Ili Simba ifuzu Robo Fainali, matokeo ya timu zote yaweje?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Mechi za mwisho za makundi ya CAF Champions League zitapigwa wikiendi ijayo.

Simba Sc ya Tanzania inashika nafasi ya nne katika kundi lake lakini bado ina nafasi ya kufuzu robo fainali. Mechi za mwisho za kundi lake ni;

Simba Vs As Vita

Al Ahly Vs Js Soura

Je matokeo ya hizo mechi zote mbili inabidi yaweje ili Simba aweze kushinda na kusonga robo fainali?
 
Hesabu mbona ni rahisi tu,ili Simba afuzu,anahitaji kushinda tu mechi ya mwisho. Simba akishinda mechi As vita moja kwa moja atakuwa amefuzu.

Mechi ya waarabu itakuwa ni ya kuangalia tu nani atafuzu wa kwanza. Lkn matokeo yoyote hayataiathiri Simba iwapo itashinda. Yaani Simba ili Afuzu narudia tena lazima ashinde na akishinda anafuzu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Why asifungwe? Vita unawachukulia poa
Sio kuwachukulia poa mpira wa Africa ni fitna na timu inayokua nyumbani inafaidika Vita wale wakija kwa Mkapa watakua wakawaida Kama walivyokua Nkana,js saoura na Al Ahly,kwa Mkapa Simba hamwachi mtu salama Simba spirit yake ipo ivyo kwenye group stage wale waarabu au Nkana sio kwamba walikua wabovu ila wakija pale kwa Mkapa hawawi wale mnaowajua watatafuta dkk ya 1 Hadi ya 90'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yetu macho,umuhimu wa game kwa timu zote hauwezi kuifanya Simba iwe na home advantage,game zilizopita walikuwa wanajaribu kutafuta points tu,usijeshangaa hii game ikaisha 4-3,5-2 maana itakuwa open game,itakayekuwa makini ndiye atashinda
 
Yetu macho,umuhimu wa game kwa timu zote hauwezi kuifanya Simba iwe na home advantage,game zilizopita walikuwa wanajaribu kutafuta points tu,usijeshangaa hii game ikaisha 4-3,5-2 maana itakuwa open game,itakayekuwa makini ndiye atashinda
As Vita watakuja kushambulia lakini tunawazidi kwa Mambo mengi ndani ya uwanja Hadi nje ya uwanja mashabiki tuu ni mchezaji wa 13 kumbuka iyo Simba ni kufa au kupona na rekodi kwetu ipo vizuri na kwa As Vita ipo vibaya...as Vita ugenini hajashinda hata mechi moja Bora sisi tulimfunga mbabane... As Vita alienda kucheza mechi ya mtoano na Bantu club Lesotho ambayo sio tishio kama Simba waliishia kupata sare tuu Sasa sembuse Hapa kw Mkapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wachezaji wa aina ya Vita kelele za mashabiki ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa maana wanaexperience kubwa kuliko Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…