Kweli mkuu, yule Mzee ni mwongo Sana.
Eco...
Lakini mimi sijaandika "vijarida."
Mimi nimeandika kitabu na kikawa mashuhuri kwa kufikia kutiwa katika Cambridge Journal of African History.
Wala si mimi niliyokitangaza dunia nzima.
Kitabu kimetangazwa na mabingwa wa historia ya Afrika: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.
Nikaalikwa Northwestern University.
Nikatiwa katika mradi wa Harvard na Oxford University Press kuandika Dictionary of African Biography.
Nikatiwa katika mradi wa Nyerere Biography.
Nikatiwa katika mradi wa Magufuli kuandika historia mpya.
Hivi si vijarida.
Wala mimi si muongo.
Allah ameniepusha na sifa hiyo.
Alhamdulilah.
Lakini akutukanae hakuchagulii tusi.
Kalamu yangu imebadili historia ya uhuru wa Tanganyika.
Leo mnamsoma Abdul na Ally Sykes katika historia ya TANU na mnamsoma baba yao Kleist Sykes katika historia ya African Association.
Halikadhalika mnamsoma Sykes Mbuwane katika historia ya German Ostafrika.
Leo mnamsoma Mufti Sheikh Hassan bin Ameir katika historia ya kupigania uhuru halikadhalika mnamsoma Sheikh Suleiman Takadir.
Leo mnawasoma Denis Phombeah na Dome Budohi hawa mmoja anatoka Nyasaland mwingine Kenya kadi zao za TANU No. 5 na 6 na walikuwa viongozi wa TAA.
Nyaraka za Sykes zimetufungulia haya yote.