Ilikuwaje Mkoa wa Mara ukaitwa 'Jamhuri ya Watu wa Chui'?

hii kitu ni halisi kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu walifanyiwa watu wa mara hasa serengeti na tarime, nilikuwa naishi mugumu enzi hizo baada ya vita ya kagera ilikuwa ni balaa, naikosa sana vita ya waikoma na wakurya ya kuibiana ng'ombe ilikuwa ni show down ya hatari.
 

Taratibu. Huyu nimeshamjibu kiungwana.
 

Aise hii hadithi nilikuwa siijui wataalamu wa document tutengenezeeni hii mtuwekee kwenye library kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo
 
Hii ishu ndo kwanza naisikia. Wenyeji wa huko mtuelezee vizuri ilkuwaje hadi huyo jamaa akaamua kuitangaza hiyo jamhuri?
 
ukombozi utaanzia uko uko this issue is like that of king mareale pale moshi alipomgomea nyerere akitaka mikoa ya kaskazini ijitenge na tz ndipo mwl akasema kua kamwe isije ikatokea watu wa kaskazini kupewa nchi waongoze.
 
Wakuu kwakweli kama kuna mambo yanayoumiza na kuhuzunisha ni kipindi hicho watu wa mara walitendewa unyama mbaya sana yaani ilifika hatua vijana wakalazimishwa kulala na mama zao na baba na mkamwana wake wanafanya tendo la ngono tena mchana mbele za watu kisa wanaombwa bunduki kuna watu hata leo wako tayari kutoa ushahidi na wengine wanawafahamu pili sababu kuu hasa ya nyamaghanya kutangaza taifa huru la ENGWE ni manyanyaso ya nyerere kukusanya ng'ombe za watu kipindi cha vita ya kagera kwamba wanachangia vita ya kagera sasa kuna bwana mmoja alikuwa akiishi kagera akaja pale gibaso akamwambia Amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya watu wa engwe kwamba uganda haikuvamia tanzania bali ikuwa ni mbinu ya mwalimu kumsaidia obote hata lile daraja lilipigwa na jeshi letu la tz nyamaghanya aliposikia hivyo akaitisha mkutano mkubwa GWITÖNGA akauliza vijana je mpo tayari kutetea mifugo na watu wenu ndindipo wote wakajibu tuko tayari siku hiyo saa tano na nusu usiku wimbo wa taifa tukufu la engwe ukapigwa na kupandisha bendera ya ngozi ya chui nina ushahidi na vielelezo hata mkivitaka leo wakuu ina umma sana kwa unyama ambao watu wa mara walitendewa na askari toka zanzibar ni kitu ambacho sintakisahau kamwe!!
 

Asanti moghaka!
 
Nakumbuka jinsi vijana kutoka visiwani walivyopora mali za wana-Mara na kuwafanyia manyanyaso yasiyo na kifani.
 
nakumbuka ile inshu...ilikuwa 1982....tanzania huko mkoani mara ilitokea vita kubwa...kati ya majeshi ya serikali na majeshi ya nyamahanga...ilidumu kama wiki tatu.....watu walikufa sana.....
 

ni pm mateja.
 
Watanzania kazi tunayo mbona na history ya kuchakachua,Ndo maana Mwalimu mmoja wa History pale Kigurunyembe Secondary School alikuwa hapendi kufundisha somo la History ya Tanzania akidai imejaa upotoshaji kwa kiwango cha kutisha mwanzoni sikumuelewa lakini kwa haya ninayoyaona hapa sasa nimemuelewa alikuwa na maana gani.
 
Aise hii hadithi nilikuwa siijui wataalamu wa document tutengenezeeni hii mtuwekee kwenye library kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo
huwezi kuijua kama ulizaliwa miaka ya tisini au 2000.
 
Kujitenga kuna mambo kadhaa ambayo ni kama vile
1.mtu kutoridhishwa na utawala wa nchi yake.
2.kuzorota kwa huduma muhimu za kijamii katika eneo lake.
3.mgawanyo wa rasili mali kutoka eneo hilo kuwaneemesha wachache haswa viongozi na ama maeneo viongozi wanayotoka ama vinginevyo
MKUU KICHULI naomba ni juze tafadhali kilichompelekea huyu Nyamaghanya kufanya hilo tukio la kistoria ambalo tuliowengi hatukulifahamu ni nini haswa?
 
 

Kuna taarifa kuwa mandela alivyotembelea Tanzania alitegemea kukuta bonge la nchi ....maana nyerere alikuwa anasaidia sana nchi zengine....
Lakini nyerere akatoka nduki kwa aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…