Mkuu wewe ndio mweupe sana kwenye uchumi eti una compare GDP ya Belgium na Tz ili useme haiwezekani? Sasa nikupe challenge.
Model ya bima ya afya wametohoa Rwanda ina hiyo special package ya Jeshi alafu kuna wafanyakazi wa umma, then kuna wale wenye kipato cha chini kabisa wasio kwenye sekta rasmi n.k
2. Justification yake ni kwamba michango inategemea income bracket uliyopo. Rwanda wameigawa mara 4 kwahiyo utachangia kulingana na uwezo wako wa kiuchumi lakini wale waliopo chini kabisa yaani wanaoishi kwenye umaskini wa kutupwa basi serikali inawachangia totally wakishirikiana na mfumo wa crowdfunding wa kijamii tunaweza uita "Ujirani mwema"
3. Mchango wa serikali ya Rwanda ni almosy 14% pekee kwahiyo haiathiri mapato ya Serikali kabisa kwenye kuendesha mfuko.
4. Usichofahamu ni kwamba mfuko ukiwa na pesa zinazungushwa kwenye biashara mbalimbali na masoko ya hisa hivyo pesa inazaa ili mfuko uwe unakua zaidi na kupunguza risk ya float.
5. Unasema GDP ya Belgum blah blah, sasa naomba ufaham Tz imeizidi GDP ya Rwanda karibu mara 6.7 kwa data za 2018. Sasa kama Rwanda kufikia 2011 walikua na coverage ya 90% bima ya afya sisi tunashindwa nini??
Tusiishi kwa kukariri tujifunze Rwanda tupunguze ujuaji.