Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi Bora

Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi Bora

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Mwalimu Nyerere alipokuwa analeta Ujamaa kwa watanzania, aliponda sana masuala ya kuchukua fedha za nje, na moja ye hotuba yake aliwaponda sana wanaotaka mishahara mikubwa kwamba hela tunapata wapi.

Na hapa sisemi kwamba nakubaliana na falsafa ya Ujamaa, najaribu kuzungumzia masuala ya fedha ambayo Nyerere aliyaponda na kuwaambia watu maendeleo hayaji kwa fedha bali kwa vitu vinne, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Kwenye suala la watu, ktk kiingereza kuna misamiati kadhaa, people na human capital, argument yangu ni kuwa Mwalimu alimaanisha Human Capital not just people. Ndio sababu kulikuwa na mikakati ya kukuza Human Capital kwa miradi mbalimbali kama UPE.

CCM wanajinasibisha kwenye falsafa za Ujamaa na Kujitegemea, lakini je kwa sasa tunaona mkakati wa kuboresha vitu hivyo vinne ambavyo Nyerere aliona ni msingi wa maendeleo kabla ya fedha. Hivi karibuni nilifuatilia mjadala fulani humu jukwaani nikasoma hoja nzuri za Analogia Malenga na Logikos kwenye mambo yanayofanana na haya. Nilipenda staha zao kwenye kuweka hoja.

Hata wao nawauliza kama wanaona hiyo misingi minne ya maendeleo kama inafuatwa na CCM, au ndio imebaki siasa chafu na uongozi tu ambao pia unategemea pesa za nje na bado hazitumiki ipasavyo. Kwa maana ya Hoja ya Nyerere ni kuwa hata ukipata hela kiasi gani kama hauna hivyo vitu vinne utabaki mtumwa tu.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom