SoC02 Ili kujua idadi sahihi ya wakazi na makazi ya watu; Mfumo wa uhesabuji sensa ya watu na makazi watumike mabalozi na viongozi wa mtaa?

SoC02 Ili kujua idadi sahihi ya wakazi na makazi ya watu; Mfumo wa uhesabuji sensa ya watu na makazi watumike mabalozi na viongozi wa mtaa?

Stories of Change - 2022 Competition

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
Tanzania nchi yangu, naipenda nchi yangu TANZANIA.

Kwa sasa nchi yetu inaenda kufanya zoezi la muhimu mno la kujua idadi ya watu,maeneo wanayoishi na hali zao kwa ujumla.

Kwa umuhimu huu napenda kuwaomba watu wote waliohumu jf kuwa mawakala wa kuhakikisha kila mmoja anahesabiwa.

Natoa pongezi kwa rais wetu kwa kuonyesha namna zoezi hili lilivyo na muhimu,na navipongeza vyombo vya habari na media mbalimbali ikiwemo jamiiforums kwa kuwakumbusha watanzania mda wote juu ya tarehe ya kuhesabiwa.


Pamoja na jitihada zinazotumika kwenye zoezi hili kwa miaka yote ila napendekeza kuboresha namna ya kulifanya zoezi hili ili kuleta usahihi zaidi.

Napendekeza serikali yetu iwatumie mabarozi na wenyeviti (wa vitongoji,mitaa na vijiji) kwa sababu mbalimbali zikiwemo;

UADILIFU NA USAHIHI WA ZOEZI LA UHESABUJI SENSA.
Viongozi wa mitaa na vijiji ndio watu waliojirani zaidi na wakadhi wa maeneo husika,hivyo ikiwa watatumiwa viongozi hawa basi kutakuwa na uhakika wa kila mtu kuhesabiwa.

KUONDOA DHANA YA UHESABUJI SENSA NI AJIRA KWA MAWAKALA ZAIDI KULIKO KUJITOLEA.
Sio siri kwa sasa sensa inajadiliwa zaidi katika engo ya masilahi na kuliko hata uadilifu na ufanyaji wa zoezi lenyewe kwa usahihi. Kwa miaka ya nyuma rushwa ilipenya ili kupata nafasi hii ya kuwa wakala wa uhesabuji watu.

KUONGEZA THAMANI KWA NAFASI ZA VIONGOZI WA MITAA NA VIJIJI.
Kutokana na sababu ya kutopata mshahara kwa viongozi hawa,kunapelekea vijana wengi na watu kutotamani kuwa viongozi wa mtaa na vijiji. Hivyo basi ikiwa nafazi za kuhesabu watu yaani sensa itapelekwa kwa viongozi hawa itasaidia kuwapata wasomi wengi kwenye nafasi hizi za serikali za mitaa na vijiji.

KULIFANYA ZOEZI KUWA SHIRIKISHI ZAIDI KWA WANANCHI.
Kuondoa ile hali ya mtu anaishi eneo B kwa miaka nenda rudi na akamshawishi tu mtendaji apate saini yake na akapata kazi kwenye eneo A basi viongozi wa serikali za mitaa watumike ili kuondoa ujanja ujanja huu.

IWE CHACHU NA MOTIVATION ILI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA KWA KUGOMBEA UONGOZI KWENYE SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI.

Kilio cha ajira kipo midomoni mwa vijana wasomi wa kitanzania kwa kuwa fursa za kazi zipo finyu ukilinganisha na idadi ya wahitimu mavyuoni.

Ikiwa nafasi za serikali za mitaa na vijiji ikagombewa kama inavyogombewa ubunge na udiwani basi kwa kiasi fulani ingesaidia kupunguza kilio hichi hata kwa uchache. Utakuta wazee tu ndio viongozi wa mitaa wakijitolea zaidi kuwa viongozi kwakuwa huko chini hakuna binasi yoyote.

KUTAFANYA ZOEZI LIENDESHWE KWA MUDA MFUPI ZAIDI NA KUACHA TABIA YA KUPIKA TAARIFA ILI KUENDANA NA MUDA ULIO.

Kutumia watumishi wa serikali ambao hawana udhoefu wa kutosha na mitaa ya maeneo husika inafanya zoezi kuchukua muda mrefu zaidi au kulipua ili kuendana na muda.

Kwa kuhitimisha tu ni kuwa sensa ya watu ni lazima ifanyike na watu wenyeji wa eneo ili kuleta dhana ya ushiriki kwenye jamii.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom