Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Umeongea vizuri sana na kwa utulivu, lakini na wewe naona uko gizani kama wengine. Kujitenga na dunia siyo lazima useme hadharani kwamba hutaki kushirikiana na dunia, au uamue kuvunja mahusiano ya kidiplomasia. Unaweza ukawa bado uko kwenye mahusiano na wenzako lakini hutui ushirikiano wa kutosha na unafanya mambo kinyume na utaratibu uliokubalika.

Raisi Magufuli aliliingiza taifa kwenye giza nene kwasababu zisizokuwa za msingi, KIBURI, JEHURI, HADAA, MABAVU na UJUAJI. Hivi unadhani kulikuwa na ulazima wowote wa kuzuia ndege zetu zisiruke nje ya nchi yetu ??? Moja ya sababu ya ndege kutoruka na kuogopa kukamatwa kwasababu ya madeni yalitokana na sisi kutoheshimu baadhi ya mikataba ya kimataifa ya uwekezaji (Bilateral Investment Treaties- BIT's).

Sasa kukupasha tu, kule chini maneno ya Mtwara kuna muitalia alipewa ardhi kwa ajili ya uwekezaji. Tanzania na Italy tulisaini BIT. Moja ya kanuni kubwa kabisa kwenye BIT ni Rule Against Expropriation and The Most Favoured National. Ikatokea vijana wa Magufuli wakiwa wamepewa amri kwamba wanyang'anye ardhi ambayo haijaendelezwa, kumbe kuna utaratibu wao wakanyang'anya.

Sasa jamaa akapeleka kesi kwenye mahakama za kimataifa akawa anavizia mali zetu: Lakini ukweli ni kwamba Mzee alishauriwa afuate utaratibu lakini alipuuza kwa madaha. USALAMA WA TAIFA wakamshauri sasa amualike jamaa aje Tanzania ili wakubaliane, kumbe jamaa walikuwa wanataka akifika tu wamkamate na kumtandika kesi za kutosha. Jamaa akawa mjanja akitoa masharti wakutane naye nje ya nchi.

Hebu tafuta kesi ya SUNLODGES V Tanzania (Expropriation Case) maana nimeona wewe walau una akili kuliko hawa vijana wengine ambao kazi yao ni kupiga vigelegele ilhali hawafamu kitu.....

Sasa hii ni akili ya wapi kweli, hivi idara za USALAMA WA TAIFA hali zikifahamu kwamba mikataba imesainiwa na nji na kuna utaratibu wa kujitoa. Kwanini wasaidie utekelezaji wa mambo ambayo mpaka sasa yamekuwa na madhara makubwa kwa taifa letu ???
 
Mkapa alikuza uchumi na kusamehewa madeni lakini kumbuka acacia wameingia kipindi chake hakukua na mgodi mkubwa tofauti Williamson diamond mine
 
Unajua ni kwa nini Nyerere alikuwa reluctant kufungulia uchimbaji holela wa madini?
Alikuwa ana akilizi za ziada kuliko maraisa wote wa Tanzania, lakini pia Tanzania lilikuwa ni taifa changa bado.

Alikataa kuruhusu madini yachimbwe hili linakubalika, lakini alifuata kanuni na taratibu za dunia na sheria za kimataifa: Tena alifanya kabisa majadiliano na ushirikiano hata na watu ambao alikuwa hakubaliani nao. Ndiyo Tanzania ilifanikiwa sana kwenye nyanja nzima ya Kidiplomasia......
 
Nakubaliana kabisa na wewe, lakini mkakati wa kujikwamua kutoka kwenye hiyo mifumo ya kibeberu ni ipi ???
Unaufahamu mchezo wa CHESS ??? Siku zote anayemshinda ni yule mwenye kusoma vizuri na kutabiri hatua za adui.
Niliipata point yako mkuu. Tunatakiwa kujikwamua kwa akili na tahadhari ya hali ya juu. Si kwa makelele na vurugu kama walivyokuwa wanafanya watu tuliowaamini kuwa wana uelewa mkubwa wa mambo.
 
Mwendazake ameifilisi Tibisii na kundi lake
 
I believe 'diplomacy is an art of compromise'
My maan, my maaan! You have made my day.
Tungekuwa jirani ningekununulia hata kawaha ndugu yangu, umezungumza nilichokuwa nakitafuta humu ndani.

DIPLOMACY is an art of maintaining communication and relations among nations. It also includes virtues like compromise, reciprocity, consensus, consent and good-faith. Babu Nyerere was a master of this, that's why he left us a hefty fortune of diplomatic clout.

Raisi Magufuli and his cronies were unstable, dangerous and volatile, ameacha madhara makubwa mno kwa nchi, lakini kuna watu bado hawataki kukubali ukweli ambao uko wazi.....
 
Ni kama nakuelewa brother, lakini tukimjudge Magufuli kwa kuangalia angle moja tutakuta hakuna alichokifanya

Kitu ambacho kwa maoni yangu, si kweli.
 
Umeegemea kwenye point ya mwisho kabisa, na hayo mawazo yako ni yakimaskini na kutokujiamini. Baadala ya kuchakata kichwa tunafanyaje na rasilimali zetu. Unakimbilia kujihusisha na dunia ndo wewe utakuja kutusainisha Hadi ushoga ili upate misaada
Mkuu, mbona tumejadiliana vizuri tu tokea mwanzo na sijakutuhumu wala kukukashifu kwa chochote kile mkuu. Kwanini uanze kunitolee kashfa mbaya kama hizi ilhali mimi sijakutenda chochote ???
 
Mwendazake tu acha kusingizia watanzania wote
 
Sasa Kama kikwete naye kakosea, magu kakosea tuchukue kipi Sasa. Kama kikwete aliweka diplomasia na uhusiano ikawa hola haya magu kajisolate kajipigapiga tumefika hapa tulipo hafu unasema tumerudi 25 years nyuma Tena.
 
Ndugu yangu Malcom, in all honesty, taja machache (notable) kati ya hayo mengi sana Magufuli aliyofanya vizuri.
  • Ujenzi wa miondombinu mikubwa ya kimkakati.
  • Uandishi mkubwa wa marudio ya sheria za nchi.
  • Kurudisha nidhamu ya kazi kwenye utumishi wa umma.
  • Kuwapa nafasi za uongozi vijana na wanawake.
  • Kuimarisha (Syncronization) mfumo wa ukusanyaji mapato ya serikali (GEPG)
Sasa njia zilizotumika kufanikisha haya ni suala jingine ambalo linahitaji mada yake, lakini katika haya nasema mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Japo ukweli utabaki kwamba alivurunda kwenye mambo mengi tu nyeti na ya msingi, kiasi ambacho kilihatarisha na kufunika haya mafanikio yake.
 
Ni kama nakuelewa brother, lakini tukimjudge Magufuli kwa kuangalia angle moja tutakuta hakuna alichokifanya

Kitu ambacho kwa maoni yangu, si kweli.
Nakubaliana kabisa na wewe, hatutakiwi kumhukumu mwanadamu katika upande mmoja. Kuna mambo mazuri sana Raisi Magufuli ameifanyia nchi: Japo lengo la huu uzi ni kutaka kufahamu kwanini wale wataalamu kutoka TISS, JWTZ, Foreign Affairs, BoT na Ministry of Finance waliamua kuunga mkono na kufanikisha mambo ya hovyo yaliyokuwa yanafanywa na Raisi Magufuli ilhali wao wanafahamu fika mfumo wa dunia ulivyo na mahitaji ya nchi yetu ???

Ilikuwaje watu wataalamu wa Uchumi, Sheria, Diplomasia na Ulinzi wakaamua kuicha nchi itumbukie kwenye korongo refu ambalo tunahangaika kutoka mpaka sasa ??? Kwanini hawakuchuliwa hatua pale walipotaka kufanya vitendo vya kihaini baada ya Raisi kufariki ??? Kwanini bado wanaendelea kulelewa huku wakizidi kulihadaa taifa ???
 
Umekosea sana kuwaambia haya, ungeacha wahangaike kuyatafuta wenyewe.
Bwana Yesu alisema "Usimwage lulu kwa nguruwe"
 
MALCOLM LUMUMBA: mada yako ni nzuri Sana vipi lakini unajua kwamba nchi yetu Sasa hivi ipo gizani?Umeeleza vema yaliyotekea ni mabaya lakini haya mambo hayana budi kutokea ili unabii utimie,baada ya gizi hili kipita mwanga utakuja .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Malcom naomba utuonyeshe hivyo vyombo ingebidi vifanye nini kwa ukaidi ule wa JIWE..
 
Madini uliyotema hapa na unayoendelea kutema kwenye huu Uzi nakunyooshea mikono juu! Wewe kwangu ni bingwa! Ni mwalimu!

Heshima yako Mkuu!
 
Ni swali zito na fikirishi kwa mustakabali wa Taifa letu.

Tuseme bila kumung'unya maneno! Hao watu ni wahaini. Hao watu inabidi wanyongwe mpaka kufa hadharani.
 
Exactly, alikuwa anaprotect natural resources za nchi ili nchi inufaike nazo baadae. Wakaja marais wasioona mbali wakafungulia uchimbaji bila kujali kwa kusaini mamikataba ya ovyo yasiyoinufaisha nchi ilimradi tu wamekidhi mahitaji ya ulafi wao. Shame on them!
 

Bandiko bora kabisa lililogusia history, Geopolitics na diplomasia .
 
Bandiko bora kabisa lililogusia history, Geopolitics na diplomasia .
Sisi ni sehemu ya ulimwengu huu tuna haki pia ya kuweka mustakabali mpya wa mwenendo mpya wa mtazamo wa uendeshaji wa masuala ya ulimwengu. Kukwepa kutumia haki hii kisa tuna tetea status quo ya set up ya sasa ambayo haitunufaishi wote bali baadhi yetu hasa wale tulio wakabidhi dhamana ya uongozi ni kukiri udhaifu ambao hatupaswi kuwa nao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…