ukiongezeka kutoka asilimia 69.8 mpaka 90, mambo ambayo Profesa Tolly Mbwete alisema hayakidhi mahitaji.
“Tehama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) inapaswa kuwafikia wananchi wote. Kama fedha hazitoshi ni vyema Serikali ikakopa ili kuweka mazingira wezeshi badala ya kutowafikia baadhi ya watu wake. Na kwa nini udahili wa kidato cha kwanza ni asilimia 80 badala ya 100? Nadhani haya ni malengo madogo kwa Taifa ndani ya miaka mitano ijayo,” alisema huku akihoji Profesa Mbwete.
Mhadhiri Mwandamizi wa UDSM, Dk Benson Bana alisema haoni jipya kwenye vipaumbele vilivyobainishwa na kusisitiza kuwa jambo muhimu kwa Serikali ni kubadilisha mtazamo uliopo miongoni mwa Watanzania ili waondokane na uvivu kwa kurudisha miiko na maadili ya watumishi serikalini na kuongeza uwajibikaji.
 
Wewe ndio umepiga porojo kwa kutoeleweka unachosema. Ilani ya CCM imejitoshekeza na tingatinga lipo la kuitekeleza. Mzee aliyedhoofika kiafya hatumtaki.

Kama hujaelewa mbona umejibu mkuu?
 
Issues Hapa si Uzuri wa Ilani, issue Hapa Je Wana-Moral Authority ya Kuyatekeleza. Jibu Ni Hapana,Haya ni Maneno Matupu

Yasiyokuwa na Uhalisia wala Matunda. Ni Kipindi Kingine kwa Watanganyika Kudanganywa na Masisiem. Tuspochukua Hatua ya

Kuwakataa Waziwazi basi Tumekwisha.
 
Toeni na nyie ilani ya ukawa tuione acheni kubwabwaja

Kwa umri CCM ilio kaa madarakani haistahili kuja na ilani ya uchaguzi, inatakiwa ije ituambie yale maiaha bora yako wapi? Ukweli kuhusu Escrow ni upi? Kwanini wameahindwa kuzuia rushwa? Kwanini wanafunzi bado wanakalia mawe?? Kwanini watumishi wa umma bado wanidai serikali? Kwanini shilingi inaporomoka? Kwanini hakuna dawa hosipitali? EPA vipi? MEREMETA vipi? Twiga kupanda ndege imekaa je???...........
 
this time hata Bana amewananga, kweli mwaka huu wataona kila rangi
 
kama imewezakana kujengwa UDOM na sasa muhimbili mpya kule lugeza... kipi cha ajabu kujengwa hizo hosipital huko kusini? Just thinking. ukiweka ushabiki pembeni vitu vingine ni rahisi tu.

Wakuu salaam sana!
Kama mjuavyo ccm imezindua ilani ya uchaguzi inayoonyesha namna ya kuwadanganya tena watanzania kwa kupindi kungine cha miaka mitano! Kiukweli hii sio ilan ila ni laana kwa watz. Mfano kuna kipengele kinazungumzia kujenga hospital tatu kubwa za rufaa kanda ya kusini, kuboresha kilimo kupitia sera ta kilimo kwanza. Hizi ni baadhi tu ya mambo ya kusadikika yaliyoanishwa kwenye hii ilani. Bila kuwa shabiki, hizi porojo kwa watanzania. Hakuna mahali popote pameandikwa mtanzania atamiliki rasilimali zaidi ya kusema kuwa itafufua viwanda.

Sijaweza kuiattach hapa, ila wataalam wanaweza kuipakuwa ili wadau wote waisome na wajipime kisha wafanye maamuzi.
 
Tukiacha mipasho, vijembe na zomea zomea pamoja na minenguo ya burudani nzuri, haya ndo mambo yatakayo mpaisha Dr John Pombe Magufuli.

Issues za JP Magufuli in Summary:
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za mwana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa

UKAWA waje na mbadala tuone.
 
UKAWA sije ingia mtego w kujibu mipasho.
Ila hapo namba tano, sijui kama wale wa ESCROW na RICHMOND wataingia hapo.
 
Hivyo vyote tulishaaidiwa na hicho chama ndugu hakuna ahadi mpya hapo tena ahadi za zamani zilikua tamu masikioni kuliko hizo,Tanga tuliambiwa litakua jiji la viwanda miaka mitano.iliyopita but mpaka leo hakuna kiwanda kilichoongezeka
 
Uchaguzi mkuu 2010 uliwapanikisha sana CCM. Walidhani kuporomoka kwao kisiasa ni kwa sababu ya hoja ya wapinzani ya katiba mpya. Kikwete akaanzisha mchakato wa katiba mpya, japo haikuwepo kwenye ilani yao. WanaCCM wenzake wakajenga hasira. Lakini kama mjuavyo mchawi hajifichi. Katiba mpya ilikwama mikononi mwao asubuhi na mapema. Hawataki kusikia katiba mpya. Wanaona kwenye katiba mpya ilijaa chuki za wananchi dhidi ya utawala wao. Wakatupa chooni ile rasimu ya wananchi. Katiba mpya haikupatikana hadi leo.

Katiba mpya ndio chimbuko la UKAWA, ambao sasa wameenda mbele zaidi hadi kuachiana majimbo na nchi. Nina uhakika ilani ya kwanza ya ukawa mwaka huu 2015 ni katiba mpya, halafu nyingine zinafuata. KATIBA MPYA ndio iliyowaunganisha wapinzani.

Ilani ya CCM haizungumzii katiba mpya kwa sasa. Hio hoja imekufa rasmi. Sijui wanadhani wananchi hawana shida tena na katiba mpya, sijui.

Bahati mbaya sana wamelala na bundi. Aliekwamisha katiba mpya kama mwenyekiti naye ni mmoja wa timu ya kampeni ya ccm. Tulianza na Mungu, tutamaliza na Mungu! Bahati mbaya nyingine zaidi kuliko yote kiongozi mwenza katika kukwamisha katiba mpya, ni mgombea mwenza mbio za urais. Tulianza na Mungu! Tutamaliza na Mungu!

Huyu mama yeye huwa ni mwenza tu. Akiwa mwenza katiba mpya ilikwama. Hata sasa akiwa mwenza urais, urais pia utakwama!
 
Back
Top Bottom