CCM HAINA TENA WABUNIFU NA ILANI YAKE IMEDHIHIRISHA KUCHOKA KWA CCM.
TUIPUMZISHE.
katika taasisi yoyote lazima kuwepo na magwiji wa ubunifu,mikakati mizito na stadi. hawa kwa kimombo wanaitwa THINK TANKS.
kwa mara ya kwanza kabisa nimeshuhudia CCM ikifeli kwa kila kitu.
kuanzia kauli mbiu ya CCM mwaka huu. nimeona Magufuli akisema wao ni KAZI TU.
ilani ya CCM kwa kadri ilivyoelezwa.
ELIMU:
Itakuwa bure kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.
hakuna matumaini ya kuifanyia mapinduzi elimu yetu iliyodorora kabisa huku ikikumbwa na matatizo lukuki kama ukosefu wa mazingira stahiki ya kujifunzia na kujisomea, ukosefu wa mabweni mashuleni, ukosefu wa maji mashuleni, ukosefu wa vifaa vya kujifunzia ikiwemo vitabu na vifaa vya maabara,ukosefu wa umeme mashuleni.
eti CCM imeishia kuahidi elimu bure mpaka kidato cha nne katika mazingira hayahaya ya shule za kata ambazo hazina umeme,hazina mabweni,hazina vitabu, hazina maji, hazina nyumba za walimu nk.
CCM haina tena magwiji wenye uwezo wa kulisaidia taifa hili.
elimu nchini Tanzania ipo katika mdororo usioelezeka na kunahitajika mipango madhubuti ya kuifanyia mapinduzi elimu yetu ili iwe ya kisasa zaidi na yenye kuakisi ubora wa juu kabisa ndani ya miaka kumi ijayo. CCM imefeli kabisa na kudhihirisha kuwa imechoka sana kwa ilani hii ninayodiriki kuiita kuwa ni ilani isiyostahili kupelekwa kwa wananchi.
UCHUMI.
nchi kwa sasa inahitaji mipango na mikakati makini ya kulifanya taifa lipige hatua kubwa katika maswala ya TEKNOLOJIA NA VIWANDA ili kulifikisha taifa katika mapinduzi ya viwanda katika miaka isiyopungua 30 ijayo. naona hapa ccm haina kabisa mpango wala mkakati wowote wa kueleweka.
mimi Joseph Mshinga sipo tayari na sitakuwa tayari kuunga mkono ilani yoyote katika kipengele cha UCHUMI ikiwa hakuna mpango wenye matumaini ya kulifanyia mapinduzi ya viwanda taifa letu. Hatuwezi kuwa taifa la kuombaomba miaka yote. CCM katika kipengele hiki wanaomba wapewe kuiongoza nchi kwa staili ileile ya kuombaomba na kukopa. Kibaya zaidi wanaendeleza mazingira ya kulifanya taifa letu liendelee kuwa la kuombaomba,kukopa na tegemezi ili tuendelee kuuza madini na kila aina ya utajiri wetu kwa mikataba ya bei ya pelemende kwa kuwa hatuna teknolojia. CCM mpaka sasa ni chama cha ujamaa lakini katika ilani yao hakuna ujamaa uliowekwa na wala hakuna ile kauli maarufu ya ujamaa na kujitegemea lakini naona hapa ccm inatuhakikishia kuendelea kulifanya taifa letu kuwa tegemezi badala ya kujitegemea.
#HILI HALIKUBARIKI# kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo tuikatae katakata CCM isiendelee kutuharibia taifa letu.
sisi tunahitaji taifa ambalo ifike muda madini yetu tuchimbe wenyewe kwa teknolojia yetu wenyewe, tutengeneze bidhaa zetu wenyewe kutokana na raslimali asili zetu kwa teknolojia yetu na kwa viwanda vyetu. CCM haina kabisa think tank kwa sasa. Ilikuwa miaka ya 70(1970s) wakati ambapo viongozi wa wakati ule waliamua kuanzisha viwanda vya kila aina katika kila kona ya nchi ili kuuishi uchumi halisi. leo ccm haina tena uwezo huo na wala historia hawaikumbuki tena.
CCM THINK TANK HAS BROUGHT THIS VERY POOR MANIFESTO EVER SEEN IN TANZANIA GENERAL ELECTION.
hotuba ya Magufuli imejikita katika kuongelea matatizo madogomadogo ambayo ni ya kiutendaji na majibu ya kutaka na kutatua matatizo ya watanzania hayamo katika ilani ya CCM. TUIKATAE CCM.
tunahitaji uchumi imara utakaofanya yafuatayo.
1.uchumi utakaoruhusu darasa la saba kuwa na ajira zinazoendana na elimu yao kwa kuwa siyo kila mtanzania atasoma zaidi ya darasa la saba.
2.uchumi utakaoruhusu na kuwahakikishia wenye elimu ya kidato cha nne nao kupata ajira kulingana na elimu yao maana si kila mtanzania ana ndoto za kusoma zaidi ya kidato cha nne. Wengine elimu ya form four inawatosha kwa matakwa yao lakini lazima tuwe na uchumi unaowahakikishia kundi hili ajira ili waweze kuendelea na maisha yao.
3.uchumi utakaowahikishia kidato cha sita kupata ajira zinazolingana na elimu yao na ujira unaolingana na elimu yao. siyo lazima kila mtanzania afike chuo kikuu lakini tuna wajibu kama taifa kuhakikisha kila kiwango cha elimu kinaingia kwenye mfumo wa ajira kwa kulihakikishia kundi husika kupata kazi/ajira ili kila mtu aishi kwa kazi yake.
4. uchumi utakao wahakikishia wenye elimu ya chuo kikuu kupata ajira na ujira unaolingana na elimu yao.Kwa mazingira ya sasa hata wenye degree hawana uhakika wa kupata ajira. kwa mantiki hiyo hata wenye elimu ya chini wengi wanalazimika kujitahidi wafike chuo kikuu ili kwa kiasi fulani waweze kupata jira lakini bado hata degree haimhakikishii mtanzania kupata ajira hata ile ya kinyonyaji. Tunahitaji uchumi wa kutoa ajira kwa kila kundi.
5.tunahitaji uchumi wa kulifanyia mapinduzi taifa katika sekta ya elimu,afya, miundombinu nk.
uchumi ukiwa imara watanzania watafanya mambo mengine wao wenyewe kupitia vipato vyao halali.
mfano.
#mtu mwenye kazi na mshahara hahitaji kusomeshewa mtoto wake bure. kwa hiyo wazazi wengi wakiwa na kazi zao wanaweza kuwapeleka watoto wao shule kwa gharama zao. Umasikini ndio unawafanya watanzania wahitaji usaidizi kutoka serikalini katika kusomesha watoto wao lakini kama wakiwa na kazi kila mtu ataweza kumsomesha mtoto wake na kumudu gharama zinazohitajika.
#wakiwa na kazi kila mtu anaweza kumudu kujenga nyumba yake ya kawaida na kuishi maisha anayoyataka.
nk nk nk nk.
kwa sasa ni sahihi kuwa baadhi ya mambo yanahitaji usaidizi wa serikali kabla uchumi haujasimama na kumuwezesha mtanzania kugharamia mwenyewe gharama hizo kupitia ajira yake. Mambo hayo ni pamoja na kuifanya elimu kuwa ya bure mpaka chuo kikuu ili kila mtanzania mwenye uwezo na nia ya kuifikia elimu ya juu asome na kufika huko bila kujali kama ni watoto wa matajiri ama wa masikini. kwa mantiki hii elimu ya bure bado ina umuhimu mkubwa katika mazingira ya sasa.
TUIKATAE CCM ILI KULIOKOA TAIFA.
NA:
JOSEPH NGIKILI MSHINGA
@(visioned to industrial revolution)@