Uchaguzi 2020 Ilani za Uchaguzi za Vyama Vikuu vya Siasa

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,692
Wanabodi salam!

Ninaomba kwenye huu uzi tujadili kuhusu ilani za vyama vya upinzani hasa vile ambavyo tayari vimeshatoa ilani zao.
CDM wao tayari wameshatoa ilani yao na sera yao kubwa ni
UHURU HAKI NA MAENDELEO.

ACT Wazalendo wao pia walizindua ilani yao jana yenye sera kubwa.ya "KAZI NA BATA"

CCM nao walizindua ilani yao ikiwa na sera kubwa "TUMETEKELEZA KUWA KISHINDO TUNASONGA MBELE PAMOJA"
Vyam vingine bado sijapata nakala za ilani zao. Tunawasubiria.

Kwa hawa waliotoa ilani kwanza nimebaini yafuatayo

1. ACT walijiandaa ukamilifu sana kuingia kwenye huu uchaguzi. Ilani yao sio tuu imeonyesha gap liko wapi lakini pia imeonesha na njia ya utatuzi wa hilo tatizo. Ilani hii ukiisoma kwa mtu asiye na kuzuzuka kwa chama basi hii ilani is the best. Na imeonesha pasi kificho ni maeneo yepi ambayo tunaweza kupata fedha za kutekeleza yaliyo ahidiwa.

2. Ilani ya CHADEMA nayo haikupishana sana na Ile ya ACT ingawa kwa CHADEMA imeongea wazi wazi kuwa "watatafuta maridhiano ya kitaifa" ndani ya siku 100 za kwanza kwamba kuwe na makubaliano ya kutokulipana kisasi. Hi ni katik a juhudi za kuleta tena umoja wa kitaifa. Ilani hii haikuishia hapo bali iliendelea kupoint mambo kadhaa ambayo yatatekelezwa ndani ya siku 100 za kwanza.

3. Ilani ya CCM imesheheni mambo lukuki ila yenyewe imekuwa kimya sana kuhusu watumishi wa serikali pamoja na maendeleo ya mtu binafsi. Imejikita zaidi kwenye maendeleo ya vitu hasa miundo mbinu.

Kwa haraka haraka nimeona kwa mara ya kwanza upinzani Tanzania umekuja na ilani ambazo zimegusa maisha ya mtanzania halisi na ikiwa kweli watasimamia basi watanzania watakuwa watu wenye furaha sana.

Swali langu kwa wapinzan ni moja tuu

He wanejipangaje kuhakikisha ilani hizi zinasomwa na kueleweka na kila mtanzania?

Pia watafanyaje kuhakikisha rais aliyeko madarakani anaondoka kwa amani ikiwa atashindwa kwenye uchaguzi?

Swali la tatu je watahakikishaje haki inatendeka kwenye uchaguzi ikiwa bado tume sio huru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…