Ilikuwa tarehe kama ya leo january 2011

Ilikuwa tarehe kama ya leo january 2011

Tupo sana miaka ya shetani....... he he he......nimeangalia kidogo nikaona ID nyingi zilizochangia huu uzi ni RIP.....teh teh teh......ni makomandoo tu hustahimili vishindo.......

Walale pema huko walipo. .

Napenda kuwajulisha kwamba wimbo wa Taifa umebadilishwa na Darasa. ......Eti siku hizi unaitwa Muziki. ....
 
sijakuelewa mkuu uliposema hukuwahi kuwauliza mods kuhusu password yako, unataka kusema mods wanajua password zetu au?

Ha ha ha ha...

Labda wangeweza kunipa option ya kuweka password mpya au wangeweza kuunganisha ile ID ya Jambo Forums na hii ya Jamii Forums. .....
 
Tarehe kama ya leo, mwezi wa kwanza, mwaka 2011 (6th Jan 2011), Nilipata fursa ya kujiunga na Jamii Forums. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kudumu humu jamvini mpaka sasa ..

SABABU YA KUJIUNGA
Habari za SIASA motomoto nilizokuwa nikizipata miaka ile kwenye JAMBO FORUMS, ndizo zilikuwa chachu ya mimi kujiunga tena...

KWA NINI TENA?
Baada ya kukaa nje ya mtandao kwa muda mrefu, nadhani Jambo Forums waliondoka na password yangu... Nilijaribu sana kukumbuka password lakini niliambulia patupu...."Sikuwahi kupata wazo la kuwauliza Mods"

MAFANIKIO
Nimeweza kupata marafiki wengi ,ambao tunafurahi pamoja, tunashirikiana katika mambo mbalimbali.Kimsingi wamekuwa ni sehemu ya familia yangu....
Lini ningekwenda Tanga na kuenjoy kiviile kama sio JF? Big Up sana Arusha-WING, TA-WING na DAR-WING....

Nimeweza kufuatilia mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea Nchini,ya kupendeza,kuhuzunisha nk.... Daima nitashukuru kuwepo kwa Jukwaa la Siasa maana bila wao, hakika nisingefika hata huku Chit Chat....

SHUKRANI ZA PEKEE.

Ziwafikie Mods ambao mpaka sasa hawajawahi kunipa hifadhi kule BAN GUEST HOUSE... Nasikia kule kuna mateso balaa, alinidokeza Mungi . Muendelee na moyo huo huo, mkizidi kufanya kazi yenu kwa umakini, msinikumbuke kabisa katika huo ufalme wa BAN..

Pili kwa mume mpenzi Filipo ,kwa kunidaka juu juu.. Nakiri kwamba upinzani upo ,tena mkubwa toka kwa Smile , ladyfurahia , sweetlady Arabela amu ila sintolala usingizi kabisa.... Baadhi ya niliowataja kwa namna moja wanampenda au wanapendwa na mume wangu.... Nayahesabu kwamba ni mapungufu ya kibinadamu....
UJUMBE:
Mimi na Filipo hatukukutana barabarani ,na kama hamuamini angalieni lini tulijiunga JF....


Nawatakia Upendo, Furaha , na Mafanikio katika kila Jambo mtakalolipanga kwa mwaka huu mpya 2013...

Copy: PakaJimmy , Blaki Womani , Preta , Lily Flower , Arushaone , Mr Rocky , Mungi , Mzee wa Rula , LiverpoolFC , Erickb52 , Smile , Arabela , Dark City , madame V , Nicas Mtei na wengine ambao sijawataja...

nilikuwa wapi kuona hii kitu jamani kweli siku hizi nimekuwa mvivu kutembelea jukwaa hili

hongera sana kwa kuwepo jf kwa muda huo bila ban ila mwambie Filipo anipe mzigo wangu kabla sijaanza makeke hapa hahahahaha bestito hongera sana
 
Back
Top Bottom