Ile adhabu shuleni ya kuvalishwa kibao cha Swahili Speaker ilikuwa jau sana

Ile adhabu shuleni ya kuvalishwa kibao cha Swahili Speaker ilikuwa jau sana

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Leo bhana, katika pitapita zangu za hapa na pale, nikaangukia shule fulani, Basi bana, nikakutana na mwanafunzi kapendeza zake, lakini shingoni kavaa bango kubwa limeandikwa “Swahili Speaker”.

Aisee! Hapo hapo akili ikafanya flashback kali moja kwa moja nikarudi enzi za 2003 hadi 2009 nilipokuwa sekondari.


Jamani tulikuwa na mambo! 😂
Hilo bango lilikuwa kama hukumu ukinaswa tu umeongea Kiswahili, basi unavalishwa hilo bango mchana kutwa. Na mbaya zaidi, wanafunzi walikuwa wanawindana balaa! Kila mmoja anatega mwenzake, kama vile ni mchezo wa paka na panya

Unasikia mtu anakuita kwa makusudi:
“Eeeh, njoo kidogo…”
Ukijibu tu kwa Kiswahili — umeshamalizwa! 😂

Nimejikuta natabasamu mwenyewe pale, nikikumbuka zile mbinu za kijanja, mitego, na furaha ya kumkamata mwenzako. Lakini pia ile aibu ya kubeba bango siku nzima… dah!

Cha kuchekesha zaidi, hilo bango lilikuwa na jina la utani maarufu sana tuliloliita… ila ndiyo hivyo tena, kumbukumbu imenichezea—jina limenigomea kabisa! 😅

Wewe mdau, kwenu liliitwaje hilo bango? Au bado linaishi hadi leo?

1778058164513.png
1778058220647.png
 
Back
Top Bottom