Hakuna kitakacho fanyika chini ya ccm, ahadi ni zilezile tangu nchi ipate uhuru, maadui ni walewale ujinga umaskini na maradhi, tena maradhi mengine yamesabaishwa na ccm kama kipindupindu, watu wanakosa maji safi na salama matokeo yake wanahara hovyo tu, halafu mtu kutoka nyumba hiyohiyo anakuja sema atayamaliza na alikuwa sehemu ya serikali, upuuzi tu, magufuli aliuza nyumba kwa bei ya kutupa halafu wanakuja jenga nyingine kwa garama za kutisha ndio mtu makini aliebaki ccm? Sie malofa kwa sabab tumefanywa malofa na chama tawala, wao mamwinyi kwa sababu wamejifanyia hayo kwa kura tulizo wapa, sie wapumbavu kwa kuwaweka ikulu miaka 50 wakati kila muongo ahadi ni zilezile hazitekelezwi, leo magufuli aje na kipi kipya, walewale tu.