MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
- Thread starter
- #201
Alichotakiwa Raisi Magufuli ni kutumia busara zilezile za Nyerere kwamba kwenye baadhi ya mambo akaze, lakini kwenye mambo yale ambayo yana maslahi ya pamoja kwa dunia (Common Interest) afanye Compromise. Kama nchi ilikuwa imeingia kwenye mikataba ya hovyo, basi angeanzisha utaratibu wa kuipitia upya (Contractual Review) hata kama ingetuumiza kidogo, lakini ilikuwa ni lazima iwe hivyo kwasababu Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete walifanya makosa kwa kuingia kwenye hiyo mikataba mibaya kiuhalali kabisa bila kulazimishwa.Exactly, alikuwa anaprotect natural resources za nchi ili nchi inufaike nazo baadae. Wakaja marais wasioona mbali wakafungulia uchimbaji bila kujali kwa kusaini mamikataba ya ovyo yasiyoinufaisha nchi ilimradi tu wamekidhi mahitaji ya ulafi wao. Shame on them!
Tanganyika ilivyopata uhuru wake, ilikuta kuna mikataba mingi sana ya hovyo ambayo ilisainiwa na serikali za Uingereza na Ujerumani. Akili ile ya kiutaifa (Nationalism) inakushawishi kwamba ni lazima ujitoke kwenye hiyo mikataba, lakini busara inakupa swali gumu: UNAJITOAJE ???
Mzee Nyerere alikutana na mikataba kama hii:
- The Belbase Treaty 1921- Ambao ulitaka Tanganyika iruhusu Congo, Rwanda na Burundi kutumia bandari ya Dar es salaam kwa malipo ya pound mbili tu kwa mwaka, halafu huo mkataba ni wa milele yani (Ad Infinitum).
- The Nile Water Agreement 1929 - Mkataba umesainiwa na waingereza miaka ya 1929 huko na unataka Tanganyika wasitumie maji ya ziwa Victoria.
- Royal Workers Agreement 1961 - Mkataba unaitaka Serikali ya Tanganyika kuendelea kuwaajiri wafanyakazi wenye asili ya kizungu ambao bado wako Tanganyika.
- Heligoland Treaty 1890 - Umetengeneza mpaka baina ya Tanganyika na Malawi, lakini haukuchora mpaka maalum ndani ya ziwa Nyasa, hivyo kila nchi inaleta taarifa zake.
Hivyo akatoa miaka miwili na kutumua Notes of Exchange kwa kila taifa ambalo lilisaini mikataba na Tanganyika kabla ya Uhuru kwamba kuanzia mwaka 1961 hadi 1963, inabidi zitume Notes of Exchange ya kuonesha kwamba wanataka kuendeleza hiyo mikataba na serikali ya Tanganyika. Nchi nyingi zilijibu na zile zilizopima kina cha maji zikihisi Tanganyika ilikuwa inatania zilipata hasara baada ya muda kupita.
Wazungu wao walishawishi sana kuanzia kule UMOJA WA MATAIFA kwamba mikataba ya kikoloni inabidi iheshimiwe, lakini Mzee Nyerere akiwa na wakina Mzee Job Lusinde na jopo la wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi, kama Earl Seaton walikaa na kupanga mkakati maalumu wa kupambana na hii mitego ya wazungu. Nyerere's Doctrine of State Succession ilifanikiwa sana na nchi nyingi za Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Msumbuji wakaiga na kufanikiwa kujinasua kwenye hii mitego.
Mzee Nyerere akaenda mbali zaidi, mwaka 1963 kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika akaanzisha kitu kiitwacho The Doctrine of Intangibility of Frontiers. Kwamba mipaka ya wakoloni ni lazima iheshimiwe ili kuzuia taharuki na vita barani Afrika. Mzee Nyerere aliona mbali sana na kufahamu fika kwamba asipopendekeza hili mapema wakati nchi nyingi hazijapata uhuru na likapitishwa basi Tanganyika na maeneo yake mengi yatakuwa salama.
Hivyo wakakubaliana nchi zote huru za Afrika kwamba iwe hivyo, na nchi zote zilizopata uhuru zikalazimika kufuata huu utaratibu hata kama haziupendi. Hadi kufika leo, japo The Doctrine of Intangibility of Frontiers ina mapungufu yake makubwa, lakini ilisaidia kuleta utulivu barani Afrika.
Sasa hebu jiulize kabisa kwa mtu hulka ya Raisi Magufuli, angekuwa ndiyo Raisi wa awamu ya kwanza na akakutana na mambo kama haya. Leo hii Tanzania si ingekuwa imeparanganyika na kuwa vijinchi vidogo vidogo vingi au hata imeshavamiwa na mataifa jirani ??? Raisi gani anavunja mikataba bila kutumia busara huku akiamini yeye anajua kila kitu, mwishowe anaiingiza nchi kwenye korongo la ajabu.
Kibaya zaidi anadiriki kabisa kushirikiana na IDARA YA USALAMA WA TAIFA kutaka kuteka wawekezaji ambao wamemshinda kwenye hoja. Bahati mbaya kumbe hao wawekezaji ni mijasusi ya nje inapata taarifa na kuanza kuhujumu nchi. Hivi kweli USALAMA WA TAIFA umepungukiwa watu wenye akili hadi kufikia This Lowest Point in History ????
SHAME,.....