Ile shule waliojirekodi kumbe mdogo wangu kamaliza hapo, nimempigia kumuhoji kanipa ushuhuda huu

Ile shule waliojirekodi kumbe mdogo wangu kamaliza hapo, nimempigia kumuhoji kanipa ushuhuda huu

Moja kwa moja..

Niimeona video inayoTrend ya Wanafunzi wa Kike wakifanya vitendo vya hovyo, kutukana na kusema "ficheni mabwana zenu " walivyokuwa wajinga zaidi walionyesha nembo yao ya shule na namba zao za mitihani hapo ndipo watu wakatafuta jina la shule jibu likaja ni "Aboud Kumbe Sekondari School" iliyopo Dar es salaam

Nilivyoona jina ninakumbuka nina mdogo wangu ambaye sasa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) mwaka wa pili alimaliza hapo kidato cha Sita mwaka jana , nikaamua kumpigia simu nimuhoji kuhusu tukio na hali ya shule yao kwa kipindi alichosoma . Kwanza kumbukumbu zangu zinaniambia mdogo wangu tokea kipindi anasoma pale advance aliwahi kuniambia kuwa ile shule Ina vitendo vingi vya kihuni hadi huko mabwenini kwao.

Nilivyompigia kumuuliza umeona tukio linaloTrend sio shule yako ni kweli ? akajibu ndio ni shule yake tena anashukuru lile tukio kujulikana na angefurahi zaidi ile shule ingechunguzwa na kuwekewa mkazo zaidi kwani matukio ya kihuni yapo mengi sana watu kuchomana Visu , kupigana vyupa , kupewa suspension hovyo ni suala la kawaida sana na akakazia upande wa mabinti ndio kabisa micharuko kupindukia yale yalioonekana ni madogo.

Shule yenyewe Ina O_level na A_level . O_level ndio wanaongoza kwenye matukio ya hovyo na ya kihuni imefikia hatua mpaka hapo shuleni Wanafunzi wakubwa wa A_level wanawaogopa madogo wa O_level kutokana na uhuni wao uliokithiri

Akaendelea kwa kusema ile shule haina mifumo ya kidini kama shule nyingine utakuta kuna maAmir na Amirat kwa ajili ya kusimamia malezi ya Kiislamu upande kikiristo utakuta CASFETA nk lakini kwao hata vipindi vya dini hakuna ni vurugu mechi . Na nidhamu pamoja na maadili kwa ujumla ni zero hali ni mbaya .


Experience yangu binafsi katika shule za Serikali Dar haswa za Kata .

Mimi Adriz nimemaliza form 4 shule ya kata haikuwa rahisi hata kidogo kutoboa mazingira magumu ya ufundishwaji , miundombinu nk na swala la mmomonyoka wa maadili na uhuni limeenea Kwa kiasi kikubwa mpaka niliwahi kujisemea kuwa Mwanangu wa Kike bora asisome kuliko kusoma shule za Kata , nashangaa hapa Jf LIKUD anavyowapanga na kuwajaza , Mimi niliyesoma hizo shule mpaka kufika chuo Kikuu nawasihi hizi shule ni hatari sana na ni risk kubwa mwanao kusoma hapo haswa mabinti.

Shule niliyosoma Wanafunzi walikuwa Wanakambi yao ndani ya eneo la shule wanacheza , kamari , wanavuta bangi , kukuta wanaume na Wanawake tena sometimes unakuta wamekuja na viredio wakiimba na kucheza Visingeli live katika eneo la shule bila uwoga wowote . Walimu hawaogopwi na hakuna kufuata Sheria hali ilizidi kuwa mbaya mpaka mkuu wa shule akaita wanajeshi wawili kunyoosha shule kuanzia hapo shule ikawa inaongozwa kijeshi .

Wale wanajeshi Mwenyezi Mungu awalipe kheri popote walipo maana walikuja kuikomboa shule yetu katika kufa kifo cha jumla mpaka ikaja kuwa na nidhamu ya hali ya juu , kosa lolote baya unapelekwa kwa Wajeshi kuadhibiwa na walikuwa wakizunguka mitaani na shuleni kukamata Wanafunzi wahuni sugu na ilikuwa wakikamatwa inapigwa kengele ya dharura Wanafunzi wote tunakusanyika assemble kuona wakiadhibiwa kikatili . Hali ya nidhamu ikareje mpaka nikamaliza salama ila kizazi nilicho kiacha nilisikitika sana maana kilikuwa kimepinda zaidi na Wanajeshi muda wao ulikuwa umeisha wanatakiwa waondoke .

Tukio la kujirekodi wakati nipo Advance

Nilipambana nisisome shule za hovyo tena , Alhamdulillah advance nikachaguliwa shule nzuri yenye nidhamu kubwa , jina kubwa mpaka viongozi wakubwa washawahi kusoma hapo kipindi cha nyuma .

Tukio la kushangaza likitokea walipomaliza form 6 wetu , Kuna wadada waliokuwa wanaishia katika hostel zinazomilikiwa na MaSister baada ya mtihani wao wa mwisho walipofika hostel walivua Mashati ya shule na kubaki na nguo za ndani juu(Sidiria , singlend nk ) wakawa wanapiga ngoma kukatika na kucheza hovyo kama machangudoa , ile video iliTrend sana mitandaoni bahati nzuri ilikuwa ngumu kujua shule kwani ilikuwa sketi tu ndizo zinazonekana .

Kesho yake shuleni ikapigwa kengele ya dharura sisi tuliobakia tukaitwa na kupewa onyo Kali tusifanye kama wenzetu na ikatangazwa na Mwalimu mkuu kuwa wale Wanafunzi ndio basi a anaenda Necta kuomba matokeo yao yafutwe . Siku chache baadae Wanafunzi wote waliohusika kwenye ile video wakaja na Wazazi wao wakaomba msamaha mbele ya Wanafunzi wote na walipewa adhabu na shule kuwa wanaripoti na kusafisha mazingira.

Niliona huruma Wazazi waliokuja wote walikuwa wa Kike kuna wengine walilia wakati wanatuomba msamaha Wanafunzi walimu na shule kwa ujumla mpaka nikapatwa na huzuni kubwa😥😟

Hitimisho

Shule za Kata haswa za Dar , Kuna uhuni sana haya mnayaona sasa mitandaoni ni madogo kuna mengi yapo nyuma ya pazia . Sasa imekuwa fashion Wanafunzi kutengeneza content za hovyo shuleni mwaka huu ndio imezidi clips zipo nyingi sana mpaka unajiuliza wapi tunaelekea

Wito kwa wazazi msijisahau katika malezi ya watoto wenu na kuhakikisha wana marafiki na sehemu salama ya kusoma.

Wito kwa Serikali ziangilie kwa jicho pana shule hizi za Kata , Elimu zitolewa na wanaoafanya hayo mambo ya hovyo wachukuliwe hatua kali
View attachment 3698174

#UziTayari
Kabla sijaongeza chochote nikupongeze, umeandika mkuu!🤔.
Maana bila shaka uliacha kazi ukafanya kazi.

Narud kiweka nyongeza yangu.
 
Na wewe ch0k0 una elimu gani mfano kunishinda mimi kobazi tuanzie hapo
Yaani una comment matusi mwanzo mwisho. Sasa hii ndiyo akili ya kobazi ilipoishia. Kobazi mwenye akili kidogo ni Assad tu
 
Ukiona mtu anasema shule ni shule tu ujue hazijui shule za kata za Dar, kama uliwahi kusoma huwezi kamwe kutaka mwanao asome hapo.
 
Mwenye haya ma ID yote ni huyu adriz?

Alafu eti analeta uzi wa vile vitoto vidoooogo eti vihuni 🤣🤣🤣
Walimu wasiku hizi mashoga tu kipindi chetu unagongwa hadi unaanza kuiogopa shule kuliko kituo cha polisi
Kwani unafikiri hawawezi? Wameaacha mtu ana kichapa kitoto fimbo tatu tu media zote zinajaa kuchukua habari sasa hivi wameamua kufundisha tu
 
Ukiona hostel zinamilikiwa na masista usidanganye watu huwa na nidhamu coz hufatiliwa sana usichafue kanisa acha kabisa unafiki huo
Ni kweli hiyo , au mpaka nikuletee full details ?

Kama mpaka viongozi wakubwa wa dini wapo wahuni inakosa vipi hostel ?
 
Back
Top Bottom