Hydrobenga
JF-Expert Member
- Jun 24, 2012
- 1,127
- 212
Watanzania kazi tunayo mbona na history ya kuchakachua,Ndo maana Mwalimu mmoja wa History pale Kigurunyembe Secondary School alikuwa hapendi kufundisha somo la History ya Tanzania akidai imejaa upotoshaji kwa kiwango cha kutisha mwanzoni sikumuelewa lakini kwa haya ninayoyaona hapa sasa nimemuelewa alikuwa na maana gani.
Kuna taarifa kuwa mandela alivyotembelea Tanzania alitegemea kukuta bonge la nchi ....maana nyerere alikuwa anasaidia sana nchi zengine....
Lakini nyerere akatoka nduki kwa aibu
Taratibu. Huyu nimeshamjibu kiungwana.
Hapana. Hii taarifa ama umeitunga mwenyewe au uliingizwa choo cha kike na aliyekupa. Kabla ya kuwekwa kizuizini Mandela aliwahi kuja Tanzania. Kwa hiyo alijua kuwa ni nchi ambayo miundombinu yake bado haijaendelezwa. Haikuwa mara yake ya kwanza kutembelea Tanzania alipotoka kizuizini.Kuna taarifa kuwa mandela alivyotembelea Tanzania alitegemea kukuta bonge la nchi ....maana nyerere alikuwa anasaidia sana nchi zengine....
Lakini nyerere akatoka nduki kwa aibu
Kujitenga kuna mambo kadhaa ambayo ni kama vile
1.mtu kutoridhishwa na utawala wa nchi yake.
2.kuzorota kwa huduma muhimu za kijamii katika eneo lake.
3.mgawanyo wa rasili mali kutoka eneo hilo kuwaneemesha wachache haswa viongozi na ama maeneo viongozi wanayotoka ama vinginevyo
MKUU KICHULI naomba ni juze tafadhali kilichompelekea huyu Nyamaghanya kufanya hilo tukio la kistoria ambalo tuliowengi hatukulifahamu ni nini haswa?
Hapana. Huyu alikuwa hana nia ya kupindua serikali ya Tanzania. Yeye alichofanya ni kujimegea eneo lake na kutangaza Jamhuri ya watu wa chui. Na Jamhuri yake ilikuwa inaishia eneo moja tu Tarime.
Ilikuwa ni baada ya vita vya Uganda. Jamaa alikuwa kama ana wazimu vile.
..........kwa kuzingatia hapo no. 3, ina maana wale jamaa wa Mombasa (MRC) hapo nchi jirani wana hoja eeeh ?
Kuna taarifa kuwa mandela alivyotembelea Tanzania alitegemea kukuta bonge la nchi ....maana nyerere alikuwa anasaidia sana nchi zengine....
Lakini nyerere akatoka nduki kwa aibu
Nyamaghanya alikuwa jembe kweli na ni shujaa wa kweli wa mkoa wa mara nakumbuka mwaka 1982 alitangaza jamhuri ya watu wa chui nami nikiwa miongoni mwa wakazi wa nchi yake makao makuu yakatangazwa kuwa ni GIBASO na mishahara ya watumishi wake ni ng'ombe alikuwa na jeshi hodari sana likiitwa Esaiga ya gesambiso na vijana wa kati ambao walikuwa hodari wa kupiga mishale ndipo mchongameno akaamua kumwaga jeshi lake toka zenji kuja kumsaka shujaa wa wanamara wakashindwa kumkamata ikabidi watumie mbinu ya kupitia kwa mke wake mdogo ndipo akauwawa au akajiua mwenyewe kwenye mashimo ya gwisalaa hakukamatwa wala hakuzikwa mwili wake ulifichwa ili kukwepesha mauaji zaidi toka jeshi lake
Baada ya VITA VYA KAGERA kumalizika kulikuwa na matatizo POST WAR TRAUMATIC DISORDER SYNDROME(PTSD) kwa Wanajeshi wetu,Wengi walipoteza maisha yao kwa visa mbali-mbali kama vile Unywaji wa pombe,Kugombea Wanawake na Ugomvi mwingine usiokuwa na maana,Tatizo hili la PTSD limeua Wanajeshi wetu wengi sana wakati huo ni kwa sababu tu Serikari yetu haikuweza kugundua na kubuni mbinu ya kuwasaidia Wanajeshi wetu waliopatwa na matatizo haya ya PTSD,Naamini kabisa kuwa Huyu ndugu NYAMHANGA alipata matatizo ya PTSD Ndiyo maana aliweza kuchukua silaha nyingi na kujenga Ngome yake pale GIBASO,Hakuwa yeye bali tatizo hilo la PTSD NDILO LILILOMFANYA ATENDE KITENDO HICHO.Maana Mwanajeshi akipata tatizo hilo anaweza kufanya Kitendo chochote kile ikiwa pamoja na wengine kuamua KUJINYONGA bila kuogopa yeyote yule,Hivyo ilitakiwa wakati huo Serikari yetu ingewaweka Wanajeshi wote waliopatwa na tatizo hilo sehemu maalumu ili kupatiwa Matibabu na Ushauri NASAHA mpaka watakapoonekana wamepona kutokana na PTSD Kwa nchi masikini kama yetu Haikuwa rahisi kugundua tatizo hili kwa Wanajeshi wetu na Tiba yake,Kwa Upande wangu mimi siwezi kumwita SHUJAA kwa kitendo alichofanya maana alikifanya sababu ya tatizo la PTSD Ugonjwa ambao huwapata Wanajeshi Baada ya kumaliza VITA.
Hapana. Huyu alikuwa hana nia ya kupindua serikali ya Tanzania. Yeye alichofanya ni kujimegea eneo lake na kutangaza Jamhuri ya watu wa chui. Na Jamhuri yake ilikuwa inaishia eneo moja tu Tarime.
Ni story ndefu iliyoanza baada ya Vita vya Kagera baada ya Watu wachache akiongozwa na Kiongozi wao kujitangazia Utawala wao na Uongozi wao Miaka hiyo. Kuna wakati huyu jamaa alikamatwa na Mwl Nyerere wakati huo akiwa Rais aliomba wamlete kwake, jamaa aliomba msamaha na kuagizwa asitishe Vita akasamehewa.
Mtiti ulianza tena kwenye miaka ya 1984 hapo ndipo kumbukumbu zangu zitakapoanzia maana naikumbuka vzr sana operation hii maarufu kama "Operation Nyamaganya" ilitolewa amri popote alipo apatikane akiwa hai au amekufa.
Haikuwa rahisi kumpata ilikuwa vita iliyohusisha Majeshi yetu yote tunatoyafahamu ikiwa ni pamoja na Usalama wa Taifa ambao kwa kiasi kikubwa walichangia kumsoma huyu Rais wa Ingwe (Chui).
Hatima yake huyu jamaa aliuwawa yeye na Mwanae katika mapambano makali yaliyodumu kwa muda mrefu.
CJAHITIMISHA BUT NAWASILISHA.