Ili kuisaidia nchi na kumsaidia Rais Samia, je tumfanyie an honest MTR based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo to determine tunapokwenda?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo la kuchanganya Lugha
JF ilipoanzishwa, it was meant to be an online user generated social forum, mtu una post chochote, kwa lugha yoyote ya public, bila kuvunja kanuni za jf.

Kwa kadri jf inavyozidi kukua, inazidi kuimarika na kuzidi kuboreka, hivyo sasa iko kwenye transformation from just a social media to mainstream media, ukipost heading kwa kuchanganya lugha, heading yako inabadilishwa kuwekwa lugha ya Kiswahili, sometimes mabadiliko hayo yana changes the meaning iliyokusudiwa.

Bandiko hili ni la swali, Ili kuisaidia nchi, na kumsaidia Rais Samia, Je tumfanyie an honest MTR, based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo ili to determine tunapokwenda?.

Heading hii imechanga lugha kwasababu maneno mengine ya Kiingereza hayana Kiswahili.

MTR ni Mid Term Review, na SMART Objectives ni malengo ya kimkakati ambayo ni Specific, Measurable, Achievable, Realistic, and Timely na hizo Objectives ziko za short term, medium term na long term.

Hivyo ili kuisaidia nchi, na kumsaidia Rais Samia, ni muhimu kumfanyia an honest MTR ya performance appraisal yake ya toka alipoanza, hapa alipofika, hivyo ku determined kule anakokwenda au anako tupeleka.

Hii MTR, hufanywa na watu wanaofanya kazi na wenzetu wazungu ambapo wanapima utendaji kazi wako.

Kwa kawaida hii MTR hufanywa na boss wako anaye ku supervises. Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Rais wa JMT ndie the top boss na anafikia maamuzi ya mwisho yeye kama yeye, anaweza kushauriwa na washauri wake na wasaidizi wake, lakini kwenye kufikia maamuzi, anafikia maamuzi yeye kama yeye na hawajibiki kufuata ushauri wa yeyote!.

Sehemu pekee ambapo Rais wa JMT atawajibika ni kwenye katiba ya JMT, hiyo katiba ambayo Rais wa JMT anawajibika, ni mali ya wananchi Watanzania, hivyo the real boss ni Mwananchi, ndiye mwenye nchi, mwenye katiba, ndiye aliye muajiri Rais wa JMT kwa kura yake, ndiye anayemlipa mshahara kwa kodi yake, hivyo Mwananchi wa Tanzania ndiye boss wa Rais Samia, na Rais Samia ni mtumishi tuu wa watu, aliyepewa dhamana kututumikia kwa kutuongoza, hivyo ni haki kabisa kwa Mwananchi wa kawaida kabisa kama mimi kumfanyia Rais Samia MTR.

The SMART Objectives zetu hapa za kumfanyia Rais Samia MTR ni ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, time frame yake ni miaka 5, hivyo MTR ya ilani ya uchaguzi ya CCM ilipaswa iwe July 2023, lakini kwa vile Samia ameipokea nchi na urais March 2021, then MTR yake ndio sasa.

MTR ni ya kazi gani?, unamfanyia Rais wa JMT MTR ili iweje?.
MTR ni muhimu sana ili kupima ulipotoka, ulipo hivyo ku determine kule unakokwenda the target ikiwa ni 2025.

Ili kumtendea haki Rais Samia, kwenye hii MTR yangu, kwenye Strategic Objectives sitaitumia ilani ya uchaguzi ya CCM, kwasababu hii ni ilani ya mtangulizi wake, hivyo kuitumia sio kumtendea haki, badala yake mimi nitatumia mabandiko yangu yenye expectations zangu za kisiasa tuu juu yake kumhusu Rais Samia kama Rais wa JMT, toka alipoingia mpaka hapa alipofika ili kum determine na kukuwekea projection ya 2025.

Moja ya eneo nitakalo jikita ni eneo la katiba, sheria, haki, siasa na demokrasia ili ku determine kama 2025 tutafanya uchaguzi huru na wa haki kweli au tutaendelea kufanya uchaguzi 'huru' na wa 'haki' kama kawa!.

Strategic Objectives zangu ni mabandiko yangu kumhusu Rais Samia, hivyo MTR zangu za Samia ni hizi
  1. Hili ndio bandiko langu la kwanza la urais wa Rais Samia, hivyo hii ndio MTR yangu ya kwanza kwa Rais Samia Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri
  2. TZ Trends & Analysis: Hoja 30 za The Economist Kumhusu President Samia. Kuna za Kweli, za Uongo na Uzushi na Kutaka Kumpangia Watakacho Mabeberu, Jee?
  3. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  4. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
Ili kuziona hizo MTR, ni lazima ufungue bandiko husika, halafu nikimaliza MTR zote ndipo nitakuja na conclusion ya projection za Uchanguzi Mkuu wa 2025.

Hii ni hatua ya kwanza ya ushirikishwaji, jee tumsaidie Rais Samia, tumfanyie an honest MTR, based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo ili to determine tunapokwenda?, au tusimtathimini rais wetu, tuendelee tuu kwenda hivi hivi, halafu tathimini ifanyike kwenye kampeni za 2025?.

Paskali
Update from mchangiaji very objective.
Mkuu mbenge , asante sana, tangu bandiko hili limepanda, wewe ndie mchangiaji wa kwanza kuchangia kuhusu MTR.
P
 
Ukiacha angalizo lako lisilo na maana yoyote ( Maana jf unaweza hata kuandika kifaransa na tukachangia tu ) , Ni hivi , viongozi wa Tanzania huwa wanaamini wana akili kuliko raia yoyote , na huwa wanaamini wanajua kuliko yeyote yule , viongozi wengi wa Tanzania wanaamini kwamba wanaowafuatia kwa akili ni watoto wao tu , mifano ni mingi .

Sasa hata tukishauri mpaka damu itutoke kichwani unadhani watatusikiliza ?

 
Sasa hiyo picha ni viongozi au watoto wa viongozi?

Nchi isiyo ya Kifalme kama Tanzania Katiba Ndio Kiongozi
 
Andiko zuri lakini hakuna Rais hapa. Sijui alitoka wapi masikini huyu. Naamini atapita na Tanzania itabaki.
 
Sasa Samia anashaurika?Labda tujiunge naye kuandaa script za movie za Utalii!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Itasaidia nini wakati hata hao wanaomshauri hasikii

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Maadam unafanya peke yako ni rahisi kulazimisha majibu unayoyataka wewe kwa sababu zako binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…