A QUEEN
Senior Member
- Jul 26, 2019
- 118
- 246
Ni aibu sana kitu unafanya kwa siri ghafla kikajulikana hadharani🙌. Upande wangu kama ambavyo ilivyo kwa watoto wengi hasa wa kike nilikatazwa kutumia simu mpaka nifike kidato cha nne,jambo ambalo binafsi sikukubaliana nalo.Nilipewa hela ya tuition nikanunua simu kiswaswadu nikawa natumia kwa siri baadae ile simu mama yangu akaikuta akaificha😁😁
Ni hivi mpaka Leo sikumbuki aliikuta vipi mara ya kwanza ila ninachokumbuka mpaka Leo ni jinsi alivyonifuma nayo mara ya pili.Mara baada ya kugundua alipoificha ile simu(chumbani kwake kwenye begi analoweka khanga na vitenge vyake chini kabisa)nikawa naenda kuchukua ile simu natumia weekend nairudisha.Siku moja niko chumbani akapigiwa simu ya msiba nikajua hapa lazima lile begi litaenda kufunguliwa ilibidi niirudishe bila kupenda.Nikamkuta kakaa living room nikamuomba kuingia chumbani kwake nikachukue mafuta hapo simu nimeibana kwenye kanga ila ghafla ikadondoka chini😭😭
Nimeona mahali nikakumbuka hii kitu nikaona nilete huku tukumbushane ya zamani.