Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tukiacha mipasho, vijembe na zomea zomea pamoja na minenguo ya burudani nzuri, haya ndo mambo yatakayo mpaisha Dr John Pombe Magufuli.
Issues za JP Magufuli in Summary:
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za mwana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa
UKAWA waje na mbadala tuone.
Kwani lazima ya UKAWA iwe mbadala? Haikubaliki ilani kufanana maudhui? Kama UKAWA wangeanza kutoa ilani yao kama hiyo, CCM wangeibadili hii? Hivi kuna watu bado wanaamini katika ilani? Mbona vyama vyote tu vina ilani nzuri tu? JK alitekeleza mambo yasiyomo kwenye ilani ya CCM mfano Katiba mpya, akayaacha yaliyo katika ilani ya CCM mfano Mahakama ya Kadhi. Je, alifanya vibaya?UKAWA waje na mbadala tuone.
CCM ni mabingwa wa jadi wa ahadi zisizotekelezeka.
Pekuapekua ahadi za Jakaya Kikwete uone aliyoahidi na aliyotekeleza.
CCM ni rangi ile ile mkuu masopakyindi.
Shtuka!!
Nilishangaa kusikia kuna div 5, na nlisikitika kuona waziri wa elimu hajui kusoma wala haijui nchi yake!!! Nlihuzunika kuona twiga wanapandishwa ndege...bila kusahau uharamia wa pembe za ndovu!!! Wizi wa fedha za serikali...utumiaji wa mabavu na vyombo vya ulinzi!!
Kwa kuongezea tu, 1usd=2000+ tsh!!!
HII YOTE NI BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 50 YA UHURU!!! WE NEED UKAWA NOTHING ELSE.
Cc baro The Tomorrow People na wooote ambao wanajidanganya ccm ndio jibu la shida za wa tz.
Mkuu Roma na barabara zake safi haikujengwa siku moja.CCM ni mabingwa wa jadi wa ahadi zisizotekelezeka.
Pekuapekua ahadi za Jakaya Kikwete uone aliyoahidi na aliyotekeleza.
CCM ni rangi ile ile mkuu masopakyindi.
Shtuka!!
Vizuri sana tena sana!Yote yaliyopo katika ILANI YA CCM yanayoweza kutekelezeka hayo ya itifaki, mishahara ya viongozi, posho, magari ya kifahari na nk.
Kwa sababu serikali chini ya ccm haijawahi kumpa mlipa kodi kipaumbele ndio maana daima maslahi yao mbele. Moja ya kielelezo kuwa tunalipa kodi kwa ajili ya maslahi kwanza viongozi jinsi wanarukiana vichwa kama mbuzi, rushwa na hujuma kupata nafasi za ubunge.
Hakuna litalowezekana isipokuwa kupitia kodi tutazolipa sisi wenyewe, hivyo maendeleo ni haki yetu sio zawadi au hisani.
Kwa maana mikopo yote tutalipa kwa kodi zetu watanzania wanyonge, si mnajua mwalimu unalipa kodi kupitia mshahara wako mdogo lakini wabunge, mawaziri, rais halipi kodi japo mishahara yao kwa mwezi ni mshahara wa mwalimu miaka miwili na nusu.
Angekuwa mjanja angeainisha vyanzo vya mapato vya kutekelezea ahadi hizo, kama hana basi amfuate January Makamba !Kusema ukweli Magufuli anaweza maana siyo mwanasiasa. Naamini atafanyakazi kurudisha heshima ya ccm
Tingatinga lazima awahenyeshe safari hii
Ulizaliwa enzi za chai maharage, huoni mbadiliko?Tunatakiwa tuweke thread ya Sera za CCM Tangu Mfumo wa vyama Vingi kuanza.Wale wenye kumbukumbu watusaidie.Mimi binafsi naona marudio,hizo zimeendelea kuwa fimbo za kumchapa mpumbavu na Lofa.Wameanza Goli la mkono,wakaenda na kusema ni makapi waliohama CCM,hawakuishia hapo wanaendelea kusema Oil chafu na msumari wa kwanza wa aliyewahi kuwa mkuu wa kaya anaongea kwa nguvu kubwa tena ya kujiamini!!! Wapumbavu na Malofa!! Tumewavumilia sanaa,this is too much.
Kwa nondo hizi lazima UKAWA wakae