Nilianza kufanya kazi nikiwa bwana mdogo sana baada ya muda alikuja ajiliwa msichana mmoja hapo idarani kwetu, hakuwa amenizidi sana umri ila alikuwa mkimya kupitiliza.
Yeye kazi zake zilikuwa nyingi zaidi asubuhi ila mimi asubuhi huwa sina kazi sana hivyo kiubinaadam huwa napata huzuni hivyo huwa nikifika naanza kumsaidia kazi zake, hapo ndo tatizo lilipoanzia, baada ya muda akaanza kunizoea, akaja jua mimi nimtani wake wa kabila hivyo tuaanza kutaniana taniana, nikaja jua kama ameolewa hivyo nikawa namheshimu sana.
Sasa ghafra akaanza utani wa kuvuka mipaka, manzoni nilimpuuzia ila baadae akazidisha, akaenda zaidi kuniambia matatizo yake na mumewe jinsi anavyoteseka.Basi ijumaa moja kama utani nikamwambia kama anamaanisha anachosema basi aje jumamosi na nikamuelekeza, jumamosi kama muda wa saa tatu asubuhi kanipigia simu kuwa ashafika nilipomuelekeza, nikajua labda utani kweli kwenda namkuta basi nikampeleka hadi geto ila, ilikuchukua muda sana kumvua nguo maana anadai hakuwahi kuchepuka ila mwisho nikala mzigo.
Baada ya kula kula mzigo kama miezi 6 nikasia sikia tetesi kutoka wanyakazi wenzetu kuwa anaujauzito ila kila nikimuuliza alikuwa anakataa, basi mikasema haya hayanihusu mi nikaendelea kula mzigo. Ila baadae alinambia mwenyewe kuwa ni kweli ana ujauzito na ni wangu ila akanambia, akija jifungua salama atanambia.
Baada ya miezi 9 alijifungua salama,siku moja ndo akanambia story nzima kuwa baada ya kukaa muda mrefu bila ya kufanikiwa kupata ujauzito walienda hospital kupima ila jamaa ndo akaonekana anatatizo hawezi kutungisha mimba lakini cha ajabu jamaa hataki kuwaambia ndugu zake na ndugu zake mwanaume kila mara wanamsema na yeye mwanaume anaungana na ndugu zake kumsema, hivyo ndo akaamua kutafuta mtoto mwenyewe.
Yule mwanamke alinipenda sana, yule mtoto anafanana na mimi sana ila jamaa hainijui kabisa, nilikuwa kwenye mahusiano na yule msichana kwa miaka 8 ila hata tunaofanya nao kazi idara moja hawajaweza hata kutuhisi.
Yule jamaa aligoma kumlea yule mtoto kabisa ila mimi nilimsaidia sana yule mwanamke mana najua kisheria si mwanangu ila sikutaka mtoto apate shida kwa ujinga wetu, hadi siku mtoto anataka kubatizwa mwanamke akaniletea karatasi ambalo kunasehemu ya kuandika jina la mtoto, mimi nikaandika jina nililopendekeza nae akafurahi.
Nilimsaidia kulea mtoto hadi alivyofika miaka 5 yaani hadi mtoto anajua kuwa mimi ni baba pia maana alikuwa anakuja nae sana kwangu, ila mwisho nikamuomba yule mwanamke aendelee na mumewe, alilia sana ila niliacha kazi pale nikabidirisha namba ya simu pia hadi sasa tangua tuachane ni miaka 4.
Ila mwisho alinambia huyu jua ni mwanao, akikua nitamwambia ukweli wote kama akiamua kukutafuta sawa.