Ilikuwaje mpaka ACP Abdallah Zombe akanusurika kufungwa?

Ilikuwaje mpaka ACP Abdallah Zombe akanusurika kufungwa?

Aliteuliwa kuwa jaji kutokea wapi? Muda kidogo maana yake nini?
Alikuwa wakili wa kujitegemea ofisi zake Morogoro,akateuliwa kuwa jaji, kesi ya Zombe ilimkuta akiwa senior jaji tayari,na kabla hajasoma hukumu tayari alishakua Jaji mteule wa mahakama ya rufani ya tanzania,ni moja ya majaji walio nyooka sanaaa ndio maana hutaona majaji wa kariba yake wakiwa assigned kesi za kisiasa zile za kupoteza muda.

By the way,jamaa alikua jaji 2004
 
Si haba. Haiyumkiniki tunasogea. Pole pole ndiyo mwendo.

Kiswahili hakijawahi kuwa rahisi kihivyo mjomba, hasa pande za kwetu buseresere.

"Muda kidogo" au "ndiyo kwanza" kwani kwa uelewa wako ni kama muda gani?
Wenye kiswahili chao wanaelewa nilichomaanisha, pole sana kwa kutoka uswekeni hiyo mimi hainihusu.
 
Zombe alimpotosha Bageni kama kiongozi wa wenzie wauaji, Bageni akijua Zombe wako wote akaingia chaka at the end Bageni ikala kwake Zombe yuko huru...Koplo Saad Alawi mpaka leo hajulikana alipo....hahahahaha ila Karma inamtafuna sasa..
 
Pitia series kwenye gazeti la mwananchi imeandikwa vizuri sana. Kiufupi ni ujinga na uzembe wa serikali. Zombe alishitakiwa kwa mauaji, na hakuua wa kuwepo eneo la tukio. Hata kama ni kweli alitoa amri, je sheria zetu zinasema ukituma au kutoa amri ya kuua kinyume na sheria ni kosa la kuua? Ndio maana akatoboa kirahisi, halafu Jamhuri baada ya kuona imechemka, ikamuomba Jaji ampate na hatia ya kupanga mauaji. Wakaambia hiyo sio kesi iliyopo hapa.

Bageni aliyekuwepo eneo la tukio na ndie alikuwa most senior officer yeye alihukumiwa kunyongwa baada ya serikali kukata rufaa.

Wanasheria wa serikali uzembe hawajaanza na kesi ya Mbowe, ndio jadi yao.
Hivi huyo Zombe bado yuko hai!
 
Hivi huyo Zombe bado yuko hai!
Yupo sana

1633709015348.png
 
Ushahidi uko wazi kabisa juu ya order alizotoa kwenye mauaji yale ya wafanyabiashara ikawaje yeye hakukutwa na hatia? Inanikumbusha picha moja ya kihindi inaitwa "Andha Kanoon" maana yake "Sheria Kipofu"

Wakuu ilikuwaje mpk Zombe akanusurika kufungwa? Karibuni
Ni kama kesi ya Sabaya!

Kuna techinc inachezwa kwenye uandishi wa mashitaka ndiyo inayokuja kuvuruga hukumu.

Mfano Sabaya alikuwa mkuu wa wilaya ambaye ni mtendaji wa serikali, pia yupo kwenye kamati ya ulinzi na usalama ambao katika majukumu yao ni pamoja na kuzuia na kukamata.

Sasa alipoenda kukamata na kulengeshewa rushwa, mwandika mashitaka kaandika ujambazi wa kutumia silaha badala ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka!

Kwenye hukumu waweza kuta akatemwa, si kwasababu hajafanya kosa, lah hasha, isipokuwa alichoshitakiwa nacho ni tofauti na alichotenda.
 
Si haba. Haiyumkiniki tunasogea. Pole pole ndiyo mwendo.

Kiswahili hakijawahi kuwa rahisi ki hivyo mjomba, na hasa pande za kule kwetu buseresere.

"Muda kidogo" au "ndiyo kwanza" kwani kwa uelewa wako ni kama muda gani?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]! Yaani mmeamua kuingia class kabisa
 
Ushahidi uko wazi kabisa juu ya order alizotoa kwenye mauaji yale ya wafanyabiashara ikawaje yeye hakukutwa na hatia? Inanikumbusha picha moja ya kihindi inaitwa "Andha Kanoon" maana yake "Sheria Kipofu"

Wakuu ilikuwaje mpk Zombe akanusurika kufungwa? Karibuni
Nimeota Kingai katolewa Kafara
 
Back
Top Bottom