Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

Mtu anakuja kuwekeza unamuita beberu
Diplomasia ya wapi
 
Hivi Rwanda ni dunia
Fdi au Fci kutoka Rwanda na uganda ni asilimia ngap
 
Hawezi kukujibu tena ongezea awataje ata watatu then atueleze walifanya yapi ao watatu?

Ayo majina hutokosa la January, Membe na Nape hapo ndo utajua kweli hatuna watu nchii hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hawakuwa wanaamini ule utapeli, bali ilikuwa ni shuruti. Na ilikuwa ukionyesha kwenda kinyume na ule utapeli unatekwa, kuuwawa au kubambikiwa kesi. Yaani tulipata kiongozi muovu, hisia zake akawa anatulazimisha tuziamini!
Hapa ndio kauliza
Those people we call elite walikua wapi
TICC na vyombo vingine walikua wapi
 
Tanzania itaendeleaje hata hatuna Uwekezaji kwenye technology..?
Umeona wapi serikali ilopita ikipeleka vijana kwa ajili ya ujasus wa kitekinolojia
Uliona wap tukifanya sampling ya technology ..??
Sisi n mazuzu
Ili tupate maendeleo lazima serikal iwekeze kwenye ujasus wa kitekinolojia na ujasus wa kiuchumi sio kutisha investors
 
Hawezi kukujibu tena ongezea awataje ata watatu then atueleze walifanya yapi ao watatu?

Ayo majina hutokosa la January, Membe na Nape hapo ndo utajua kweli hatuna watu nchii hii

Sent using Jamii Forums mobile app
Ben mkapa alifanya nchi yetu first class diplomacy
Alichotakiwa ku fanya Magu pamoja ma ku renovate weakness hakutakiwa kugombana na investors
Tumeonankipinf chake aki close mikataba mbalimbali bila sababu za maana
Like gas, bagamoyo
Afu anaenda ku invest charity na burigi what a shame
 
Na kama kuiba Dili misimamo na maamuzi yao basi wanakuondoa kwa mbinu zao
 
Kuna njia ipi mbadala ambazo nchi za Afrika zitatumia kulinda masilahi yake? Huoni aliyoyapa Gadaffi? Labda utasaidie hata kidogo, nchi kama Tanzania itawezaje kulinda rasilimali zake kwa njia ya urafiki na mabeberu?
Nchi kama Singapore na Korea-Kaskazini ambazo ni ndogo kuliko Tanzania ziliwezake kuwa tajiri huku zikiendelea kushirikiana na mabeberu kama Marekani, Uingereza na Uchina ??? Lakini pia, ni lazima ufahamu kwamba kushambuliwa Muhammar Qhadaffy kuna historia ndefu sana. Hivi mnaikumbuka michezo yake lakini :

-The Lockerbie Incident ???
Majasusi wa Libya mwaka 1988 walilipua ndege ambayo ilikuwa na inatoka ujerumani na kuua abiria zaidi ya 200.
Unapoanza michezo hatari kama hii ni lazima uhakikishe kwamba unaweza kuicheza mpaka mwisho, maana hawa wenzetu wanaweza kukuwekea kiporo hata miaka 100. Ndiyo maana Mwalimu Nyerere aliwaambia watanzania wanaopigania uhuru kwamba Mabeberu hawa nikuwasema na kuwaabisha tu, kupambana nao kijeshi hatuwezi.

  • Kuwaunga mkono waasi wa Tuareg
  • Kuwaunga mkono PLO na UGANDa kwenye uvamizi wa Tanzania

Yeye Muhammar Qhadaffy alikuwa anajitanabaisha kwamba yeye ni mtoto wa Gamal Abdi Nasser wa Misri, hivyo akawa anaiga karibia kila tabia ya Nasser. Sasa Mzee alifanikiwa sana katika kuijenga nchi yake na kuleta maendeleo, lakini ukichagua kuishi maisha kama ya Nasser, Ayatollah, Kim n.k ni lazima uwe makini sana sanaaa. Kuna mengi unaweza kukutana nayo ambayo yatakugharimu..

Hoja ni kwamba unaweza kufanikiwa kulinda maslahi ya nchi yako bila kusababisha kadhia na taharuki, mbona Lee Kuan Yew aliweza jamani ??? Haya mambo ya kusingizia mabeberu kwenye kila kitu yataligharimu hili bara letu
 
Hivi Nyakubonga kuna Raisi ambaye alifanikiwa kukuza uchumi wa Tanzania kwa kupitia Diplomasia kama Mzee Mkapa ??? Japo alikuwa na makosa yake mengi tu, lakini alitumia vizuri mtaji ulioachwa na Mzee Nyerere. Unakumbuka baada kwenda G8 nini kilitokea: Hivi unakumbuka uwekezaji ulivyokuwa nchini na madeni mengi ya nje kufutwa ???

Tena naona mnasahau kuhusu changamoto za kiusalama zilizokuwepo huu ukanda wetu mnamo miaka ya 1995-2003, nchi nyingi ziliingia kwenye matatizo makubwa lakini unafahamu kwanini Tanzania ilitoka salama ??? Tanzania ilikuwa inaangaliwa katika jicho la kipekee sana linapokuja suala zima la siasa za Afrika. Leo hii nini kimetokea ??? Binafsi siamini kabisa kama Tanzania ina msuli ule iliyokuwa nao miaka hiyo......

Halafu leo Raisi Magufuli alitaka kutuaminisha kwamba hawa watangulizi wake hawakufanya chochote wala lolote kwa nchi hii: Ilhali mifumo yote ambayo ilimfanikisha hata yeye kuvuruga nchi yetu ameikuta imejengwa na wao. Sisi kama nchi bado tuna safari ndefu sana, lakini njia na mbinu za watu kama Magufuli ni hatari mno na zimeturudisha nyuma miaka 25. Kurudi kwenye ile nafasi yetu, inawezekana lakini itachukua muda sana na nguvu ya ziada.

NB: Mimi ninachouliza iliwezekanaje nchi ikawa ikavurugwa hivi, ilhali kuna taasisi nyeti zenye wasomi na wataalamu ambao walikuwa wanafahamu fika nchi ilikotoka. Kwanini washiriki utekelezaji wa mauti ya taifa letu halafu leo hii wanaachwa bila hata kupigwa kitanzi au kunyongwa kwa uhaini ili wapuuzi wengine wasidiriki kabisa kurudia jambo kama hili ???
 
Mpinge kwa hoja ndoo tutakuona mwanaume

Sasa hapo unataka nipinge kwa hoja gani wakati bandiko lake lenyewe limejengwa juu ya msingi potofu?

mwambie kwanza aweke ushahidi wa audio au video ili kuthibitisha kwamba JPM alikuwa anajaribu kuitenga Tanzania na Mataifa mengine(Dunia)


halafu akishafanya hivyo tutajadili hoja zake,kinyume na hapo hakuna cha kujadili hapa!!
 
Nakubaliana kabisa na wewe, lakini mkakati wa kujikwamua kutoka kwenye hiyo mifumo ya kibeberu ni ipi ???
Unaufahamu mchezo wa CHESS ??? Siku zote anayemshinda ni yule mwenye kusoma vizuri na kutabiri hatua za adui.
 
mkuu inawezekana jamaa kiukweli hakuwavizuri nyanja zote. Lakini isiwe sababu ya kuondoa sifa kubwa alizokua nazo kwa kuanza kumtukana na kuonesha jamaa alikuwa hatendi mazuri. Na pia tusitupilie macho yetu yote kwenye kitu kimoja Kama wewe unavyouweka uhusiano na dunia Kama ndio chanzo cha maendeleo ambacho jpm hufanya nakuona yale aliyo yafanya ni zero. Na pia umesema unatakiwa ujenge ndani na nje ni sahihi lakini sidhani Kama unaweza ukaanza na nje hafu ukafwata ya ndani ni wapuzi tu Hawa wa Sasa ndio mawazo yao. Lakini njia sahihi ni kuimalisha kwanza ya ndani ya nje huja yenyewe sio lazima uzunguke. hebu niambie Kama nyerere dam ambalo lilikuwa ndoto ya mda mrefu likikamilika litavutia wawekezaji wangapi? Naona umeitaja China na marekani kuwa ni maadui na pia Zinafanya biashara nikweli lakini uhusiano alionao China kwa mmarekani sio wakujipendekeza Kama wakwetu ambao mwisho ni unyonyaji mchina aliweka nchi yake Katika mazingira ya uwekazaji mmarekani akavutiwa kwa uwekeza japo walikuwa ni maadui na mbaka Sasa ni maadui lakini wanafanya biashara kutokana na uhitaji. Pia hata hapa kwetu Katika EAC hatukuwa vizuri na Kenya but Kenya wamenunua kwetu mazao kwasababu wanauhitaji. Kwa hiyo hii point yako ya kuangalia Sana uhusiano na dunia huku tukiwa mikono mitupu mm nadhani haiko sawa.
 
Mkuu Asante kwa andiko lako, Kwanza nikupongeze kwa kutumia lugha halisi kwenye mazingira ya kiutafiti(ulioufanya)

Kunambo umeyaongea ukwel Ila Kuna mengine umepotosha...

Sasa niamze na ukwel, Ni kwel hatuwezi Kama nchi Kuendelea bila kushirikiana na nchi zingine, hila haliwezekani, na hakuna hata nchi moja ambayo inaweza ku survive, bila kuwa na utegemezi wa nchi nyingne, na kwa kuwa kwangu mtanzania sijawahi kuona awamu yoyote ile iliyojitenga na jamii za kimataifa, ndyo maana tunamabalozi karb nchi zote, na tuna mjumbe(balozi) katika general assembly, UN..

Sasa hoja ya pili kwamba nchi imeingia kubaya, sijui unazungumzia awamu ipi ila Kama ya JPM, hapana, maana Mwamba alitaka kuifanya nchi kujitegemea, kuwa sawa na kujari masilahi ya wananchi, hebu twende kwa mifano mkuu, nchi yetu ndo Kwanza tunaawamu ya 6 yaan tunarais wa 6, tukiwa tunamiak 60 ya Uhuru,je can we compared na nchi USA?? Ambayo inarais wa 47?? Inamiaka zaidi takriban 100+ ya Uhuru?? Je democracy ya kwetu inaweza kuwa sawa na wao??

Mkuu, huwezi kuwa masikini ukacompite na tajiri, hapana[emoji15][emoji15] unachotakiwa Ni kuwa na akili ili ujikwamue kutoka hapo, na ndicho alichokuwa anakifanya Mwamba,

Sasa tatzo lilikuja wapi?? Ni kwenye mifumo, baada ya JPM kulala, kwa kuwa hatuna mpango wa maendeleo wa mda mrefu, (tuseme miaka 15-30) miladi yote ambayo iliibuliwa na miongozo yote, inawekwa kando taratb lakini kwa uhakika, Nini kinafuata, tunarudi nyuma kwa kasi ya ajabu kubwa na kwa sabab hatuna vision, and planning, for the long term, tunapiga maketime au kurud nyuma,

Itoshe tu kusema, JPM Wala raisi wa awamu yoyote hakuwahi kujitenga na dunia na Wala hatatokea Rais kwa sabb hyo Ni world order, ila kila1 ana application yake tofauti namna ya kuhusiana na mataifa, itoshe tu kusema hvi tz hii inahitaji mtu jasiri kabisa ambae siyo kwamba anaongea kwa karamu, ila anaongea kwa vyote, Tena in strongly voice, vinginevyo kunawatu wamepinda kuiba kwao Wala hawoni shida, kuona wenzao wanaishi Kama wakimbizi si shida, kuwahurumia akina mama wanaoteseka na maji na huduma za afya Wala hawaoni kuwa tatzo..

Mkuu tz itajengwa na wtz wenyewe ila si kwa kwa kulia Lia et msaada, masaada, na Ni dhambi kuomba kitu ambacho unauwezo nacho..

Mr B
 
Mimi hasa ningependa kufahamu mtazamo wako binafsi kuhusu utawala wa Magufuli ulikuwaje na ukoje hivi sasa? Unaweza kurejea michango yako hapa JF kama afanyavyo Pascal Mayalla.
Sijawahi kubadilisha msimamo wangu kuhusu Raisi Magufuli kwasababu naamini katika kweli, lakini pia nina miiko yangu ya maisha ambayo ndiyo mwongozo wangu. Lakini kikubwa ni kwamba nilianza kuwa adui wa watu wengi humu ndani baada ya kuanza kukosoa aina ya utawala wa Magufuli: Hivyo bila hata kufanya rejea kama bwana Mayalla I'M AN OUTCAST and I MUST ADMIT I LOVE THIS MONIKER,........
 
Nakubaliana kabisa na wewe, lazima Afrika tujifunze kujitegemea na naamini kabisa hili tunaliweza.
Lakini mbinu za kufika hapo haziwezi kuwa zile ambazo tulizijaribu miaka mitano iliyopita.
 
Mimi Malcom Lumumba nitasema ukweli daima, fitna kwangu mwiko. Raisi Magufuli kuna mambo mengi sana aliyafanya vizuri lakini mambo ya nje na diplomasia haviko kwenye hiyo orodha. Dunia yetu ya leo siyo ile ya karne ya 18 na 19 ambayo ulikuwa unaweza kujifungia tu (Isolationism) halafu mambo yakawa yanaenda tu. Tunaishi kwenye ulimwengu wa utandawazi, hivyo ni lazima tunavyojenga ndani na nje tujenge: Lazima kuwe na uwiano mzuri......
 
Nakubaliana kabisa na wewe, lazima tulinde rasilimali zetu kwa WIVU MKUBWA, lakini siyo kutumia ile njia ambayo kipenzi chenu alikuwa anaitumia. Amevuruga mambo na itifikati katika kiwango kikubwa sana,.....

amevuruga kitu gani!!!
mtu mpumbavu akikusoma anawezasema uko timamu kumbe unaumwa kichwa.

unalalamika watu kuchukia mama kusafiri,tukuulize ushirikiano ni kusafiri peke yake!!mtu yuko hewani akirudi makamu karuka lakini umeme na maji hakuna huku.
 
amevuruga kitu gani!!!
mtu mpumbavu akikusoma anawezasema uko timamu kumbe unaumwa kichwa.

unalalamika watu kuchukia mama kusafiri,tukuulize ushirikiano ni kusafiri peke yake!!mtu yuko hewani akirudi makamu karuka lakini umeme na maji hakuna huku.
Anhaa bwana Grinch upo,......???
 
Hivi mtoa mada unadhani kabisa hayo mambo uliyoyaandika hapo juu jiwe angeyajua kweli?

Yeye nje ya mabarabara hakua anajua chochote kile khs Mambo ya diplomasia, uchumi, usalama etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…