Mkuu kwani wewe ni ngebo pia? Maana nilitaka adadavue jinsi alivyomuanza kumuimbisha mwalimu wake na kisha kupata alichokitaka.
Simulizi inaanza hivi, ingawa ni ndefu: Huyo mwalimu ndiye alinifundisha kuandika nikiwa darasa la kwanza.
Nimezaliwa 'mashoto', wakati naanza kujifunza kuandika nilikuwa natumia mkono wa kushoto.
Enzi hizo tulianza kujifunza kuandika kwa kuchora chini, mkitoka hapo mnapewa tablet za mbao na chaki na mkitoka hatua hiyo, mnaanza kutumia karatasi zenye line pana mchanganyiko na nyembamba pamoja na penseli maalumu zenye mrija mpana.
Kuhangaika kote huko, kuanzia kuchora chini, kuandikia ubao akawa ananipa tu ushirikiano na shoto langu.
Tulipofika hatua yakuanza kuandikia karatasi, akanigeuka kidhalilishaji.
Siku1 wakati nahangaika kuandika alikuja akanifinya kitoto, yaani mashavu yote kwa mikono miwili, akani'hook' juu kwa kutumia mashavu aliyonifinya kisha akanikita na konzi zito la adabu na kusindikiza kwa maneno...'nije nikuone tena unaandikia huo mkono wako wa mavi utaniona'...dah!
Ebanaeeh, alinivuruga kisaikolojia na kuanza kujilazimisha kuandikia mkono wa kulia, kifupi alinirudisha nyuma!
Kiukweli alinikomesha, maana nilijilazimisha hivohivo hadi nikazoea lakini mwandiko wangu sasa, ni mbovu hadi leo.
Moyoni halikunitoka hilo tendo na kupanga kwamba nitakapokuwa mkubwa na mimi atanikoma, hayo yalikuwa ni maneno tu ya ghadhabu, lakini sikujua nitamkomeshaje.
Mawazo hayo yalikuwa kama sala vile, maana nilipo maliza masomo na kupata kazi, tulikuja kukutana naye nishakuwa mkubwa nikamtongoza bila yeye kunifahamu background ya ninayemtongoza.
Alijikakamua kunibeza kwamba mi ni mdogo sana kwake, kwa nini namueleza upuuzi kama huo, maana nilianza kwa kumuamkia ....' shikamoo damkubwa'...
Nikakazia maneno yangu, kisha tukaishia kuwa wapenzi.
Nilichokuja kukigundua ni kwamba penzi kwa ajili ya kulipa kisasi ni tamu sana kuliko penzi la kawaida na usipokuwa makini linaweza kuvurugia 'future' zako.