Uchaguzi 2020 Ilani ya CHADEMA kuhusu Bima ya Afya ina ulaghai

Uchaguzi 2020 Ilani ya CHADEMA kuhusu Bima ya Afya ina ulaghai

Kwa uelewa wangu SERA ndio huzaa sheria ambazo hutumika kutekeleza SERA. Takwimu za kiasi cha kulipa kitaletwa na sheria husika.

Jambo la msingi kwenye hiyo SERA YA CHADEMA ni kuwaingiza watanzania wengi iwezekanvyo ili "premium" iwe ndogo.
 
Mimi Nataka nikuelemishe juu ya jinsi bima ya Lissu itakavyofanya na funding yake itakuwaje.

Nisaidie je unafikiri pesa kiasi gani kinatakiwa kuweza kuendesha mfumo mzuri wa afya Tanzania?

hapo ndio tutaanza mjadala mpaka zaidi
 
Mkuu wewe ndio mweupe sana kwenye uchumi eti una compare GDP ya Belgium na Tz ili useme haiwezekani? Sasa nikupe challenge.

Model ya bima ya afya wametohoa Rwanda ina hiyo special package ya Jeshi alafu kuna wafanyakazi wa umma, then kuna wale wenye kipato cha chini kabisa wasio kwenye sekta rasmi n.k

2. Justification yake ni kwamba michango inategemea income bracket uliyopo. Rwanda wameigawa mara 4 kwahiyo utachangia kulingana na uwezo wako wa kiuchumi lakini wale waliopo chini kabisa yaani wanaoishi kwenye umaskini wa kutupwa basi serikali inawachangia totally wakishirikiana na mfumo wa crowdfunding wa kijamii tunaweza uita "Ujirani mwema"

3. Mchango wa serikali ya Rwanda ni almosy 14% pekee kwahiyo haiathiri mapato ya Serikali kabisa kwenye kuendesha mfuko.

4. Usichofahamu ni kwamba mfuko ukiwa na pesa zinazungushwa kwenye biashara mbalimbali na masoko ya hisa hivyo pesa inazaa ili mfuko uwe unakua zaidi na kupunguza risk ya float.

5. Unasema GDP ya Belgum blah blah, sasa naomba ufaham Tz imeizidi GDP ya Rwanda karibu mara 6.7 kwa data za 2018. Sasa kama Rwanda kufikia 2011 walikua na coverage ya 90% bima ya afya sisi tunashindwa nini??

Tusiishi kwa kukariri tujifunze Rwanda tupunguze ujuaji.
Na ukumbuke population ya Rwanda na Tz ni tofauti sio unachongoa mdomo tu
 
Mimi Nataka nikuelemishe juu ya jinsi bima ya Lissu itakavyofanya na funding yake itakuwaje.

nisaidie je unafikiri pesa kiasi gani kinatakiwa kuweza kuendesha mfumo mzuri wa afya Tanzania?

hspo ndio tutaanza mjadala mpaka zaidi
Ukienda NHIF watakupa vipeperushi vinavyoonyesha aina mbalimbali za bima . kulingana na uwezo wako. Kama unahitaji tembelea ofisi zao.

Huduma zinazozotolewa sasa ni bora mfano mimi natibiwa hospitali zenye hadhi kama Hindumandal na vipimo vikubwa nafanya kwa kutumia bima hiyohiyo.
 
Vip ya CCM inasemaje kuhusu afya mbona Magufuli katoa ahadi kwamba bima ya afya inakuja je ipo ndani ya ilani?
 
Soma vizuri uelewe hoja yangu kisha ujibu accordingly. Kama kila mtanzania atapata bima inayomuwezesha kupata huduma bora kwa nini kuwe na bima maalum kwa ajili ya askari? Huoni hapo tayari kuna tofauti ya huduma. Je huyo mtanzania mwenye hiyo bima atatibiwa Hindu mandal au Aga khan au ataishia hospitali ya wilaya?
Msingi wa hoja yangu ni kuwa kipato binafsi cha mtu ndicho huamua akate bima ya aina gani, atibiwe wapi, mtoto wake asome wapi siyo blah blah.
Mpaka sasa nimepost uzi aina tatu soma zote ujibu hoja kwa hoja.

Wewe ni bado mweupe kama ulivyoambiwa. Tatizo la bima ya Tanzania kwa sasa ni kuwa penetration ya bimani ndogo hivyo wanaochangia bima kuwa wachache kupelekea kuwa ghali. Kama watu wengi wangechangia bei ya bima ingeshuka kwa maana mahitaji ya Huduma ya afya yangetoka kwenye kundi dogo kutokana na kundi kubwa linalochangia.

Kuwa na affordable insurance ni issue tu ya priorities, sera na utashi wa kisiasa lakini linawezekana kabisa.Chaumma walisema hilolinawezekana na walitoaoption ya serikali kutoa % ya kodi za simu za mkononi kuchangia bima. Mbona REA imezekana kutokana na tozo zilizowekwa kwenye mafuta? Kwa nini isiwe bima?
 
KWA UJUMLA WAKE NI KWAMBA CHADEMA HAWANA SERA NZURI WATATUHARIBIA NCHI JPM JEMBEEE
 
  • Thanks
Reactions: RMC
wewe ni bado mweupe kama ulivyoambiwa. Tatizo la bima ya Tanzania kwa sasa ni kuwa penetration ya bimani ndogo hivyo wanaochangia bima kuwa wachache kupelekea kuwa ghali. Kama watu wengi wangechangia bei ya bima ingeshuka kwa maana mahitaji ya Huduma ya afya yangetoka kwenye kundi dogo kutokana na kundi kubwa linalochangia. Kuwa na affordable insurance ni issue tu ya priorities, sera na utashi wa kisiasa lakini linawezekana kabisa.Chaumma walisema hilolinawezekana na walitoaoption ya serikali kutoa % ya kodi za simu za mkononi kuchangia bima. Mbona REA imezekana kutokana na tozo zilizowekwa kwenye mafuta? Kwa nini isiwe bima?
Wewe na wenzako ndio hamjui kitu. Nyinyi mnadai laki sita kwa mwaka ni nyingi lakini hamtaki kusema bima yenu ya unafuu itakuwa shilingi ngapi! Mnadai hadi mshinde ndipo mtapanga bei baada ya kuunda serikali na kupitisha sheria.

Sasa wakati huo mkigundua kuwa ili kutoa huduma bora ya bima premium inatakiwa iwe laki nane ambayo ni ghali kuliko ile ya sasa mnayoibeza kwa na huku tumeishawapa kura kwa ahadi isiyotekelezeka si mtakuwa mmetuingiza chaka.

Unadai mtatoa bima nafuu wakati hujui itakuwa nafuu kiasi gani! Shame on you.

Unapotoa ahadi ya uchaguzi unatakiwa uwe na uwezo wa kuifafanua na kuitekeleza.
 
Kwa hiyo wewe kazi yako ni kupinga ilani za vyama vya upinzani siyo? Wewe hapo ulipo au jamaa zako wana bima?
 
Kwa hii ilani ya Bima ya afya, CDM nawapa kura na nawaombea kura kwa ukoo wangu wote!
 
Hiyo ni bima ya matabaka na wala sio muundo mzuri.
Ni tofauti na bima ambayo Lissu anaiongelea ya Belgium.

kwanza kuna issue ya economy of scale. Kama kila mtu atakuwa na bima, bei yake itashuka sana.

kwasasa wenye bima ni kama milioni mbili tu katika nchi ya watu karibu milioni 60.

Nilivyo mwelewa Lissu, kama bima ya afya itakuwa lazima kama ilivyo lazima kulipa kodi. Watanzania milioni 20 wanaweza kukata bima. Chukulia bei ya chini kabisa ya laki moja kwa mwaka. Hiyo unapata trilioni 2.

Lakini kwasababu watu watalipa kulingana na uwezo wao au mishahara yao kama ilivyo sasa. Ni rahisi kabisa kwa mwaka makusanyo kuwa trilioni tatu ambazo ni zaidi ya bajeti ya wizara ya afya.
Kwahiyo kuna matabaka katika kulipa lakini utumiaji ni ule ule Yaani wagonjwa wote watapata huduma ile ile moja tofauti na sasa ambapo huduma inafuata malipo yako.

tukija kwenye malipo. Vijana wa miaka mitano mpaka 40 Tanzania ni almost asilimia 70 na hawa hawaumwi umwi. Juu ya miaka 40 hawazidi asilimia 15 na hawa ndio wana magonjwa makubwa, na watoto chini ya miaka mitano nao magonjwa Yao ni madogo madogo
Ukiweka bima ya laki moja kwa mwaka kwa watu wenye kipato cha chini hata wafanyabiashara ndogo ndogo wataweza kulipa.

katika kundi la chini kabisa lets say watu milioni tano watalipiwa na serikali, hiyo ni bilioni 500. Hiyo sio pesa nyingi kwa ajili ya afya ya watu kwa mwaka. Hata serikali ikilipa trilioni moja kwa mwaka bado sio mbaya.
Haya mambo ya watu binafsi kuambiwa bima ya maana milioni mbili kwa familia yataisha.

economy of scale itashusha sana bei.

Huo ndio mfumo wa bima wa huko Ulaya. Sio wa matabaka. Matabaka yako kwenye kulipa lakini huduma wote mnapata ile ile.
Ukienda NHIF watakupa vipeperushi vinavyoonyesha aina mbalimbali za bima . kulingana na uwezo wako. Kama unahitaji tembelea ofisi zao.
Huduma zinazozotolewa sasa ni bora mfano mimi natibiwa hospitali zenye hadhi kama Hindumandal na vipimo vikubwa nafanya kwa kutumia bima hiyohiyo.
 
Kama kila mtanzania atapata bima inayomuwezesha kupata huduma bora kwa nini kuwe na bima maalum kwa ajili ya askari? Huoni hapo tayari kuna tofauti ya huduma. Je huyo mtanzania mwenye hiyo bima atatibiwa Hindu mandal au Aga khan au ataishia hospitali ya wilaya?
Wewe una matatizo mawili.
1. Unachambua mapendekezo ya sera ya Chadema ukiwa ndani ya kasha/box la sera dhanifu ya CCM - ninakushauri ujiondoe kwanza kwenye kasha hilo, jiweke huru kisha angalia kwa ufasaha yanayotokea nje.

2. Umeshindwa kutambua assumption kuu ya Bima ya afya (na bima nyingine) kwa watu (makundi rika) wote hawaumwi na kwenda kutibiwa kwa wakati mmoja.

Unatakiwa kujua kwamba iwapo watanzania wengi watakuwa kwenye bima ya afya kila mtu atalipa premium kidogo (affordable) kuliko sasa ambapo watu walio katika mpango wa NHIF ni wachache hivyo kutakiwa kulipa premium kubwa kwa kuwa ni wachangiaji wachache.

Chukua mfano mdogo. Iwapo kila Mtanzania atalipa shilingi elfu 5 kwa mwaka ikiwa ni premium ya mwaka kiasi hiki kinaleta tzs, 5000*60,000,000 (bilioni mia tatu); kila mtamzania akichangia tzs elfu kumi kwa mwaka NHIF itaingiza kiasi cha 10000*60,000,000 (bilioni mia sita). Wanaohitaji accessories za ziada beyond standard health care wataweza kuchagia zaidi. Hii ni dhana ya economies of scale kwenye uchumi na commerce.

Sasa kama serikali imedhamiria mpango huu itashindwaje kuutekeleza? Mpango huu unaweza pia kutekelezwa sambamba na kubadilisha dhima ya sera ya afya ta nchi kutoka kugharimia kuponya wagonjwa wasifariki kwenda kuimarisha huduma za afya ya jamii ili wananchi wawe na afya bora, wasiugue hovyo, hivyo kupunguza mzigo wa gharama za matibabu/dawa na miundombinu ya afya (serikali/NHIF) na kuongeza gharama kwa kila mtu mmoja mmoja kuishi kwa kufuata kanuni za kuwa na afya bora - kula chakula bora, kufanya mazoezi, kuishi katika mazingira bora, kujielimisha zaidi juu ya matakwa ya public health.

Jiondoe kwenye kasha utaelewa tu
 
Hiyo ni bima ya matabaka na wala sio muundo mzuri.
Ni tofauti na bima ambayo Lissu anaiongelea ya Belgium.

kwanza kuna issue ya economy of scale. Kama kila mtu atakuwa na bima, bei yake itashuka sana.

kwasasa wenye bima ni kama milioni mbili tu katika nchi ya watu karibu milioni 60.

Nilivyo mwelewa Lissu, kama bima ya afya itakuwa lazima kama ilivyo lazima kulipa kodi. Watanzania milioni 20 wanaweza kukata bima. Chukulia bei ya chini kabisa ya laki moja kwa mwaka. Hiyo unapata trilioni 2.

Lakini kwasababu watu watalipa kulingana na uwezo wao au mishahara yao kama ilivyo sasa. Ni rahisi kabisa kwa mwaka makusanyo kuwa trilioni tatu ambazo ni zaidi ya bajeti ya wizara ya afya.
Kwahiyo kuna matabaka katika kulipa lakini utumiaji ni ule ule Yaani wagonjwa wote watapata huduma ile ile moja tofauti na sasa ambapo huduma inafuata malipo yako.

tukija kwenye malipo. Vijana wa miaka mitano mpaka 40 Tanzania ni almost asilimia 70 na hawa hawaumwi umwi. Juu ya miaka 40 hawazidi asilimia 15 na hawa ndio wana magonjwa makubwa, na watoto chini ya miaka mitano nao magonjwa Yao ni madogo madogo
Ukiweka bima ya laki moja kwa mwaka kwa watu wenye kipato cha chini hata wafanyabiashara ndogo ndogo wataweza kulipa.

katika kundi la chini kabisa lets say watu milioni tano watalipiwa na serikali, hiyo ni bilioni 500. Hiyo sio pesa nyingi kwa ajili ya afya ya watu kwa mwaka. Hata serikali ikilipa trilioni moja kwa mwaka bado sio mbaya.
Haya mambo ya watu binafsi kuambiwa bima ya maana milioni mbili kwa familia yataisha.

economy of scale itashusha sana bei.

Huo ndio mfumo wa bima wa huko Ulaya. Sio wa matabaka. Matabaka yako kwenye kulipa lakini huduma wote mnapata ile ile.
Kwanza idadi ya kaya ambapo ndio unit ya kuchaji malipo ya bima, haizidi milioni nane hivyo hiyo edtimation yako kwa kubase milioni 20 haiwezi kukaribiana na uhalisia. Hivyo mapato yatakuwa pungufu ya hayo.

Pili uwezo wa kuchangia. Kumbuka kuna bima za CHF ambapi makato ni sh 30,000 lakini bado kuna upinzani kwa kuonekana ghali. Rejea vitambulisho vya machinga sh 20,000 ambapo Lissu mwenyewe anasema ni ghali sembuse bima ya laki moja. Uwezo wa kutoa ruzuku una mipaka, unaweza kuona ni hela kidogo lakini ukianzia kwenye makusanyo ya mapato kwa mwezi ukatoa midhahara na kulipa madeni kinachobakia hebu kiangalie. Sasa hapo ndipo ugharamie sio tu bima bali matumizi mengine kama elimu, nk ndipo mtihani unapokuja.

Kinachowezekana kwa serikali yeyote itakayokuwepo madarakani ni kuendelea kupanua wigo wa bima lakini haitawezekana kila mtu akatibiwa katika first class hospital bado premium utakayolipa itakuwa determinant kubwa wapi utibiwe na matibabu yapi upate.

Uelewe kuwa bima sio kila kitu bado kuna bajeti ya sekta ya afya ambayo ndiyo hasa hutumika kufanya investment katika sekta hiyo na ndiyo yenye kufanya huduma ziwe bora. Hivyo ubora utaendelea kuwa huu huu . Katika uzi wangu nilitolea mfano Ubelgiji ambapo bajeti ya sekta ya afya ni kama asilimia10 ya GDP sasa ukichukulia idadi yao ndogo ya watu na ukubwa wa GDP yao unaweza kuona kabisa kuachieve huduma bora ya afya sio suala la bima tu. It is more than that.
 
kwanza hilo la wananchi kuwa wabishi kuchangia ni kwasababu hawaoni faida ya hizo bima na Pia elimu sio kubwa.

lakini kama hiyo bima itamwezesha mlipaji kutibiwa hospitali zote Tanzania na kuhakikishiwa dawa kwa asilimia 100. Nina uhakika watu wengi watalipa.

kaya zinaweza kuwa milioni 8. Lakini kuna familia Baba na mama wanafanya kazi wote. Bima ikiwa kama kodi hawa wote watalipa. Pia Kuna vijana wengi ambao hawana familia nao watalipa. Hata kama haifiki milioni 20 kakini milioni 15 inaweza ukijumlisha na wale wa hali ya chini ambao serikali itawalipia.

muhimu kuliko vyote ni kuondoa matabaka kwenye matibabu.
Hiyo bima ya elfu 30 ni mbovu kabisa. Huwezi tibiwa hata hospitali ya rufaa. Ndio maana watu wengi hawataki kujiunga.

Uingereza ina watu karibu milioni 67. Huduma ya afya ni bure kwa kila mtu na madawa guarantee asilimia 100. Finding yake inapitia kwenye kodi. Wenye pesa nyingi wanalipa zaidi na wasio na pesa serikali inawalipia.

Kwahiyo kwa kutumia economy of scale kama nilivyoelezea hapo juu inawezekana kabisa. Ni suala la kuamua tu.
Kwanza idadi ya kaya ambapo ndio unit ya kuchaji malipo ya bima, haizidi milioni nane hivyo hiyo edtimation yako kwa kubase milioni 20 haiwezi kukaribiana na uhalisia. Hivyo mapato yatakuwa pungufu ya hayo.

Pili uwezo wa kuchangia. Kumbuka kuna bima za CHF ambapi makato ni sh 30,000 lakini bado kuna upinzani kwa kuonekana ghali. Rejea vitambulisho vya machinga sh 20,000 ambapo Lissu mwenyewe anasema ni ghali sembuse bima ya laki moja. Uwezo wa kutoa ruzuku una mipaka, unaweza kuona ni hela kidogo lakini ukianzia kwenye makusanyo ya mapato kwa mwezi ukatoa midhahara na kulipa madeni kinachobakia hebu kiangalie. Sasa hapo ndipo ugharamie sio tu bima bali matumizi mengine kama elimu, nk ndipo mtihani unapokuja.

Kinachowezekana kwa serikali yeyote itakayokuwepo madarakani ni kuendelea kupanua wigo wa bima lakini haitawezekana kila mtu akatibiwa katika first class hospital bado premium utakayolipa itakuwa determinant kubwa wapi utibiwe na matibabu yapi upate.

Uelewe kuwa bima sio kila kitu bado kuna bajeti ya sekta ya afya ambayo ndiyo hasa hutumika kufanya investment katika sekta hiyo na ndiyo yenye kufanya huduma ziwe bora. Hivyo ubora utaendelea kuwa huu huu . Katika uzi wangu nilitolea mfano Ubelgiji ambapo bajeti ya sekta ya afya ni kama asilimia10 ya GDP sasa ukichukulia idadi yao ndogo ya watu na ukubwa wa GDP yao unaweza kuona kabisa kuachieve huduma bora ya afya sio suala la bima tu. It is more than that.
 
Jaribu kurudia kusama Uzi wangu na post ziliz44ofuatia kuhusu suala hili la bima ya afya. Hebu toka nje ya boksi la ushabiki na uwe critacal kidogo utaona facts.

Kwanza hiyo principle ya bima ambayo kwa lugha rahisi " kusanya kwa watu wengi na uwalipe wachache" naifahamu vizuri tena pengine kuliko wewe. Pili Bima inapopokea premium inawekeza ili iweze kugharimia huduma kusudiwa baadae inafahamika vyema hivyo 8mambo hayo mawili sio mjadala.

Katika ilani yenu na maelezo ya Lissu majukwaani kuna key issue mbili ndizo zimenipelekea kuona mnafanya ulaghai. Issues zenyewe ni kuwa: mtatoa bima nafuu kuliko sasa inavyotolewa na pili huduma za afya zitakuwa bora na mmelinganisha na Ubelgiji.
Maelezo yangu yote yana refute huo ulaghai wenu na nimetumia data na facts kuanalyse hoja zenu.

Premium inawekwa kutaalam zaidi na kwa kila huduma kuna minimum amount lazima ipatikane wingi wa wanachama una limitation yake katika kushusha kiwango cha kuchangia. Nikupe mfano: Bima za nagari huwa hazishuki pamoja na kuwa idadi ya magari inaongezeka sana. Pia ukikata third party ukigonga kwa makosa gari yako hautengenezewi ila uliyemgonga anatengenezewa. Lakini ukikata comprehensive hata kama una makosa gari lako na la mwenzako litatengenezwa na bima.

Maana yangu ni hii kinacholeta utofauti wa gharama za kugharimiwa ni premium uliyolipa sio wingi wa wenye bima. Angalia idadi ya magari kama hapa Dar na idadi ya ajali zilivyo ndogo kwa mwaka na kiwango kila mwenye gari anacholipa hakipungui laki moja na nusu kwa nini basi kisishuke tu jinsi magari yanavyoongezeka?

Pitia vizuri post zangu ikiwemo ya mwisho kabla ya hii utaelewa.

NATAMANI KUNGEKUWA NA LUVE DEBATE.
 
Na ukumbuke population ya Rwanda na Tz ni tofauti sio unachongoa mdomo tu
We jamaa unachekesha population ni issue au GDP?
Tumewazidi population zaidi ya mara 6
Lakini vile vile tumewazidi GDP zaidi ya mara 6 sasa tofauti ni ipi?

Familia ina watu 5 inaingiza elfu 5 kwa siku
Na familia yenye watu 10 inaingiza elfu 10 kwa siku ina tofauti gani?

UVCCM bhana
 
Acha kuzunguka, kwani Lissu aliposema CHADEMA watatpoa huduma bora za afya kwa kufananisha na Ubelgiji alitegemea nini? Mimi nimeonyesha kwa data kuwa ili utoe huduma za kiwango hucho utahitani kuwa na kipato zaidi ya ubelgiji ukixingatia sisi tuko mara tano zaidi kuliko wabelgijibna uchumii wetu uko chini mara tisa kuliko wao. Huo muujiza hauwezekani.

Hata sasa bila bima kwa baadhi bado watu wakienda hospitali wanatibiwa mfano wazee wote wanatibiwa bure.

Wilaya mbalimbali zina mfumo wa bima ila bado haujamfikia kila mtu lakini hilo linaendelea kufanyika.

Ninachokataa ni hicho mnachodanganya watu kuwa chini yenu huduma zitakuwa bora.

Jinsi uwezo wa kiuchumi unavyoongezeka ndivyo huduma za afya zitakavyoendelea kuboreshwa.

Comparison, forecast au projection katika uchumi ni vitubvya kawaida.
Mkuu shida hauna elimu yoyote kuhusu Bima au uchumi ndio maana unabisha bila objectivity.
Nmeshakwambia model ni Rwanda maana ulianza kuhoju cjui kwanini Jeshi lina package yake ndio nikatoa hayo maelezo.
Rwanda imeweza ingawa tumezidi GDP mara 6.7 sasa jikite hapo wao wamewezaje kuwa na coverage ya 90%? Achana na belgium kwanza jikite kwa Rwanda

Naomba ujibu hili kwanza
 
Lissu na wenzie wanajisumbua tu Nchi hii kuongozwa na upinzania bado waendelee kujiandaa ila kwasasa hatupo tayari kuwapatia nchi.
 
Back
Top Bottom