Uchaguzi 2020 Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 - 2025

Ngoja tuipitie vizuri.
Ni kweli ngoja tuipitie vizuri baada ya kuidai kwa siku kadhaa. Ila kwa muhtasari uliotolewa, Sera zinatoa mwanga kuhusu Tanzania ya kesho.

Angalizo: Kama hii Ilani ilikuwa imeandaliwa mapema, iweje wagombea wote, akiwemo wa Urais na Mgombea mwenza, wasinadi Sera badala yake wanajikita kudharilisha wagombea wa vyama vingine, hasa CCM. Yawezekana ni "copy & paste" Ilani za vyama vingine?
 
Ilani bora kuliko zote Tz
Naisoma Ilani ya CHADEMA msitari kwa msitari, kifungu kwa kifungu, ukurasa kwa ukarasa, kwa umakini sana. Nitakuwa naweka mreshonyuma wa maoni yangu nikianzia na kifungu cha siku 100 za Serikali ya CHADEMA.

Imendikwa kwenye Ilani kwamba, Ndani ya siku 100 tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya taratibu za kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

Hakika nia ni nzuri kabisa kutoka kwa viongozi ambao wamejipambanua ni wagomvi, wenye hasira, watu wa visasi na wazandiki. Najiuliza ni mwujiza gani utafanyika kumbadili Shetani kuwa Malaika?

Baadhi ya tabia hizo zilizojionesha waziwazi na zinaendelea, ni pamoja na:-
1) Kama Chama Kikuu cha Upinzani, kiliwaengua wabunge wasio wa chama katika Baraza la Mawaziri Kivuli Bungeni.
2) Wabunge waliokaidi amri ya M/kiti kujifungia ndani, wakati wa korona, bunge la bajeti likiendelea, walifukuzwa kwenye chama.
3) Wabunge na Madiwani waliokihama, wakidaiwa kununuliwa, hadi sasa wanaitwa wasaliti, japo walitumia uhuru na haki yao (msingi mkuu wa hiyo Ilani).
4) Wagombea wote, wakiwemo wa Urais, kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea, wanatumia lugha isiyokuwa na dalili zozote za maridhiano.

Mkuu Mwanahabari Huru kama kweli ni Ilani bora kuliko zote Tz, najiuliza, kwa hulka ya viongozi wa CHADEMA, Je, nia yao ni ya dhati kweli?
 
Kumbe bakabaka waliondolewa yale maduka yao ya duty free! Hapa Tundu Lisu akikomaa na hili anaweza kupata kura za jwtz,Polisi uhamiaji, Magereza na Zimamoto.
 
Nitapigia Kura Chadema Kuipigania Tanzania Yangu....Tukutane Machinjioni
 
Huu hapa ni Muhtasari wa Ilani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)
...

Baada ya CHADEMA kupigiwa kelele kutokuwa na Ilani, hatimaye wame "copy & paste" muundo wa Ilani ya CCM. Nitarejea kuendeleza uchambuzi wa Ilani ya CHADEMA vs CCM kuhusu maendeleo ya watu, Sera inayonadiwa kwa nguvu zote na Viongozi wa CHADEMA wakishindwa kueleze maana yake ni nini kiuhalisia kwa maisha ya kila siku ya MTU.
 
Kuhusu Uchumi:
CHADEMA: KUJENGA NA KUMILIKI UCHUMI IMARA NA SHIRIKISHI. Uchumi ni nyanja kuu katika maendeleo ya binadamu. Kwa kutambua hilo Chadema kimejipanga kuutafsiri ukuaji wa uchumi kwa vitendo ili kuwepo kwa mabadiliko chanya katika maisha ya kila Mtanzania. Hili litawezekana kwa kufumua mfumo wa sasa wa uchumi wa kijamaa ambao umeshindwa kuboresha hali ya maisha ya Watanzania, na kuanzisha mfumo wa soko jamii ambao unalenga kufungua fursa kwa kila mtu kutumia vipaji vyake katika kuzalisha na kumiliki mali. Mfumo huu mpya wa uchumi wa soko utaambatana na uanzishaji wa uchumi wa kidigitali ambao unazidi kushika kasi katika nyanja zote za uzalishaji na utoaji huduma katika dunia ya utandawazi. Moja ya njia ya kufanikisha azima hiyo, CHADEMA imepanga Kujenga, kuimarisha na kusimamia uchumi wa kitanzania kwa kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na hisa na wawekezaji wenye mitaji mikubwa.

CCM: MAPINDUZI YA UCHUMI KWA MAENDELEO YA WATU. Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu wa kujenga uchumi wa kitaifa ili kuhakikisha kwamba Watanzania ndio wanufaika wakuu wa uchumi na maliasili za nchi na ndiyo wenye kauli juu ya namna uchumI unavyoendeshwa. Kwa muktadha huo CCM itaelekeza Serikali kuendelea na juhudi za kuifanya Tanzania kuwa nchi inayojitegemea kiuchumi pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na nchi nyingine. Juhudi maalum zitaelekezwa kuhakikisha rasilimali za asili za nchi hii, hasa ardhi, madini, gesi asilia, mafuta, maji na misitu zinanufaisha wananchi na Taifa kikamilifu.

Ili kufanikisha hilo, CCM itaelekeza
Serikali kuendelea kujenga mazingira ya kiuchumi na kibiashara ambayo yatavutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje na ambayo yatakuwa tulivu na
yanayotabirika.


Ukisoma kwa umakini, vyama vyote vimedhamiria kukuza uchumi, lakini tofauti ni jinsi ya kufanikisha hilo. Uchumi kwa CHADEMA utatategemea wawekezaji wenye mitaji mikubwa, ambao kimsingi wanatoka nje. CCM kwa upande wake, wataendeleza juhudi za kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji wa ndani na nje. Kwa maana hiyo Uchumi kwa CHADEMA utakuwa tegemezi tofauti na uchumi wa kujitegemea kwa upande wa CCM.

HITIMISHO: CCM imeonyesha kuwa inawezekana kujenga uchumi imara kwa kujitegemea. Mifano ikiwa ni miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za jamii, ambayo imefanikishwa ndani ya miaka 5. Kwa upande wa CHADEMA ni kitendawili kwani pamoja na kupata mabilioni ya fedha za ruzuku na kuchangiwa na wabunge, chama hakina fedha za kuendesha kampeni, ukiachia mbali kutokuwa na ofisi kuu ya chama.
 
Ikawaje mkuu. Interested
 
Nyie offis zenu si mmejengea kodi zetu... haha afu unalipwa ivi sh ngapi ivi ulewe alafu utume upupu uku?? Uwekezaji wenyewe kipengele bado utakesha kwenye maoffisi ukionga upate hati miliki bora wa nje maana uwa tunajua kodi itakua pia kubwa kwao and pesa zitaingia mtaani vijana tuzitendee haki
 
Na hizi hoja, du, au?
 
nimeisoma ilani ya chadema yenye kurasa 104 kwa nusu saa nikaimaliza, ya ccm yenye kurasa 364 bado naisoma
Wameandika porojo na uongo mwingi wakidhani ndio inakuwa nzuri
 
Analysis nzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…