Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Alichotakiwa Raisi Magufuli ni kutumia busara zilezile za Nyerere kwamba kwenye baadhi ya mambo akaze, lakini kwenye mambo yale ambayo yana maslahi ya pamoja kwa dunia (Common Interest) afanye Compromise. Kama nchi ilikuwa imeingia kwenye mikataba ya hovyo, basi angeanzisha utaratibu wa kuipitia upya (Contractual Review) hata kama ingetuumiza kidogo, lakini ilikuwa ni lazima iwe hivyo kwasababu Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete walifanya makosa kwa kuingia kwenye hiyo mikataba mibaya kiuhalali kabisa bila kulazimishwa.

Tanganyika ilivyopata uhuru wake, ilikuta kuna mikataba mingi sana ya hovyo ambayo ilisainiwa na serikali za Uingereza na Ujerumani. Akili ile ya kiutaifa (Nationalism) inakushawishi kwamba ni lazima ujitoke kwenye hiyo mikataba, lakini busara inakupa swali gumu: UNAJITOAJE ???

Mzee Nyerere alikutana na mikataba kama hii:
  1. The Belbase Treaty 1921- Ambao ulitaka Tanganyika iruhusu Congo, Rwanda na Burundi kutumia bandari ya Dar es salaam kwa malipo ya pound mbili tu kwa mwaka, halafu huo mkataba ni wa milele yani (Ad Infinitum).
  2. The Nile Water Agreement 1929 - Mkataba umesainiwa na waingereza miaka ya 1929 huko na unataka Tanganyika wasitumie maji ya ziwa Victoria.
  3. Royal Workers Agreement 1961 - Mkataba unaitaka Serikali ya Tanganyika kuendelea kuwaajiri wafanyakazi wenye asili ya kizungu ambao bado wako Tanganyika.
  4. Heligoland Treaty 1890 - Umetengeneza mpaka baina ya Tanganyika na Malawi, lakini haukuchora mpaka maalum ndani ya ziwa Nyasa, hivyo kila nchi inaleta taarifa zake.
Mzee Nyerere, alikuwa ni moja kati ya binadamu wenye akili nyingi mno: Alifahamu kabisa kwamba kama angetumia ubabe, basi Tanganyika ingepata madhara makubwa sana. Hivyo akatumia michezo hiyohiyo ya wazungu kuwashinda: Akatengeneza kitu kiitwachoa Nyerere's Doctrine of State Succession. Ambapo alisema hivi, kwanini Tanganyika iendelee kubanwa na mikataba ambayo wawakilishi wake hawakuwepo wakati wazungu wanaisaini ???

Hivyo akatoa miaka miwili na kutumua Notes of Exchange kwa kila taifa ambalo lilisaini mikataba na Tanganyika kabla ya Uhuru kwamba kuanzia mwaka 1961 hadi 1963, inabidi zitume Notes of Exchange ya kuonesha kwamba wanataka kuendeleza hiyo mikataba na serikali ya Tanganyika. Nchi nyingi zilijibu na zile zilizopima kina cha maji zikihisi Tanganyika ilikuwa inatania zilipata hasara baada ya muda kupita.

Wazungu wao walishawishi sana kuanzia kule UMOJA WA MATAIFA kwamba mikataba ya kikoloni inabidi iheshimiwe, lakini Mzee Nyerere akiwa na wakina Mzee Job Lusinde na jopo la wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi, kama Earl Seaton walikaa na kupanga mkakati maalumu wa kupambana na hii mitego ya wazungu. Nyerere's Doctrine of State Succession ilifanikiwa sana na nchi nyingi za Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Msumbuji wakaiga na kufanikiwa kujinasua kwenye hii mitego.

Mzee Nyerere akaenda mbali zaidi, mwaka 1963 kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika akaanzisha kitu kiitwacho The Doctrine of Intangibility of Frontiers. Kwamba mipaka ya wakoloni ni lazima iheshimiwe ili kuzuia taharuki na vita barani Afrika. Mzee Nyerere aliona mbali sana na kufahamu fika kwamba asipopendekeza hili mapema wakati nchi nyingi hazijapata uhuru na likapitishwa basi Tanganyika na maeneo yake mengi yatakuwa salama.

Hivyo wakakubaliana nchi zote huru za Afrika kwamba iwe hivyo, na nchi zote zilizopata uhuru zikalazimika kufuata huu utaratibu hata kama haziupendi. Hadi kufika leo, japo The Doctrine of Intangibility of Frontiers ina mapungufu yake makubwa, lakini ilisaidia kuleta utulivu barani Afrika.

Sasa hebu jiulize kabisa kwa mtu hulka ya Raisi Magufuli, angekuwa ndiyo Raisi wa awamu ya kwanza na akakutana na mambo kama haya. Leo hii Tanzania si ingekuwa imeparanganyika na kuwa vijinchi vidogo vidogo vingi au hata imeshavamiwa na mataifa jirani ??? Raisi gani anavunja mikataba bila kutumia busara huku akiamini yeye anajua kila kitu, mwishowe anaiingiza nchi kwenye korongo la ajabu.

Kibaya zaidi anadiriki kabisa kushirikiana na IDARA YA USALAMA WA TAIFA kutaka kuteka wawekezaji ambao wamemshinda kwenye hoja. Bahati mbaya kumbe hao wawekezaji ni mijasusi ya nje inapata taarifa na kuanza kuhujumu nchi. Hivi kweli USALAMA WA TAIFA umepungukiwa watu wenye akili hadi kufikia This Lowest Point in History ????

SHAME,.....
 

Tunaweza kuweka ushawishi kupitia kuwa na viongozi, raia na wanadiplomasia mahiri ili wakubwa watufikirie sisi wadogo mchango wetu unaweza pia kuchangia mustakabali wa ulimwengu.

Je nchi yetu inao watu wa aina hiyo kwenda duniani kutufanyia kazi hiyo kupitia sekta mbalimbali?

Mtu kama Mohammed Dewji biashara kubwa kikanda , Dr Augustine Mahiga nyanja ya diplomasia , Prof. Abdulrazak Gurnah mshindi wa noble prize fasihi, Dr Philip Isdor Mpango katika majukwaa ya kiuchumi kimataifa, Lt. General Abdulrahman Shimbo operesheni zake kule Shelisheli Seychelles, Prof. Idris Mtulia fani ya pharmacology, General Davis Mwamunyange military intelligence nchi za kusini mwa Afrika n.k Tuliwatumia au tunawatumia ipasavyo ili kujenga ushawishi kimataifa ?

Juzi tumemuona makamu wa Rais Dr Philip Isdor Mpango akishiriki mkutano wa Bloomberg New Economy Forum 2021 Press Archives | Bloomberg New Economy na vigogo wa dunia ktk nyanja mbalimbali, Je tutaendelea kumtumia Dr Philip Isdor Mpango na nyota yake kimataifa iliyopo miaka mingi au tutampiga vita kuwa yupo karibu na mabeberu ?


Our Community Bloomberg​

750+ of the world’s most influential CEOs, leaders, visionaries, scientists, entrepreneurs, and policymakers source : Home | Bloomberg New Economy

17 November 2021
Singapore

Two-Speed Global Recovery: the Dangers of a Widening Rich-Poor Gap



Bloomberg's Shery Ahn discusses with H.E. Dr. Philip Isdor Mpango, Vice President of the United Republic of Tanzania, Tharman Shanmugaratnam, Senior Minister, Republic of Singapore, Dan Schulman, President and CEO, PayPal and Elizabeth Rossiello, CEO and Founder, AZA Finance.
 
Ona Leo Sasa....

Nini?
 
Mkuu Malcom naomba utuonyeshe hivyo vyombo ingebidi vifanye nini kwa ukaidi ule wa JIWE..
Umeniuliza swali ambalo mimi mtu wa nje ya mfumo sina ujuzi wowote ule wa utendaji wa protokali zao. Japo kama raia ninayeipenda sana nchi yangu na mwenye kufuatilia mambo, nafahamu dhahiri kwamba wao kama taasisi zilizo na wataalamu wa mambo ya ulinzi na usalama, uchumi, sheria na diplomasia wanakuwa na utaratibu wa kuhakikisha mwanasiasa havuki mipaka yake na kuvuruga nchi.

Maswali yangu mimi ni haya :
  • Ni kwanini waliruhusu nchi ikavurugika hivi na wao wakashiriki kama watu wasio na utashi ilhali wanajua walikuwa wanacheza mchezo wa hatari ???
  • Raisi Magufuli na hulka zake zile kwanini aliruhusiwa ashike ofisi kubwa kama ile, kwani hakukuwa na mtu mwingine kweli ???
  • Ni kwanini hawa watu waliosaidia kuhujumu nchi na kuiingiza korongoni hawashughulikiwi mpaka leo ili wawe mfano kwa wengine. Mbona Mwalimu Nyerere alilishughulikia lile genge la wana usalama lililokuwa linaongozwa na wakina Emilio Mzena na Peter Siyovelwa kwenye kuua watu kule Kanda ya ziwa ???
 
Mkuu Bagamoyo, huyu Mzee Mpango ni mtaalamu nguli kabisa wa Uchumi na amefanya kazi kwenye taasisi kubwa za kimataifa. Tena ndani ya serikali wapo wengi tu aina yake kwenye nyanja mbalimbali kama ulivyosema. Lakini ilikuwaje nchi ikawa inaendesha utadhani A Newly Independent Banana Republic ???

Kibaya zaidi na wao walishiriki kabisa kwenye yale mazingaombwe, lakini nashangaa mpaka sasa kwanini hawajawajibishwa na wanaendelea kudunda tu kana kwamba hakuna kilichotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…