Uchaguzi 2020 Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 - 2025

Ilani hii inaainisha maeneo yatakayopewa kipaumbele na serikali ya Chadema, vipaumbele hivyo ni pamoja na:

a. Kugatua madaraka ya uongozi na utawala kwa lengo la kuusogeza karibu na wananchi.

b. Kubadili mfumo wa uongozi na utawala ili kuongeza na kuzingatia misingi ya uadilifu, ufanisi, uzalendo na uwajibikaji

c. Kwa kushirikiana na sekta binafsi Kujenga uchumi imara wa kidigitali na shirikishi

d. Kuongeza mishahara na kuwapandisha madaraja watumishi wa umma

e. Kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje

f. Kurejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

g. Kurejesha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni

h. Kutoa elimu bora na bure kwa ngazi zote

i. Kuanzisha utaratibu wa afya bure kwa akinamama wajawazito, watu wenye ulemavu, watoto na wazee

j. Kuwajengea uwezo wanawake kusimamia na kumiliki uchumi

k. Kwa kushirikiana na sekta binafsi kuongeza wigo wa ajira na kipato chenye tija kwa vijana

l. Kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi, salama na ya uhakika kwa wote.

m. Kuwezesha Wananchi kumiliki ardhi kwa matumizi endelevu

n. Kushirikiana na sekta binafsi kuboresha miundombinu ya barabara, masoko, nishati na viwanda vya kusindika mazao vijijini.

o. Kutumia rasilimali ya maji iliyopo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na mifugo.

p. Kushirikiana na sekta binafsi Kuboresha miundombinu ya barabara, reli, usafiri wa anga na majini.

q. Kushirikiana na sekta binafsi kuboresha sekta ya utalii na maliasili.

r. Kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha uwepo wa Nishati nafuu na ya uhakika.

s. Kuboresha sekta ya madini na kuwezesha wachimbaji wadogo wanashiriki na kumiliki uchumi wa madini.

t. Kushirikisha sekta binafsi katika kuimarisha sekta ya sanaa, utamaduni na michezo na kuifanya iwe ya kibiashara.

Ilani hii imebeba maono na mwelekeo wa kisera wa Serikali ya Chadema kwa lengo la kuwashawishi wapiga kura kuchangua wagombea wa Chadema kwa vile Chadema kinaamini katika “UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU”
 
Hivi hayo maendeleo ya watu yatapatikanaje kama miundo mbinu ni mibovu!!? Mwenyezi mungu mwenyewe aliumb vitu kisha ndo kumuumba mwanadamu.Chadema msitufanye mafala.
 
HICHO CHAMA HAKINA ILANI, HAYO UMEYATOA WAPI KAMANDA?!?
 
Kila mtu ana uhuru wa kutoa na kuchukua habari lakini pia simu na bando ni mali ya mtu binafsi kwahiyo mnaobeza Ilani ya Chadema mnatimiza haki yenu kikatiba lakini haiiondoi atia mioyoni, najua dhamila zinawasuta ila kizazi chenu kitawahukumu.
 
Back
Top Bottom