Baada ya VITA VYA KAGERA kumalizika kulikuwa na matatizo POST WAR TRAUMATIC DISORDER SYNDROME(PTSD) kwa Wanajeshi wetu,Wengi walipoteza maisha yao kwa visa mbali-mbali kama vile Unywaji wa pombe,Kugombea Wanawake na Ugomvi mwingine usiokuwa na maana,Tatizo hili la PTSD limeua Wanajeshi wetu wengi sana wakati huo ni kwa sababu tu Serikari yetu haikuweza kugundua na kubuni mbinu ya kuwasaidia Wanajeshi wetu waliopatwa na matatizo haya ya PTSD,Naamini kabisa kuwa Huyu ndugu NYAMHANGA alipata matatizo ya PTSD Ndiyo maana aliweza kuchukua silaha nyingi na kujenga Ngome yake pale GIBASO,Hakuwa yeye bali tatizo hilo la PTSD NDILO LILILOMFANYA ATENDE KITENDO HICHO.Maana Mwanajeshi akipata tatizo hilo anaweza kufanya Kitendo chochote kile ikiwa pamoja na wengine kuamua KUJINYONGA bila kuogopa yeyote yule,Hivyo ilitakiwa wakati huo Serikari yetu ingewaweka Wanajeshi wote waliopatwa na tatizo hilo sehemu maalumu ili kupatiwa Matibabu na Ushauri NASAHA mpaka watakapoonekana wamepona kutokana na PTSD Kwa nchi masikini kama yetu Haikuwa rahisi kugundua tatizo hili kwa Wanajeshi wetu na Tiba yake,Kwa Upande wangu mimi siwezi kumwita SHUJAA kwa kitendo alichofanya maana alikifanya sababu ya tatizo la PTSD Ugonjwa ambao huwapata Wanajeshi Baada ya kumaliza VITA.