Ili kazi zako ziende, omba Yesu kila asubuhi usije sema una gundu

Ili kazi zako ziende, omba Yesu kila asubuhi usije sema una gundu

Nawa kumbusha kwa jina la Yesu Kristo kila asubuhi uamkapo omba hata dk 1, 2 au tatu ili bwana abariki kazi za mikono yako.

Hata kama hujaokoka omba maana hata mvua yesu huwanyeshea wema na waovu.

(lakini anza kwa kushukuru kwanza kwa kuamshwa salama maana ni vema kuingia katika malango ya bwana kwa shukurani kwanza).

Hata kama hujaokoka wewe omba tu bwana yesu yupo kwa ajili yako

^ NI MIMI MKUMBUSHAJI WAKO

View attachment 3056532
Hakuna injili ya hivyo wewe mpumbavu labda unazungumzia injili feki za Shetani mwenye nafsi 3 ...Yesu akuja duniani hili.kutumikia tamaa za miili ....watu wamegeuza kuwa mungu ni kwa ajili ya matamanio yao ya kimwili ..mnajidanganya.
 
Endelea kuota bila kua usingizini,

Alifanywa kua mwili na nani?

Kwahiyo baada ya Yesu kuja,watu wamebadilika mabaya yao?
Mungu ambaye alisema na manabii waliopita aliamua kutufikishia neno lake katika mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo
baada ya kuja yesu watu tumebadilika?
Yesu Kristo Amekuja kurudishia mamlaka kamili ya dunia hii ambayo iliyochukuliwa na shetani wakati pale bustani ya eden Adam na Hawa walivyoenda kinyume na Mungu
 
Kati ya Mungu na huyo Mama wa Mungu ni nani alitangulia kuwepo?

Au Mungu alimuumba Mama yake kwanza ili aje amzae yeye Mungu mwenyewe?
Ukianza kuuliza maswali ya Hivi nitakushangaa sana.

Kama una amini Kuna ufalme wa Mungu au yesu kurudi mara2 acha na Mimi niamini hiki ninacho kiamini.

Maana sisi tumeletewa tu hizi Imani na kuzipokea kama zilivyo.

Ndio maana wapo wanaamini kitu moto ni dhambi kuila.wengine pombe, nk

Hivyo ukianza kujiuliza maswali juu ya Imani yngu Nami nikikuuliza maswali kadhaa hutokuwa na majibu Bali Imani uliyoiamini ww
 
Mungu ambaye alisema na manabii waliopita aliamua kutufikishia neno lake katika mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo

Yesu Kristo Amekuja kurudishia mamlaka kamili ya dunia hii ambayo ilichukuliwa na shetani wakati pale bustani ya eden Adam na Hawa walivyoenda kinyume na Mungu
Kwahiyo hawa wachungaji hua wanamkemea Shetani gani wakati mamlaka yake yalisha chukuliwa na Yesu?

Hapa unaongelea mamlaka gani hayo?
 
Ukianza kuuliza maswali ya Hivi nitakushangaa sana.

Kama una amini Kuna ufalme wa Mungu au yesu kurudi mara2 acha na Mimi niamini hiki ninacho kiamini.

Maana sisi tumeletewa tu hizi Imani na kuzipokea kama zilivyo.

Ndio maana wapo wanaamini kitu moto ni dhambi kuila.wengine pombe, nk

Hivyo ukianza kujiuliza maswali juu ya Imani yngu Nami nikikuuliza maswali kadhaa hutokuwa na majibu Bali Imani uliyoiamini ww
Kwahiyo huna majibu ya swali langu sio?
 
Sawa pamoja na kwamba wewe umekaa ki-spiritist zaidi kuliko ki-biblia.
Yes mkuu I'm not religious person but I'm spiritual person and I know GOD exist but also I believe in universe and its law like Gratitude , law of attraction and so on.

Swala la Gratitude ni KEY kubwa katika kuifungua siku na kuifunga siku.
 
Mungu ambaye alisema na manabii waliopita aliamua kutufikishia neno lake katika mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo

Yesu Kristo Amekuja kurudishia mamlaka kamili ya dunia hii ambayo iliyochukuliwa na shetani wakati pale bustani ya eden Adam na Hawa walivyoenda kinyume na Mungun
Mungu na siasa wapi na wapi? hata hivyo precess ya kumtuma yesu kama mtoto kuzaliwa, kukua, kufa na kufufuka ni ndefu sana. mbona kwa uwezo wa mungu kurudisha mamlaka lilikuwa ni suala la sekunde tu.
 
Unataka nikijibu kibinadamu au kiimani?

Kwa Imani tunaamini yesu ni Mungu hivyo aliye mzaa yesu (mamake) ndo mama wa mungu
Ndio maana nikakuuliza kati ya huyo Mama wa Mungu na Mungu mwenyewe,ni nani alianza kuwepo? Au Mungu ndiye alimuumba Mama yake kwanza ili aje amzae yeye?

Nauliza ili nijifunze tu.
 
Mungu na siasa wapi na wapi? hata hivyo precess ya kumtuma yesu kama mtoto kuzaliwa, kukua, kufa na kufufuka ni ndefu sana. mbona kwa uwezo wa mungu kurudisha mamlaka lilikuwa ni suala la sekunde tu.
Soma sana neno la Mungu sisi jifunze siwezi bishana na mtu ambaye hajui anachokipinga ni nini
 
Ukishaona una haja ya kumuomba Mungu (mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote), ujue Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo, kusingekuwa na haja ya kumuomba.

Angekupa unachohitaji kabla hujaomba.
 
Ukishaona una haja ya kumuomba Mungu (mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote), ujue Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo, kusingekuwa na haja ya kumuomba.

Angekupa unachohitaji kabla hujaomba.
Mna hoja nyepesi sana wapinga Kristo
 
Tunaomba kwasababu inatupasa kufanya hivyo ili Kuwa karibu na Mungu wetu,hatuombi Ili mambo yetu yaende!

Kuna watu hawaombi/Sali lakini bado mambo Yao yanaenda vizuri mno kushinda hata tunao omba/Sali!
Wapo wanaoomba lakini hawafanyi kazi wakitegemea miujiza wapo wanaokesha makanisani lakini matendo sio mema

Wanafanikiwa bila kufanya ibada wanatumia nguvu za giza ubongo wa mwanadamu upo limit ukitaki kufanya mambo makubwa unlimited lazima ufanye ibada kumuabudu Mungu huyu wa Israel
 
Mna hoja nyepesi sana wapinga Kristo
Sema hoja nyepesi baada ya kuipangua, sasa unasemaje hoja nyepesi wakati hujaipangua?

Ni hivii, ukishaona unahitaji kumuomba Mungu tu, ujue Mungu mjuzibwa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Kwa sababu, angekuwepo, angekupa unachohitaji kabla hata hujaona haja ya kumuomba.
 
Wapo wanaoomba lakini hawafanyi kazi wakitegemea miujiza wapo wanaokesha makanisani lakini matendo sio mema

Wanafanikiwa bila kufanya ibada wanatumia nguvu za giza ubongo wa mwanadamu upo limit ukitaki kufanya mambo makubwa unlimited lazima ufanye ibada kumuabudu Mungu huyu wa Israel
Kiukweli sijaelewa ulicho andika,hebu andika tena uenda nitakuelewa
 
Back
Top Bottom