Ile roho ya Nyerere kutojilimbikizia Mali na kutotapanya Aliitoa wapi? Mbona baada ya yeye tunapata Marais majanga tu?

Ile roho ya Nyerere kutojilimbikizia Mali na kutotapanya Aliitoa wapi? Mbona baada ya yeye tunapata Marais majanga tu?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Roho ya kujitosheleza,kutotaka Makuu na kutojilimbikiza Mali. Hii roho nyerere aliitoa wapi? Zama zile nadhani Nyerere angekuwa amejilimbikizia Mali nyingi na Familia yake au Ukoo ungekuwa moja ya Koo Tajiri sana Tanzania au Africa.

Lakini tunaona watoto wake wanapambana wao kama wao walisoma shule za kawaida. Hawakuwa na ukwasi uliopitiliza miaka ile toka kwa baba zao.

Nyerere mpaka anastaahafu alisahau kujijengea Mansion au Penthouse kama hawa viongozi wetu wa sasa.

Akajengengewa nyumba kwa hisani na wanajeshi. Ambayo alikuja bado lalamika. Why nyumba kubwa vile na wala hana mwili wa kutisha? Nyerere huyu ambaye Shivji anasema hata kwenye birthday yake hakuwa anaichukulia kuwa ni big deal. Alikuwa anakata keki tena kwa mzaha tu kama baba yangu huko kijijini leo umwambia hbr za kukata cake na mishumaa.

Leo anakuja mtu anatumia pesa za walalahoi hawa kutoa zawadi ya birthday halafu walalahoi wengine wanashangilia?

Hii ni dalili ya kuanza halalisha wizi mkubwa siku zijazo. Tumeona viongozi walio kuwa wanajenga kwao na kuhamishia kila kitu kama vile wataishi milele. Nyerere Butiama kumebaki kama sehemu nyingine tu haikupewa upendeleo maalum.

Kwa miaka ile Nyerere angeweza kusema hata mkoa wa Mara uwe Jiji la Kanda ya Ziwa. He didint do that.

Leo hii wanakuja viongozi wanafanya uhuni kwa kutumia kodi za watanzania hawa maskini. Wazee wetu hawalipwi mafao yao,wafanyakazi wnakamuliwa. Hatuoneshi seriousness ya kubana matumizi.

Inaumiza walalahoi maana wanaofadika na uchumi wa Tanzania nia Magabasambusa na Magabachori peke yao. Ila wanachangiwa na maskini wao waishi maisha mazuri.
 
Tafuteni mali na nyie kwa nafasi zenu
Acheni kulialia na kulalamika
Viongozi na familia wa nchi hii
Watazidi kupeta tu,huo ndiyo mfumo
Uliyopo na waliyojiwekea

Ova
 
Hapana
Kwa hapo umekosea Chief.
Kwanini,? Mkapa alistafu bila kujenga nyumba ya Mwinyi, Kikwete naye hakujenga ya mkapa , Sasa ndugu yetu kadhihilisha wazi kabisa na kuanza kutekeleza sheria za kumuongezea aliyenacho, hafu uku mtaani wenyeviti wanapitisha bakuli la kuomba mchango wa madawati, zahanati, ujenzi wa vyoo
 
Hii yote sababu magufuri alikuwa anawaenzi watu baki au ni nini? huyu mama kumbe bado haja move on.
 
Itakuwa Bi Mkubwa kapewa ratiba taiti na masponsa wake ili akamilishe fasta fasta. Sijui wameshinikiza au wanataka kumchomoa!??? Maana si kwa sarakasi za mwendo huu wa kufurahishana juu kwa juu. Hatari na nusu. Wananchi wa chini wanapewa maneno, wale wa juu wanapewa maeneo. Wakubwa wanapewa vipande vya fedha, wadogo wanaambulia makande ya fedheha. Tanzania mpya inatoweka!!! JPM alikuwa akiona mbali kweli.
 
Kuna watu wanamuona mwl Nyerere kama nabii. Hivi pamoja na kwamba mwl Nyerere alihoji ukubwa wa nyumba lakini je aliikubali ama aliikataa?

Aliitoa waqfu kwa mayatima ama ilibaki kuwa mali yake? Ndio, nyumba ilijengwa na jeshi lakini ukifuatilia kwa undani jeshi lilikuwa mkandarasi tu gharama zimelipwa na Serikali kwa kuwa ni takwa la kisheria. Nyerere hakuyafanya haya kwa sababu nyuma yake hakukuwepo Rais mstaafu.

Kama tunakubali kwamba serikali ina fuja pesa za walipa kodi, itabidi pia tukubali kwamba jeshi lilifuja pesa ya wananchi kwa kumjengea nyumba mwl Nyerere kama hisani kama kweli ilikuwa hivyo, kwa sababu jeshi ni mali ya wananchi (JWTZ) kama ilivyo serikali.

Tusiwalaumu viongozi kwa kutekeleza matakwa ya kisheria, bali tuwalaumu kwa kuwepo sheria hizo.
 
Itakuwa Bi Mkubwa kapewa ratiba taiti na masponsa wake ili akamilishe fasta fasta. Sijui wameshinikiza au wanataka kumchomoa!??? Maana si kwa sarakasi za mwendo huu wa kufurahishana juu kwa juu. Hatari na nusu. Wananchi wa chini wanapewa maneno, wale wa juu wanapewa maeneo. Wakubwa wanapewa vipande vya fedha, wadogo wanaambulia makande ya fedheha. Tanzania mpya inatoweka!!! JPM alikuwa akiona mbali kweli.
Hivi unajua mzee Mwinyi na hayati Mkapa walisha kabidhiwa mahekalu yao na mwendazake? Na hili hekalu la mzee Kikwete lilianza kujengwa na mwendazake 2018 na kukamilika mwaka huu tena mwendazake akiwa hai likisubiri makabidhiano ndipo m/mungu alipo mkamilishia muda wake hapa duniani.
Sasa TZ mpya inatowekaje kwa bi mkubwa kusimamia na kukamilisha aliyo yaacha mwendazake?
 
Itakuwa Bi Mkubwa kapewa ratiba taiti na masponsa wake ili akamilishe fasta fasta. Sijui wameshinikiza au wanataka kumchomoa!??? Maana si kwa sarakasi za mwendo huu wa kufurahishana juu kwa juu. Hatari na nusu. Wananchi wa chini wanapewa maneno, wale wa juu wanapewa maeneo. Wakubwa wanapewa vipande vya fedha, wadogo wanaambulia makande ya fedheha. Tanzania mpya inatoweka!!! JPM alikuwa akiona mbali kweli.
Kaa kwa kutuulia mama anawakomesha mataga
 
Kuna watu wanamuona mwl Nyerere kama nabii. Hivi pamoja na kwamba mwl Nyerere alihoji ukubwa wa nyumba lakini je aliikubali ama aliikataa? Aliitoa waqfu kwa mayatima ama ilibaki kuwa mali yake? Ndio, nyumba ilijengwa na jeshi lakini ukifuatilia kwa undani jeshi lilikuwa mkandarasi tu gharama zimelipwa na serikali kwa kuwa ni takwa la kisheria. Nyerere hakuyafanya haya kwa sababu nyuma yake hakukuwepo Rais mstaafu. Kama tunakubali kwamba serikali ina fuja pesa za walipa kodi, itabidi pia tukubali kwamba jeshi lilifuja pesa ya wananchi kwa kumjengea nyumba mwl Nyerere kama hisani kama kweli ilikuwa hivyo, kwa sababu jeshi ni mali ya wananchi (JWTZ) kama ilivyo serikali.
Tusiwalaumu viongozi kwa kutekeleza matakwa ya kisheria, bali tuwalaumu kwa kuwepo sheria hizo.
Hiyo nyumba ya Butiama, Nyerere alikaa siku 14 tu kabla kifo chake. Hata sasa hakuna mtu anaishi.

Tatizo la hawa wazee, sheria zinapokuwa upande wao, wanazitekeleza mpaka nukta. Leo watumishi wana miaka karibu sita hawaijui Annual Increament kwenye mishahara yao, wakati ni hitaji la kisheria kabisa.
 
Back
Top Bottom