Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

Ilikuwaje Nyerere akamshinda Sykes?

waingereza ndio walimchagua Nyerere , kama ulikuwa hujui !! Mpango wa kuunganisha zenji na Tanganyika Nyerere alipewa maelekezo na waingereza ila sio akili yake ....Unajua kwa nn?


Kumchagua Nyerere ndio mtu pekee alikuwa brainwashed angeweza kuendeleza mipango yao ya kuwa kibaraka "'Puppet'' ....

Kwa hivyo wale wazee wa Anatoglou waliokuwa wanapambana dhidi ya mwingereza walimchagua Nyerere kwa maelekezo ya mwingereza?. Nadhani umetoka nje ya mada.
 
Kulingana na mahojiano ya Tundu Lissu na mtangazaji wa ITV , Lissu alidai mara ya Mwisho CCM kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti kwa ushindani ilikuwa mwaka 1954 kati ya Julius Nyerere na Abdulwahid Sykes. Ambapo Nyerere alimbwaga Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Anatoglou.

Swali la msingi ilikuwa ni kwamba ilikuwaje Nyerere amshinde Sykes ambaye alikuwa ni mtoto wa hapa Dar na baba yake alikuwa kiongozi wa TAA hapo kabla. Yani Nyerere kutoka Musoma aliwezaje kuwashawishi wajumbe wamchague yeye wamuache Sykes wa Dar.

Tusaidiane mbinu alizotumia Nyerere kushinda uchaguzi huo maana haikuwa rahisi.


AKILI NDUGU YANGU, AKILI.
 
Kama walik

Kama walikubaliana kumwachia Nyerere kwanini waliingia kwenye kinyang'anyiro Hadi akwashindwa hata kama unasema ni kwa kura chache

Hapo ndipo Mimi nashangaa pia. Yani Sykes wakubaliane kumuachia Nyerere halafu baadae aje agombee Tena. Hapo Mzee Said anatudanganya.
 
Vyovyote vile ila kwa akili za kawaida sidhani kama mwingereza alikaa tu pembeni akisubiri hatma bila kulinda maslahi yake. Pamoja na yote JN amefanya kazi kubwa mno kuliunganisha taifa. Nchi haina deni naye.

Kweli kabisa mkuu
 
Huwa sikisii:
View attachment 3080206

Hapo nyerere kawachwa kwenye mataa, Malkia anaongea na mtawala wa kweli, Joan Wicken, alipokuja Dar.
Huyo Malkia hakumuona Sykes,au Sykes alikuwa hajui kiingereza?

Ilim kweli ilikuwa ni muhim sana tokea tangu na tangu.

Yaani mtoto wa Kijijini Nyerere anapewa attention na malkia kuliko mtoto born town tena Kariakoo kabisa Sykes?
 
Unakua rais,unavunja taasisi ya waislam ya afrika mashariki,serikali yako,kwa miaka 25 haiteui waziri wa elimu muislam ila unateua padre kuwa waziri,na wanaofaulu na kupata elimu za juu ni watu wa dini yako kwa 75+%,mdini nani,nani mpandaji wa mbegu ya udini!?
Uteue waziri wa elimu Muslim ili akajaze madrasa badala ya madarasa?.

Nyerere alikuwa sahihi
 
Yule mzee nilikwishamdharau sana. Anataka kupaka rangi kwenye upepo. You can't undo history ya Tanganyika ambayo ndiyo iko kwenye syllabus ya NECTA kwa kuandika vijarida na kupeleka Ulaya kwenye idara za African history za vyuo vikuu vya huko. Hakuna lolote zaidi ya ujahidina Mohamed Said

Kweli mkuu, yule Mzee ni mwongo Sana.
 
CCM ilizaliwa mwaka 1977 hiyo taarifa siyo sahihi, CCM ilitokana na muungano wa vyama vya Tanu na ASP.
Waislamu wakati wakudai uhuru waliweka mbele maslahi ya taifa tofauti na makabila mengine Kama wachaga waliotaka uhuru wa peke yao.


Waislamu waliokuwa na Nyerere ni wale waislamu kweli na sio Hawa wanaotanguliza udini mbele na kujiona wao ni daraja jingine.
Uhuru ulichangiwa na watu wengi na Nyerere aliendelea kuwatumia hasa linapotokea Jambo zito aliwaita na kushauriana nao pamoja na kwamba wengi hawakuwa na elimu kubwa walikuwa na hekima na busara.

Unaelewa maana ya Succession?. CCM imetokana na TANU na ASP, hivyo TANU ikafa ikazaa CCM.
 
And u think Nyerere was just a bum and dummy?

Nyerere was and is still the brightest mind Africa has ever produced

Nyerere's thinking and outta-this-world oration capacity was next to none...

In a minute he influenced all the voters to vote for him..

Stop this nonsense thinking Nyerere was in the same lower level Sykes was in....

It was like Mercedes Benz S Class compared to a beat up Toyota GX100...what a loss

I got you. Thanks
 
Kweli mkuu, yule Mzee ni mwongo Sana.
Eco...
Lakini mimi sijaandika "vijarida."
Mimi nimeandika kitabu na kikawa mashuhuri kwa kufikia kutiwa katika Cambridge Journal of African History.

Wala si mimi niliyokitangaza dunia nzima.

Kitabu kimetangazwa na mabingwa wa historia ya Afrika: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Nikaalikwa Northwestern University.

Nikatiwa katika mradi wa Harvard na Oxford University Press kuandika Dictionary of African Biography.

Nikatiwa katika mradi wa Nyerere Biography.

Nikatiwa katika mradi wa Magufuli kuandika historia mpya.

Hivi si vijarida.
Wala mimi si muongo.

Allah ameniepusha na sifa hiyo.
Alhamdulilah.

Lakini akutukanae hakuchagulii tusi.

Kalamu yangu imebadili historia ya uhuru wa Tanganyika.

Leo mnamsoma Abdul na Ally Sykes katika historia ya TANU na mnamsoma baba yao Kleist Sykes katika historia ya African Association.

Halikadhalika mnamsoma Sykes Mbuwane katika historia ya German Ostafrika.

Leo mnamsoma Mufti Sheikh Hassan bin Ameir katika historia ya kupigania uhuru halikadhalika mnamsoma Sheikh Suleiman Takadir.

Leo mnawasoma Denis Phombeah na Dome Budohi hawa mmoja anatoka Nyasaland mwingine Kenya kadi zao za TANU No. 5 na 6 na walikuwa viongozi wa TAA.

Nyaraka za Sykes zimetufungulia haya yote.
 
And u think Nyerere was just a bum and dummy?

Nyerere was and is still the brightest mind Africa has ever produced

Nyerere's thinking and outta-this-world oration capacity was next to none...

In a minute he influenced all the voters to vote for him..

Stop this nonsense thinking Nyerere was in the same lower level Sykes was in....

It was like Mercedes Benz S Class compared to a beat up Toyota GX100...what a loss
Hakuwa chocote bali mdini tu, dictator, funga mikanda miaka mia nane, mateso kwa watanzania hadi kuvaa magunia na kula mizizi, neema kwa watanzania ilianza kuonekana 1986 baada ya mzee Mwinyi kushika inchi
 
Back
Top Bottom