Ilikuwa kosa kubwa sana Joseph Kabila kumuibia Tshisekedi ushindi wa urais Congo dhidi ya mshindi halali, Fayulu

Kura zinaibiwa na maccm leo ndiyo ukalie kupigia kelele kura za Congo?
 
Kwa hiyo Kagame akifa amani amna tena ndo maana Rwanda tunasema ina safari ndefu sana
 
Katumbi hata hakugombea 2018, mgombea wa Kabila alikuwa anaitwa Emmanuel Ramazani Shadary ambaye alipata kura kidogo sana ndio ikabidi Kabila ale dili na Tshisekedi.
Haya bhana, niliyachanganya madesa
 
Mbona sasa anaua wapinzani wake kama anakubalika hivo.
 
Kati ya Fayulu na Tshekedi, Kagame hamtaki Tshekedi, bora Fayulu.
Kwani Kagame ni nani mpaka awe na mtu anayemtaka katika uchaguzi wa wakongoman.

Huyu kagame yatamshinda tu, siku zake zinahesabika. Asilimia 90 ya nchi za afrika hazimpendi na anasemekana ndio chanzo cha mgogoro nchini Kongo.
 
Nasikia utaongozana na Netanyahu mpk USA..lkn nashangaa upo Goma sahv 🤣
 
Aliyeobiwa kura na kusimikwa Tschekedi ni Katumbi Gavana wa Lubumbashi na mmiliki wa TP Mazembe na sio Fayulu.

Fayulu alikuwa mgombea wa chama cha Kabila, ila alishika nafasi ya 3 ikabidi hesabu zifanyike kwa Tschekedi na Katumbi ndio ikawa hivyo
Tume ya uchaguzi ilokuwa chini ya Nangaa ilimtangaza Tshisekedi kuwa ndiye mshindi kwa asilimia 38.56 na Martin Fayulu akishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 34 na wa tatu alikuwa Emmanuel Ramazani Shadary ambae alipata asilimia 23.

Fayulu alipinga matokeo hayo akisema Tshisekedi alikula njama na Kabila kuchakachua kura na akaenda kwenye mahakama ya Katiba ambako mapingamizi yake yalitupiliwa mbali.

Kanisa katoliki nalo lilitoa kauli kuonyesha mashaka yake juu ya uchaguzi huo.

Uchaguzi wenyewe ulipangwa ufanyike 2016 lakini Kabila akaanza kupiga danadana na ni shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa ndilo lilomfanya Kabila apange uchaguzi ufanyike mwaka 2017 na ukazogezwa tena hadi 2018 na hapo pia machine za kupigia zipatazo 8000 ziliungua moto ulotokea kwenye bohari za tume ya uchaguzi. Machine hizo ilikuwa ni mara ya kwanza zingetumika kweye uchaguzi nchini Congo DRC.

Makubaliano yalikuwa chama cha Kabila kimuunge mkono Chadary awe mgombea wao lakini Katumbi na Jean-Pierre Bemba wakapinga wakimtaka Martin Fayulu ndie awe mgombea.

Lakini hapohapo kuna mtu akaja na majina mfukoni na majina hayo yakawa Tshisekedi na Vital Kamerhe ambae angekuwa Waziri mkuu wa Tshisekedi.

Hivyo kulifanyika kitu chaitwa "double knock effect" kwanza majina yametoka mfukoni na pili, uchaguzi ukachakachuliwa.
 
Huo ni uongo mtupu, kwani aliyeko madarakani amekataa kuwauzia hayo madini? Labda uniambie alikiuka mikataba yao ndio maana ikawa hivyo, mnakiuka miiko ya uongozi, uchaguzi baadae mnadingizia hewa.
 
Ilikuaje Nanga akubali kumtangaza mshindi, halafu leo aseme hakushinda aliiba kura?.
 
Tishekedi anaonekana mbaya na wezi wa Rwanda kwakuwa hatekelezi matakwa ya Rwanda na washirika wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…