Ile Ivory Coast ya kina Drogba, Kolo Toure, Didier Zokora na wakali wengine ilituhujumu waafrika.

Ile Ivory Coast ya kina Drogba, Kolo Toure, Didier Zokora na wakali wengine ilituhujumu waafrika.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu nimetafakari kwa makini na kujiuliza maswali mengi sana ila binafsi nimeona ni hujuma tu hakuna sababu nyingine. Haiwezekani timu iliyokuwa na wakali wote waliokuwa wanavuma kwenye timu zao za Ulaya ishindwe kufanya la maana kwenye world cup au mashindano mengine makubwa.

Hii Ivory Coast ya kina Didier Drogba, Didier Zokora, Cheikh Tiote, Yaya Toure, Kolo Toure, Solomon Kalou, Gervinho, Emmanuel Eboue, Aruna Dindane, na wakali wengine ilibidi ichunguzwe na kutuondelea mashaka kwamba hawakuwa wakifanya hujuma.
 
Taifa la Africa ambalo liko serious na lina uzalendo wa hali ya juu ambalo miaka si mingi linaweza kuchukua kombe la dunia ni Senegal tu, huu ni mtizamo wangu.

Ukiangalia wachezaji mpaka kocha wao wale jamaa wanauzalendo wa hali ya juu, hata wakipoteza mechi unaona kabisa wanajuta sio kama Nigeria, Ivory Coast na Cameroon. Ghana kuna kipindi walikuwa na uzalendo ila siku hizi ni wababaishaji tu.
 
Nakumbuka ila fainali ya Afcon kati ya Egypt na Ivory coast Drogba anakosa goli hapa na hapa. Pale nikaanza kuhisi wa Misri ni wachawi aseeh.
 
Nakumbuka ila fainali ya Afcon kati ya Egypt na Ivory coast Drogba anakosa goli hapa na hapa. Pale nikaanza kuhisi wa Misri ni wachawi aseeh.
Duu warabu walipiga Dua...japo miaka mingi imepita....nilijiuliza Kwa mazingira Yale drogba alipaisha vipi ule Mpira....Dunia hii ya maajabu...
 
Duu warabu walipiga Dua...japo miaka mingi imepita....nilijiuliza Kwa mazingira Yale drogba alipaisha vipi ule Mpira....Dunia hii ya maajabu...
Miuu Umenikumbusha mbali nilikua darasa la 5 ile fainali misri Walikua home refa anapga filimbi kuanzisha Mpira Kuna jamaa jukwaani nae alianza kusoma kisomo Mpka ile penat ya Mwsho wanapga jamaa ndo alikua anamaliza kusoma hata mm nilihis Egypt Wachawi
 
Back
Top Bottom