mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
Juzi kati hapa kulikuwa na mjadala niliokutana nao humu mtandaoni kuhusiana na Air Tanzania kufanya safari za moja kwa moja ulaya hadi hapa Tz. Kiukweli mjadala ule ulinivutia kwa kiasi chake ,lakini binafsinikagundua ili shirika hili liweze kupenya soko la ulaya itahitaji mipango,ubunifu na mikakati ya muda mrefu.
Kwanza tujiulize;
Pili Ethiopian Airlines naye hayuko nyuma.kwa mfano ndege ya ethiopia inafanya safari zake kuanzia bole👉kilimanjaro👉zanzibar kisha tena zanzibar👉kilimanjaro👉bole. Watakaofika bole huabiri ndege tena ya Ethiopian Airlines inayoenda barani ulaya hususani route ya Bole👉Heathrow uingereza. Hapo sijagusia Qatar airways na flydubai na jirani hapo kenya airways.
Hebu tumbizane ,nafasi ya Air Tanzania iko wapi hapq ya kupenya soko la ulaya?. Usiseme hapa kwamba Air Tanzania inapata faida ya route ya Dar👉Mumbai. Tunaangalia soko la utalii .mhindi na utalii wapi na wapi? Mchina na utalii wapi na wapi? Hizi safari za china na India sanasana ni ajili ya kubeba mizigo (cargo).
Air Tanzania badilikeni . Tafuteni mtu mzoefu wa hii sekta mumkabidhi shirika ili ku capitalize route za ulaya kama Waarabu walivyompa sir Tim clark shirika la fly Emirates awasaidie kuliendesha. Ukifika hapo dubai unapata ndege ya kukupeleka popote kwenye kona ya hii dunia. Iwe ni mexico au Brazil utapata . Iwe ni Huko Australia hadi new Zealand, kote huko ndege zipo. Ni kwa sababu ya mipango,udhubutu na utayari.
Anyway siwapangii ni ushauri tu.
Kwanza tujiulize;
- Shirika la ndege la Air Tanzania lina wataalamu wabobezi kwenye eneo la marketing kwa ajili ya kuitangaza Tanzania kiutalii na kuwashawishi wageni waweze kuja?
- Je shirika la ndege lina ndege za kutosha(fleet size) kukidhi mahitaji na idadi ya wasafiri wa hiyo route ya ulaya hadi afrika?
- Ukiritimba uliopo kwenye shirika hili kwa mujibu wa ripoti za CAG za kila mwaka utawezesha shirika hili ku survive kwenye ulimwengu wa ushindani wa kibiashara wa safari za ndege duniani?
- Shirika la ndege la Air Tanzania limejifunza kwa wenzao wa Ethiopian Airlines namna ya walivyoweza ku survive kwenye hii biashara yenye risk nyingi kwa miaka yote hiyo tokea 1940s lilipoanzishwa?