PreGE2025 Ili kudhibiti uhalifu, uanzishwe mfumo wa National Recognition System wenye kutunza DNA na fingerprint za watu wote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
Kwako Rais wa JMT,
Waziri wa mambo ya ndani,

Baada ya kutafakari kwa kina kama mtanzania ni kitu gani kifanyike ili kudhibiti uhalifu katika maeneo mbalimbali, Nashauri serikali iunde chombo mahususi chini ya wizara ya mambo ya ndani kitakachokuwa kinatumia mfumo wa NATIONAL RECOGNITION SYSTEM (NRS) ambao utakuwa mfumo maalumu wa utambuzi wa DNA na fingerprint kwa watu wote waliopo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wawe wazawa au wageni.

Kwa maoni yangu, mfumo huu utarahisha KAZI ya utambuzi wa mhalifu na kama utaundwa mfumo wa utambuzi wa haraka zaidi kwa kutumia, DNA, FINGERPRINT, SAUTI, USO NA MUONEKANO utarahisha zaidi.

Naomba kuwasilisha

Ahsante.
 
Hapa US wana kitu kinaitwa NATIONAL CRIME DATABASE ambayo ipo under national crime information center

Law inforcement zote zinachukua taarifa toka kwa hawa jamaa
 
Hiyo mifumo inaweza kuwekwa. Ila ukiwatambua utajukua hatua gani, mtu anakingiwa kifua na serikali. Rais.
 
Mbona tz kitengo hicho kipo hapo mambo ndani
Kuna nchi fulani mfano Canada ukitaka kwenda unaambiwa ukachukuliwe finger prints
To trace criminal antecedents,
Na majibu huwa yanarudi negative au positive
Na unapewa police clearance certificate yako

Ova
 
Haitasaidia kitu. Maana watawala hawajawahi kutaka kudhibiti uhalifu
Kama wamewahi basi wamefail kabisa maana wahalifu ni kama wanaakili kuliko vyombo vya ulinzi vya serikali
 
CCM WATAUPINGA KWA NGUVU ZAO ZOTE
 
Ndio imetoka hiyo mzee, kabla ya kuajiriwa kokote huwa wanakusanya record yako, ukionekana hapo ni kipengele. Labda uwe na kesi ndog nodogo, ila major cases ni doa kubwa mno.
Tz bado sana,tunapenda kuwakombatia wahalifu
Unakuta mtu ana likesi ehh kesho huyo huyo anachaguliwa tena kuwa mtu fulani
In short tumetengeneza taifa la majambazi wezi...system yote iko corrupt
Ila tunachokipanda soon tutakivuna tu

Ova
 
Hata ukifanya hivyo hakuna kitakachobadilika mpaka Regime itakapobadilishwa na Wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…