Liverpool VPN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 6,958
- 16,358
INTRODUCTION
Eeh bwana ehh habari zenu
Nikiri Mimi sio shabiki kabisaa wa siasa. Yaani sina Kadi ya chama chochote na sifikirii kuwa na Kadi ya chama chochoteee kileee.
Na kifupi huwa sifatilii zile habari za siasa zaidi ya hizi ambazo zinapostiwa insta kwenye page za habari za labda msingwa, Ikulu, na Wizara.
Mimi ni mtumishi wa halmashauri, Elimu yangu ni Bachelor of Science in ..... na Masters of Science in ....., na nina miaka 10 kazini Halmashauri (experience).
SCENARIO
Juzi mama alivyoteua ma-DC Kuna jambo nikakumbuka, nimeoma niwashirikishe ili mnipe jibu.
Kipindi kile mama alivyomteua nadhani Mkuu wa Magereza nilikua Dodoma kwenye semina Morena Hotel.
Sasa tukiwa tunapiga breakfast seminani zikapita gari V8 kaliii nyeusi na ving'oro pale kwenye lami ya Morena, kwamba Mkuu wa Magereza anaenda Ikulu kuapishwa.
Mimi nikaropoka "Mimi huyo miaka 5 ijayo nitapanda hizo gari nikielekea Ikulu kuapishwa baada ya kula uteuzi wa Mama"
Sasa tukiwa pale mezani jamaa mmoja akaniuliza "Una Kadi ya Chama?" Jibu likawa hapana. Ila tulipiga story na vitu vingiii kuhusu uteuzi na CCM, ila niliondoka na hili.
PROBLEM
Ili upate uteuzi haijalisha muda wako wa Kazi (Experience/duration), Haijalishi Elimu yako, ila KINACHOTAKIWA UWE NA KADI YA CHAMA CCM.
Kwamba, hata upige Kazi vipi ofisini ila ili uonekane Basi ni lazima uwe na Kadi ya CCM. Yaani ukitaka tobo la uteuzi basi shikiria Kadi ya CCM na uitangaze kama unayo, yaani ishi ki-CCM.
QUESTION
Sasa Je, ni kweli hili jambo ni sahihi? Kwamba pamoja Nina Miaka 10 serikalini na elimu ya Masters ila bado natakiwa kuwa Kadi ili mama anione mimi mtumishi wake Bora huku Kijijini?
(Halmashauri yetu ni Chaka/vijiji hasa)
Yaani ili nilambe uD(R) C, uDED, uD(R)AS, na vyengine ni lazima nijinadi ndani ya CCM na kuwashughulika na hoja za wapinzani mpaka mama atakaponisikia na kuniona?
Kwamba nikiwa hivihivi Neutral (kama nilivyosasa sina Kadi) basi hata nipige Kazi haswa ila NISAHAU UTEUZI?
#YNWA