Ile shule waliojirekodi kumbe mdogo wangu kamaliza hapo, nimempigia kumuhoji kanipa ushuhuda huu

Sijui , ila ni majina tu hata Zanzibar wana shule inaitwa Fidel Castro
Nyuma ya hayo majina ya shule kuna historia,Castro alitembelea Zanzibar bila shaka na hiyo shule yenyewe mwaka 1977.

    • Shule ya Sekondari ya Fidel Castro (Pemba): Kwa heshima ya mchango wake na uhusiano wa karibu kati ya Cuba na Zanzibar, shule kongwe na maarufu ya vipawa iliyopo Chake Chake, Pemba ilipewa jina la Shule ya Sekondari ya Fidel Castro. [1]
 
Shule yetu wenyewe wanajeshi waliingilia kati.kama sio wale sijui ingekuwaje
Mwanzoni tulikuwa na mwalimu yule anapiga ila friendly.akipita story,mausia mabinti jitunzeni usichana wenu,na vijana namna ya kupambania ndoto zao.uhalisia wa Maisha mbeleni.
Kamaliza muda wake akaondoka sijui,ghafla tulitewa chuma kinatembeza kichapo hicho.akaona haitoshi akaleta msaidizi wake anapigaa🙆
Wanaoshinda kwenye mapagale kupiga story,wavuta bangi,micharuko,watoro nk
Walinyooka.
Imagine huku ndani Kuna vyuma viwili vinatupelekea moto halafu ukimaliza hapo wanaangalia uzito wa kosa lako wanaamua upelekwe kambi ya jeshi adhabu iendelee au la.
Na kule kambini walikuwa wanapewa adhabu gani sijui,muhusika akirudi ni mkimya adabu tele.
 
Mkuu

Kwanza siku hizi hamna uhuni 2015 kurudi nyuma kama ulimaliza Dar ungeona vitimbi.

Shule kama wailes, tandika, mibulani, chalambe na jitegemee ilikua na jamaa ni Pasua kichwa.

Rudi sasa chang’ombe,kibasila,azania na tambaza hawa walikua wanaiga.

Unajua mataa ya pale serengeti au mchicha yaliwekwa kisa wanafunzi kugongwa na gari sasa pale wanafunzi wamewahi kukiwasha mpaka polisi chang’ombe wakaja.

Tambua uhuni ulikuepo Bali utandawazi ndio unaofichua maovu ya sasa.
 
enzi zetu kulikua na VITA kabisa shule na shule, nakumbuka Azania na Tambza huu ugmvi niliukuta mwishoni, Azania na Jitegemee , huu ugomvi nilikuwepo, mnatoka shule moja kwenda shule nyingine kufanya fujo
 
enzi zetu kulikua na VITA kabisa shule na shule, nakumbuka Azania na Tambza huu ugmvi niliukuta mwishoni, Azania na Jitegemee , huu ugomvi nilikuwepo, mnatoka shule moja kwenda shule nyingine kufanya fujo
Azania na Tambaza ilikuwa balaa mpaka Serikali ikaamua Tambaza iwe Advanced school. Pale Azania ndo ikawa O level mpaka A . A level waliokuwa wanakuja Azania walikuwa wanatoka mikoa mbalimbali ili wasiwe na ujasiri wa kufanya vurugu.

Ugomvi wa Azania na Jitegemee 😂😂🤣 nilishihudia mengi sana, Sasa hivi hakuna jipya ni mitandao tu inarahisha kuona matukio.
 
Mimi napenda wanafunzi kuponda walimu kama hivi
 

Attachments

  • Savefb.App - 958006135606184(360p).mp4
    1.6 MB

Sasahivi wapo wanajiandaa na practical , hapo wakiwa katika sehemu ya maandalizi kabambe ya kuhakikisha wanatusua kwenye prac ya biology
 
nimefundisha dar kwa miaka 9

nakiri kusema Wazazi wanachangia pa kibwa kuharibu watoto
kuanzia shule ya msingi nyumbani watoto wana utawala binafsi
mtoto anajifunza kula ugoro shule ya msingi sababu anarudi home...wazazi hawapo

weww angalia tu mida ya jioni watoto wanaorudi home wanavyozagaa zagaa mpaka usiku mnene
mzazi hajui hasa ni muda gani mtoto anatakiwa awe amerudi nyumbani
kwanza kuna tatizo la usafiri....
lakini fanya utafiti mdogo ...watoto mpaka huwa wanachagua magari yanayopiga mziki
yaani unakuta wamekaa mbali kabisa hawapandi
lakini wakati mwingine pia ni utata wa makonda...
sasa mtoto hajulikani muda rasmi wa kirudi home
haya pia kuna bday party ambazo watoto wanazioganize jumamosi
sidhani kama wazazi wanajua hili....kule wanafundishana uhuni uliokithiri
mtoto ana aga anaenda tution...hasa hawa wa secondary
je mzazi ulishawah piga sim shule kuuliza kama ni kweli ???
cha mwisho...
malezi ya watoto wa dar ni magumu mnooo
watu wasisingizie kazi
hata sisi wazazi wetu walikua wanashinda mashambani
ni ile hali ya kutokujali imezidi hali ya maisha
mzazi anaenda shuhulini anamuacha mtoto wa darasa la nne kwa majirani
kuna vitoto vya msingi vinazurura hovyo
yaani malezi ya wazazi wa dar ni mabobu kuwahi kutokea duniani
cha mwisho :::mkisikia mtoto wenu kachapwa shule mnawajia juu walimu
mtoto anadakwa anauzia wenzake ugoro mnataka afanyweje???
wizara imesema fimbo inazozitambua ni tatu tu
haya......mnajionea
walimu hawachapi watoto kabisa sasa hivi

soln....wazazi waangalie namna wanalea watoto hapa dar...na wawe responsible kuwafatilia mashuleni
....cha pili Utemi wa zamani urudishwe mashuleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…