Wanabodi,
Angalizo la Kuchanganya Lugha
Naomba kuanza na angalizo la kuchanganya lugha, JF ilipoanzishwa, it was meant to an online user generated social forum, mtu una post chochote, kwa lugha yoyote ya public, bila kuvunja kanuni za jf.
Kwa kadri jf inavyozidi kukua, inazidi kuimarika na kuzidi kuboreka, hivyo sasa iko kwenye transformation from just a social media to mainstream media, ukipost heading kwa kuchanganya lugha, heading yako inabadiloshwa kuwekwa lugha ya Kiswahili, sometimes it changes the meaning.
Bandiko hili Ili kuisaidia nchi, na kumsaidia Rais Samia, Je tumfanyie an honest MTR, based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo ili to determine tunapokwenda?.
Heading hii imechanga lugha kwasababu maneno mengine ya Kiingereza hayana Kiswahili.
MTR ni Mid Term Review, na SMART Objectives ni malengo ya kimkakati ambayo ni Specific, Measurable, Achievable, Realistic, and Timely na hizo Objectives ziko za short term, medium term na long term.
Hivyo ili kuisaidia nchi, na kumsaidia Rais Samia, ni muhimu kumfanyia MTR ya performance appraisal yake ya toka alipoanza, hapa alipofika, hivyo ku determined kule anakokwenda au anako tupeleka.
Hii MTR, hufanywa na watu wanaofanya kazi na wenzetu wazungu ambapo wanapima utendaji kazi wako.
Kwa kawaida hii MTR hufanywa na boss wako anaye ku supervises. Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Rais wa JMT ndie the top boss na anafikia maamuzi ya mwisho yeye kama yeye, anaweza kushauriwa na washauri wake na wasaidizi wake, lakini kwenye kufikia maamuzi, anafikia maamuzi yeye kama yeye na hawajibiki kufuata ushauri wa yeyote.
Sehemu pekee ambapo Rais wa JMT atawajibika ni kwenye katiba ya JMT, hiyo katiba ambayo Rais wa JMT anawajibika, ni mali ya wananchi Watanzania, hivyo the real boss ni Mwananchi, ndiye mwenye katiba, ndiye aliye muajiri Rais wa JMT kwa kura yake, ndiye anayemlipa mshahara kwa kodi yake, hivyo Mwananchi wa Tanzania ndiye boss wa Rais Samia, na Rais Samia ni mtumishi tuu wa watu, aliyepewa dhamana kututumikia kwa kutuongoza, hivyo ni haki kabisa kwa Mwananchi wa kawaida kabisa kama mimi kumfanyia Rais Samia MTR.
The SMART Objectives ni ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, time frame yake ni miaka 5, hivyo MTR ya ilani ya uchaguzi ya CCM ilipaswa iwe July 2023, lakini kwa vile Samia ameipokea nchi na urais March 2021, then MTR yake ndio sasa.
MTR ni ya kazi gani?, unamfanyia Rais wa JMT MTR ili iweje?.
MTR ni muhimu sana ili kupima ulipotoka, ulipo hivyo ku determine kule unakokwenda the target ikiwa ni 2025.
Ili kumtendea haki Rais Samia, kwenye hii MTR yangu, kwenye Strategic Objectives sitaitumia ilani ya uchaguzi ya CCM, kwasababu hii ni ilani ya mtangulizi wake, hivyo kuitumia sio kumtendea haki, badala yake mimi nitatumia mabandiko yangu yenye expectations zangu za kisiasa tuu, kumhusu Rais Samia, toka alipoingia mpaka hapa alipofika ili kum determine na kukuwekea projection ya 2025 kama tutafanya uchaguzi huru na wa haki kweli au tutaendelea kufanya uchaguzi 'huru' na wa 'haki' kama kawa!.
Strategic Objectives zangu ni hizi ambazo nita pick randomly na kufanya MTR.
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
Ili kuziona hizo MTR, ni lazima ufungue bandiko husika, halafu nikimaliza MTR zote ndipo nitakuja na conclusion ya projection za Uchanguzi Mkuu wa 2025.
Hii ni hatua ya kwanza ya ushirikishwaji, jee tumsaidie Rais Samia, tumfanyie an honest MTR, based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo ili to determine tunapokwenda?, au tusimtathimini rais wetu, tuendelee tuu kwenda hivi hivi, halafu tathimini ifanyike kwenye kampeni za 2025?.
Paskali
Update from mchangiaji very objective.
Mkuu
mbenge , asante sana, tangu bandiko hili limepanda, wewe ndie mchangiaji wa kwanza kuchangia kuhusu MTR.
P