Wewe na huyo unaemjibu mnatofautiana katika tafsiri ya maana ya dini! ... dini kwako wewe ni kukiri imani sahihi ni ipi wakati huyo unayejadiliana nae kwake tafsiri ya dini ni mfumo wa maisha ya mwanadamu. So ukiangalia kimaana mnajadali vitu viwili tofauti kabisa katika jina moja, kamwe hamuwezi kufikia muafaka isipokuwa mtakwazana tu wakati kila mmoja yupo sahihi kulingana na mafundiso ya dini yake.Ndugu huu ni ushauri pengine ni nje ya mada. Mgalatia mchukulie kama ndugu yako. Safari yetu ni moja tunamtafuta Mungu, tufike kwake tukiwa wakamilifu. Labda tumetofautiana usafiri tunaotumia lakini dhamira yetu ni moja.
Tunaamini katika Mungu, basi mtangulize yeye kwanza kwenye kila jambo. Dini isiwe sababu ya kumuona John ni kafiri, Jesca ni wa motoni. Kama dini fulani ingekua ndio tiketi ya kuiona pepo bila kuangalia uhalali wa matendo basi maisha yetu ya kiimani yangekuwa mepesi sana.
Sio lazima unijibu hili swali ila fanya hivi, Jirani yako hana dini na hajawahi kumkufuru Mungu kwa namna yoyote ile amekuwa akiishi katika matendo ya kupendeza, kusaidia maskini, haibi, hadhulumu, hasemi uongo nk..lakini ni hana dini.
Wewe unaamini dini yako ni ya haki na kweli unaswali swala tano sawa, lakini wewe ni mwizi, jambazi, mzinzi, unadhulumu yatima na Wajane nk lakini una dini na unaswali fresh tu.
Narudia tena sio lazima unijibu ila jiulize ni yupi ana nafasi mbele za Mungu? Kwamba atamchoma moto Jirani kwa kuwa hakuwa wa dini fulani na atakuchagua wewe kwa kuwa wa dini fulani?
Mwenyezi Mungu ameweka kitu ndani yetu, uwe una dini usiwe na dini, uwe unaamini Mungu uwe haumini ila unapotenda jambo jema unajua na unapotenda jambo baya unajua. Labda ndio tunda la mti wa mema na mabaya.
Unaweza kukutana na comments zangu kwenye mijadala mbalimbali hapa Jf hasa ya kidini ila sijawahi kumchukia mtu asiye wa imani yangu kwa namna yoyote ile. Nikimchukia Muislamu ni sawa na nimemchukia rafiki yangu wa toka utotoni, ni sawa nimewachukia Mama zangu wadogo, Dada zangu na wadogo zangu.
Nikiona kuna mtu anatumia dini kuhubiri chuki, anatumia dini kugawa watu huwa lazima nimjibu, japo sipendagi muendelezo naamini jibu langu moja au swali langu linatosha umeshindwa kubadilika basi Mungu awe pamoja nasi.
Leo unamuita Mgalatia, Kesho kafiri, kesho wanaajiri wao tu, wiki ijayo serikali inawapendelea yanaanza machafuko.
Mungu wetu ni wa wote, tujitahidi kupendana. Kukinzana mawazo kupotu lakini kusizae chuki. Kama wote wote tunatoa damu nyekundu, haijalishi rangi zetu, dini zetu. Basi sisi ni wa baba mmoja.
What you guys are missing (na hii ni mostly upande wa Christians) ni kuto-acknowledge na kutambua hoja za Waislamu dhidi ya mfumo kandamizi dhidi ya Uislamu uliotengenezwa kipindi cha awamu ya kwanza (nasema hivo kulingana na hoja zinazotajwa kuwa na uzito wa kustahili kusikilizwa). Hapa ni lazima mambo yajadiliwe kwa hoja na sio ushabiki.
Kufumbia macho manung'uniko ya upande mmoja ni kulea tatizo linalokuwa siku hadi siku.