Uchaguzi 2020 Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni huru na wa haki

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Declaration of Interest
Naomba kuanza na ku declare interest kuwa mimi ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM ambaye ni muumini wa haki na demokrasia ya kweli ndani ya Bunge. Nautoa ushauri huu kwa dhati ya moyo wangu, licha ya ukada wangu kwa chama changu, CCM.

Asiyekubali Kushindwa Sio Mshindani. Tumechoka na Kelele za Kutotendewa Haki Kila Mnaposhindwa!
Kufuatia kilio cha wapinzani kutotendewa haki chaguzi zote za nyuma kila wanaposhindwa, na uchaguzi huu kwenye urais, kuna wengi tayari tunajua upinzani unakwenda kushindwa, hivyo kuliko kusubiria vilio vya kelele za kutokutendewa haki, sasa tunapojiandaa kwa Uchanguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani hapo October 28, nautoa ushauri huu sababu tayari hisia za kutotendewa haki zimeanza kujitokeza miongoni mwa wapinzani kuwa uchaguzi Mkuu ujao hautakuwa huru na wa haki, hivyo kufuatia wasiwasi huo kwa wapinzani, licha ya mimi kuwa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, ninatoa ushauri very honestly kwa wapinzani, kuwa ni kweli uchaguzi mkuu huu utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki kama alivyoahidi rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, tumwaminie na tusiwe na shaka yoyote kabisa licha ya yeye pia kuwa mmoja wa wagombea.

Ushauri huu nauweka kwa points format na kuwaomba wana jf, tuirudishe ile jf ya zamani ya kujadili hoja iliyo mezani kwa kupangua hoja kwa hoja na sio kujibu hoja kwa viroja ikiwemo mtindo mpya wa wana jf wa kisasa kumjadili mtoa hoja badala ya kuijadili hoja iliyo mezani. Karibuni sana.
  1. Ushauri huu wa bure nimeuekekeza kwa vyama viwili tuu vya Chadema na ACT, kwasababu kwa maoni yangu hivi ndio vyama viwili pekee ambayo vimeonyesha at least some seriousness ya kiasi fulani kwa upinzani, kwa vyama vingine vyote vya upinzani, ikitokea vikashinda hata kiti kimoja cha ubunge au udiwani, ushindi huo utatokana na personal merits za mgombea individually na sio kutokana na strength ya chama chake. Tukiongelea upinzani Tanzania ya leo, tunaongelea Chadema na ACT Wazalendo.
  2. Ukiondoa CCM, hakuna chama kingine chochote cha siasa nchini Tanzania ambacho kina the ability, capacity na capabilities za kusimamisha wagombea majimbo yote na kata zote, hivyo pazia la NEC litakapofungwa, kuna wagombea wa CCM wa ubunge na udiwani watapita bila kupingwa hivyo kwenye majimbo yao, wagombea watatangazwa moja kwa moja na hawatapigiwa kura, ila kura za urais zitapigwa. Hii itakuwa ni dalili ya kwanza ya uthibitisho wa udhaifu wa upinzani wa Tanzania na nyota njema ya dalili ya ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi Mkuu huru na wa haki
  3. Kwa vile zoezi la upigaji kura kwa kura zote zinapigwa vituoni very transparently na zinahesabiwa hapo hapo vituoni very transparently mbele ya mawakala, na matokeo hadi ya urais yanabandikwa kwenye ubao wa matangazo very transparently ili kila mmoja aone,
  4. Hakuna namna yoyote ya kufanya rigging ya matokeo ya kura zilizopigwa vituoni kwa uhuru na uwazi na matokeo yakabandikwa ubaoni.
  5. Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, kuruhusu matokeo yote hadi ya urais kuhesabiwa vituoni na kubandikwa ubaoni, hii maana yake ni NEC inaendesha zoezi la uchaguzi very transparently with no any schemes and nothing to hide.
  6. Kitendo cha matokeo kubandikwa ubaoni, hiyo maana yake is to make it public ili kila mtu ayaone na kujiridhisha.
  7. Hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote kutumia simu janja yake kupiga picha karatasi za matokeo ya kila kituo kwa lengo la kutunza kumbukumbu.
  8. Nawashauri Chadema na ACT Wazalendo, wawatume wanachama wao na wafuasi wao nchi nzima, watumie simu janja zao, kupiga picha matokeo ya kila kituo, kisha kufanya an independent tallying zao. Hakuna kosa lolote kisheria kufanya an independent tallying, kosa ni kutangaza matokeo, hivyo hii independent tallying ifanyike kwa kutunza tuu kumbukumbu na kujiridhisha ili mwisho wa siku waje ku compare notes na matokeo ya NEC.
  9. Naamini kabisa NEC itatenda haki, haitazuia independent tallying, bali kusisitiza hao wafanya independent tallying wasithubutu kutangaza matokeo ya independent tallying zao, hata kama mgombea wao ataonekana emeshinda kwa matokeo ya vituoni, halafu matokeo ya NEC yakawa otherwise wise, they'll have a strong case to argue supported by undisputed documentary evidence.
  10. Kwa vile NEC nayo inatangaza matokeo ya majimbo from returning officers direct kadri yanavyopokelewa, kama wapinzani wana ushahidi usiotia shaka kuwa matokeo ya tallying ya NEC ni tofauti na independent tallying zao, na matokeo ya ubunge na udiwani yanapingwa mahakamani, Mhimili wa Mahakama uko chini ya mtu muadilifu sana, namfahamu uadilifu wake, kwasababu alikuwa mwalimu wangu pale UDSM, Prof. Ibrahim Juma, hivyo vijana wake watatenda haki.
  11. Ushauri huu wa bure ni kufuatia ukweli wa trends za hali halisi ya kisiasa nchini Tanzania zinazoonyesha hakuna ubishi kwenye urais ni mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli anakwenda kushinda urais kwa ushindi wa kishindo kufuatia track record yake supported by the deliverable visible tangible developments ya maendeleo ya kuonekanika vs empty promises za wapinzani wake,
  12. hivyo ushindi huu kwa CCM ni ushindi msafi, very clean, clear undisputed sweet victory uliopatikana kwenye uchaguzi huru na wa haki.
  13. Na kwa vile wapinzani nao watakuwa na ushahidi wa uhalali wa matokeo baada ya kujiridhisha kupitia ushauri huu wa bandiko hili, for the sake of national unity,
  14. Nawashauri wagombea wa urais wa Chadema na ACT Wazalendo, nao wawepo ukumbini pale Dodoma siku ya kutangazwa kwa matokeo ya urais ya NEC, nao wampongeze mshindi, na mshindi awapongeze alioshindana nao.
  15. Nimewashauri wagombea wa urais wa Chadema na ACT Wazalendo tuu, kwasababu nafahamu kuwa wagombea urais wengine wote wa vyama vyote watakuwepo.
  16. Na siku ya kuapishwa kwa rais Magufuli kwa awamu ya pili, pia wawepo pale Uwanja wa Jamhuri na kuhitimisha rasmi zoezi la Uchaguzi.
  17. Kazi iliyobaki ni kujenga nchi
  18. Na kwa vile CCM itakuwa imepata ushindi wa kishindo, hivyo Bunge lijalo litakuwa ni one party CCM dominated parliament, ili to make a good sense of Bunge la vyama vingi, tutamshauri mshindi JPM, kuwateua baadhi ya alioshindana nao au wapinzani makini kati ya zile nafasi zake 10 za uteuzi ili wakalete changamoto Bungeni ya kulichangamsha Bunge kuonekana ni Bunge la vyama vingi kweli
  19. Na kufuatia Watanzania kuonyesha imani kubwa kwake na kwa CCM, then awamu ijayo, hakuna haja ya kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. JPM ana uwezo wa kuiletea maendeleo Tanzania, na bado akaiachia demokrasia ikashamiri, He'll have nothing to lose and everything to gain kwa kuleta maendeleo, huku akiiiachia demokrasia ushamiri.
  20. Tutapata Tanzania ya neema yenye kuzingatia demokrasia, haki za binaadamu na uhuru mkubwa zaidi wa habari, and if ikimpendeza pia anaweza kuirekebisha Tume ya Uchaguzi NEC, kuifanya more inclusive na funga kazi ni akiisikia sauti Mungu moyoni kwake, kuacha the biggest legacy, ni kama atawapatia Watanzania Katiba mpya, and you never know, anaweza kushangaa, mwaka 2025, nchi inzima ikafanya maandamano kushinikiza ukomo wa vipindi viwili vya urais uondolewe kwasababu katiba ni ya watu na sauti ya watu ni sauti ya Mungu, Vox Populi is Vox Dei
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Pascall kaka yangu, hebu tuache bana.

Humu JamiiForum ninaamini hakuna mtu ambaye hana akili timamu, wala hakuna wendawazimu, kila member ni mzima kiakili. Huwezi ukamdanganya mtu yoyote JF kirahisi hivi.

Naomba nikutoe kasoro kidogo hapo katika para yako ya kwanza ya "DECLARATION OF INTEREST" kwanza. Kuna sentensi moja umeisahau kuiandika mwishoni na tungekuona wewe ni mkweli toka moyoni. Sentensi yenyewe ni :- MIMI PASCALL MAYALLA NAANDIKA HII MAKALA ILI NIMKOSHE ROHO MH. RAIS ILI ANIKUMBUKE KATIKA UTEUZI WAKE WA WABUNGE WA VITI MAALUM/WAKUU WA MIKOA/WAKUU WA WILAYA AU HATA UKATIBU MKUU.

Turudi kwenye kiini cha makala yako, swala la uchaguzi wa haki nchini Tanzania ni hakuna, na haijawahi kutokea, na halitatokea mpaka yatakapo fanyika mawili, kati ya haya;
1) KATIBA YA NCHI IBADILISHWE

2) RAIA WAINGIE MTAANI NA WAKICHAFUE KWELI KWELI.
 
Heshima uliokuwa nayo haipo tena mkuu umechuja sana, kwanini usiishauri tume ya uchaguzi ihesabu kura kwa njia ya wazi kama walivyofanya CCM kwenye kura za maoni kuwe na uwazi badala ya mawakala ambao hutishiwa na kufukuzwa? kwani wagombea wa CCM hawakuweza mawakala kwenye kura za maoni? tuache kukengeuka kwa sababu za maslahi badala ya kuliteteaTaifa letu.
 
Huru na haki wakati wagombea lukuki wa upinzani wamefanyiwa figisu wasifanikiwe kurudisha fomu za ubunge na udiwani?
-wametekwa
-wamekamatwa na polisi
-wengine na TAKUKURU
-wengine fomu zao zimekataliwa
-wengine wakurugenzi wamefunga maofisi baada ya kupokea za ccm
-Wengine wameporwa fomu

Sasa tutegemee ccm kupita bila kupingwa majimbo mengi zaidi.
 
😂😂 buloo bwana!
1.Bila tume huru tusitarajie lolote
2.Bila katiba mpya hakuna jipya.
3.Zungumzia figisu zilizopo na mizengwe wanayofanyiwa upinzani wanaporudisha fomu
4.Nani asiyependa kushiba?DED anaweza kumtangaza mpinzani wakati yeye kaajiriwa na mjomba?
“Acheni kujichekesha na kucheka wenyewe”
 
Wazo lako Ni zuri lakini kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Kuna kipind Mawakala wa Vyama vya upinzani walifukuzwa kutoka kwenye vituo vya uchaguzi na wengine walikamatwa na polisi. Bila Shaka ilikuwa kwenye chaguzi za marudio. Kwa vitendo Kama hivi hata Wapinzani wakiweka Mawakala kila sehemu haiwezi kusaidia Kama tu CCM wakiamua kufanya figisu.
 
Pascall kaka yangu, hebu tuache bana.

Humu JamiiForum ninaamini hakuna mtu ambaye hana akili timamu, wala hakuna wendawazimu, kila member ni mzima kiakili. Huwezi ukamdanganya mtu yoyote JF kirahisi hivi...
Imemjibu Vema ... I couldn't explain better!!

Kama Mawakala wa Uchaguzi wangekuwa wanauwezo wa kuzuia Wizi au kuensure Uhalali wa kura basi leo CCM wangekuwa tayari wako upande wa Upinzani kama siyo kufutika kabisa katika siasa za TZ.
 
Bila tume huru upinzani hawawezi katu kushinda hii vita, zitaimbwa nyimbo zote, kina Amsterdam wataongezeka lakini hili ni taifa huru. Tupiganie taasisi imara na huru, hapo tunaweza kucheza mechi zetu kirahisi, otherwise hakuna kitu.
 
Kama tayari idadi ya wapiga ni ya kupika, unategemea matokeo yawe ni ya kweli? Toka lini idadi ya wapiga kura nusu ya watanzania wote, au watu wazima wote kujiandikisha kupiga kura. Hilo bandiko lako refu ni la kupoteza muda.
 
JPM hakukosea aliposema wew ni njaa!Hapa umejikalisha uchi kutanguliza tumbo mbele!Huna hadhi tena JF,umedharauliwa na kupuuzwa!Mabandiko yako hayana mvuto,wengi wakiona mwandishi ni Mayalla(njaa),wanajua ni mwendo ule ule wa mapambio kutafuta uteuzi baada ya kuambulia kura moja!
Its a shame!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…