Ilitokeaje mpaka makanisa yanaruhusu unywaji pombe wakati inaleta majaribu ya kutenda dhambi zaidi na kukusogeza karibu na ulevi?

Ilitokeaje mpaka makanisa yanaruhusu unywaji pombe wakati inaleta majaribu ya kutenda dhambi zaidi na kukusogeza karibu na ulevi?

Pombe haijaruhusiwa ndo maana hukuti walevi na pombe zao kanisani
 
Sio wasabato pekee ndiyo hawanywi wala kugusa pombe, wapentekoste ndio namba moja kutokunywa na kugusa pombe. Ukinywa utatengwa au kufukuzwa ushirika. Kuna kanisa moja kubwa duniani padri wake alipomaliza misa akaenda klabuni tena klabu cha pombe za kienyeji kijijini. Alipomaliza kunywa kiasi chake akawasha kiko akabugia mdomoni kisha akawasha gari kurudi parokiani.

Kiingiacho si najisi , Bali kitokacho ni najisi

Kwanini wakitoa kibanzi kilicho jichoni kwa mwenzako , na huoni boriti iliyopo jichoni kwako

Kama hauna andiko la biblia linalopinga pombe, (Basi hizi zote ni hadithi za mtume)

Biblia imepinga ulevi na sio pombe
 
Chakula na Pombe ni vitu viwili tofauti kabisa.

Huwezi mlinganisha mtu alielewa na mtu alievimbiwa, mtu alielewa hufanya vitendo vya kujishusha heshima, kutukana hovyo, kuvua nguo, kujikojolea, kujiny*a, kubaka, kuwa mgomvi, n.k.

Hata mtu aliekula kawaida na yule aliekunywa pombe ni vitu viwili tofauti, aliekunywa hutokwa na harufu mbaya mdomoni, uwezo wake kiakili unakuwa umeshuka kuliko skiwa kawaida, pombe inakuwa imeanza kumshuka kunako, yupo kwenye majaribu ya kulewa maana akili yake imeshuka maamuzi, n.k.
Hivi kwa akili yako kila mtu anayekunywa pombe lazima alewe?!
 
Kiingiacho si najisi , Bali kitokacho ni najisi

Kwanini wakitoa kibanzi kilicho jichoni kwa mwenzako , na huoni boriti iliyopo jichoni kwako

Kama hauna andiko la biblia linalopinga pombe, (Basi hizi zote ni hadithi za mtume)

Biblia imepinga ulevi na sio pombe
kama pombe ina kilevi si ndiyo ulevi wenyewe huo? Iwe pombe ya nyanya, miwa, nafaka au matunda kwa kuwa ina kilevi ni pombe hiyo. Ya nini kuleta maandiko ya biblia wakati hoja inajitosheleza? Hoja hujibiwa kwa hoja
 
We ni wa dini gani Kwanza?

Haujui tofauti kati ya kutosheka na ulafi?
 
Habari zenu ndugu zangu naombeni ufafanuzi

Mungu alishakataza pombe agano la kale na hata Yesu katika ile sala ya baba yetu ulie mbinguni kuna sehemu ya kuomba tuepushwe na majaribu ili tuepuke uovu.

Sasa inakuwaje tena kwamba hii pombe inabidi tuwe wanywaji na sio walevi ?

hivi jamani kunywa pombe tu sio majaribu hayo ? Maana ukinywa unapata karaha kenye majaribu ya kutaka kuendelea, pia akili inakuwa imeshuka uwezo wa kufanya maamuzi tofauti na ukiwa hujanywa, pombe nyingine hata ukinywa bila hata kulewa zinaanza kukupa ashki ya kufanya ngono.

Walevi nao huwa wanaanza kwa unywaji wa glasi moja tu tena unakuta ni mara 1 kwa mwezi, ila ikianza kumkolea hata hicho kiglasi hakina kazi tena inabidi aanze kupiga chupa mbili hivi na mazoea huanza kujengeka ya kunywa karibu kila baada ya siku kadhaa, hapo ni mnywaji tu, akianza ulevi pombe inakuwa kama dozi ni kila siku ama mara tatu kwa kutwa kama dawa.

Hata wale walevi wa bangi, unga, sigara, kamali, uzinzi, huwa mwanzoni wanaonja kidogo tu lakini ile raha ikianza kuwakolea ni majaribu tosha, wanajikuta tayari kwenye dimbwi zito kuchomoka inakuwa taabu. Hawezi kuvuka hata siku 2 ama 3 bila kustua.

Sasa inakuwaje kwamba tunaomba tuepushwe na majaribu huku tunajiweka kwa majaribu ???

Hadi sasa ni wasabato pekee ndio nimekutana nao wao sheria zao zinapiga marufuku hata kuonja tone.
Ila bandiko lako lingekuwa na nguvu za hoja kama ungelisindikiza na mstari wowote wa maandiko unaokataza pombe.
Vinginevyo wasomaji wanalitizama kama porojo.
Binafsi mimi situmii kilevi chochote ila sii kwa sababu ya dini.
 
RC siyo kanisa ni secret society tu kama freemasons. that is why wanaruhusu vitu vyote vibaya
wana mission ya kutawala watu na kunyonya pia
walikuwa ma agent wa wazungu kututawala

Na wewe si uwe na mission hiyo kuna mtu kakukataza??
 
Habari zenu ndugu zangu naombeni ufafanuzi

Mungu alishakataza pombe agano la kale na hata Yesu katika ile sala ya baba yetu ulie mbinguni kuna sehemu ya kuomba tuepushwe na majaribu ili tuepuke uovu.

Sasa inakuwaje tena kwamba hii pombe inabidi tuwe wanywaji na sio walevi ?

hivi jamani kunywa pombe tu sio majaribu hayo ? Maana ukinywa unapata karaha kenye majaribu ya kutaka kuendelea, pia akili inakuwa imeshuka uwezo wa kufanya maamuzi tofauti na ukiwa hujanywa, pombe nyingine hata ukinywa bila hata kulewa zinaanza kukupa ashki ya kufanya ngono.

Walevi nao huwa wanaanza kwa unywaji wa glasi moja tu tena unakuta ni mara 1 kwa mwezi, ila ikianza kumkolea hata hicho kiglasi hakina kazi tena inabidi aanze kupiga chupa mbili hivi na mazoea huanza kujengeka ya kunywa karibu kila baada ya siku kadhaa, hapo ni mnywaji tu, akianza ulevi pombe inakuwa kama dozi ni kila siku ama mara tatu kwa kutwa kama dawa.

Hata wale walevi wa bangi, unga, sigara, kamali, uzinzi, huwa mwanzoni wanaonja kidogo tu lakini ile raha ikianza kuwakolea ni majaribu tosha, wanajikuta tayari kwenye dimbwi zito kuchomoka inakuwa taabu. Hawezi kuvuka hata siku 2 ama 3 bila kustua.

Sasa inakuwaje kwamba tunaomba tuepushwe na majaribu huku tunajiweka kwa majaribu ???

Hadi sasa ni wasabato pekee ndio nimekutana nao wao sheria zao zinapiga marufuku hata kuonja tone.
Hata ulaji wa chakula cha kawaida waweza kumfanya mtu kuwa mlafi kama hatakuwa na kiasi, pombe hivyo hivyo ni control yako tu kama huwezi acha.
 
Hata ulaji wa chakula cha kawaida waweza kumfanya mtu kuwa mlafi kama hatakuwa na kiasi, pombe hivyo hivyo ni control yako tu kama huwezi acha.
Kuna utofauti mkubwa sana katika chakula na pombe.

mtu alievimbiwa anaweza kwenda kulala ama kufanya mambo mengine akiwa na akili zake, ni swala la kujutia ila huwezi kuja sikia christmas mtu kavimbiwa kafanya mambo ya aibu mtaani kama pombe.

Pombe ukiitumia uwezo wa akili na kufanya maamuzi unashuka kuliko ukiwa sober, Pombe hata ukinywa inashuka chini inachochea kuzini, hata ukinywa controll yako inazidi kushuka kimaamuzi ndio hapo watu wanalewa,

mtu aanaekunywa ili ajue kipimo chake sahihi ni lazima awe kashawahi kulewa, kwenye kulewa huk kuna kujiny*a, kujikokojolea, kuzima, kuwa na hasira, kutukana ovyo, n.k.
 
Chakula kina madhara yake mwilini, mengi tu kama ilivyo pombe, dawa ni kula kwa kiasi. Umewahi kujiuliza kwanini kufunga chakula ni ibada? Na pia utafiti unaonesha watu wengi wanywaji sana wa pombe sio wafuatiliaji sana wa mambo ya uzinzi, kwani pombe inawapa satisfaction flani.
 
Acha ubishi wa kitoto wewe, Pombe sio chai wala chakula.

Tena kwa taarifa yako tu pombe ni dawa ya kulevya na ni hatari zaidi kuzidi bangi. Mtu akilewa pombe hajitambui kabisa lakini mtu hata akitumia bangi ni ngumu kumtambua maana kazi zake anafanya akiwa anajitambua, mifano ni makazini watu wengi hufukuzwa kwa ajili ya pombe licha ya kwamba wanaovuta bangi kabla ya kuingia kazini wapo, hata Kitwanga alivuliwa uwaziri kwa kutumia pombe kabla ya kuinia bungeni ikamuumbua.

Pombe inamfanya mtu ajiharishie hadharani
Pombe inafanya mtu azimie
Pombe inamfanya mtu ajikojolee hadharani
Pombe inamfanya mtu atukane hovyo
Pombe inamfanya mtu apende ugomvi mwishowe kutolewa meno
 
Nasoma kama ilivyoandikwa......
Screenshot_20230211-153557_Photos.jpg
 
Kunywa kidogo usilewe,tumia mvinyo kidogo kwaqjili ya tumbo lako,mpe masikini kileo asahau shida zake,

Kwenye mvinyo ndio kuna ukweli,acha ulevi kunywa kuchangamsha akili utalijenge taifa.

Pia kumbuka viwanda vya pombe ndio vinalipa kodi kwa kiwango kikubwa kuliko hata hizo dini ambazo kila siku zinalilia kupata msamaha wa kodi.
Kwa Maana kwamba alikua hanywi Pombe NDIO Maana Paulo akamwambia atumie kama dawa.

Kwa hiyo wakati baada ya Kristo wale watu Wa mataifa ambao walimfuata Kristo waliacha Tabia za kipagani za kunywa Pombe . Paulo AKIWA ni Mwisrael Aliyekua na uraia Wa Rumi akagundua kuwa Timotheo Ana TATIZO la tumbo na dawa wakati huo ilikua ni Mvinyo, na Timotheo alikua amesha mjua Kristo na kuacha Pombe Kwa ajili ya kujitakasa na uchafu unaotokana na kilevi.
Paulo akamshauri kuwa anywe pombe kidogo kama dawa.

Mawakala Wa Shetani katika kuingiza Ukristo bandia na kutengeneza Makristo wengi Wa uongo NDIO walioingiza pombe mpaka kwenye nyumba za Ibada.

Haiwezekani mkati usiotiwa Chachu uliwe na pombe iliyotiwa Chachu. Ni mafundisho bandia ya kishetani na yamefanikiwa kuuhadaa Ulimwengu na kuwa na Wakristo wasio na kiasi Wala utu. Wanawaza pombe na biashara yake. Pombe ni Faraja kubwa Kwa waovu na vitendo vyao viovu.
Masister na Mapadri wanaingia kwenye zinaa baada ya kunywa Pombe.
 
Nasoma kama ilivyoandikwa......View attachment 2513706
hayo ni mafundisho ya mtu binafsi aliitwa Ben Sira.

Si maneno ya Mungu wala nabii wake, wala mtu aliempa mission yoyote.

Hizo ni hekima zake yeye kama yeye ambazo hazina connection za yeye kuziandika kwa niaba ya Mungu.

Na ndio maana kitabu hiki wanaokisoma ni wakatoliki tu, hakipo kwenye biblia ya wayahudi toleo la mwanzo kabisa na wala hakipo kwenye biblia za wasio wakatoliki.

Nadhani mawazo ya huyo bwana Ben Sira yaliingizwa ili kutumia nguvu ya ziada kuhalalisha pombe
 
Ni vilevi ndivyo hushikilia rekodi kubwa ya kuchangia kodi, hapo zamani sigara zilikuwa zinalipa zaidi.

Leo hii hata wakiruhusu vilevi vya ziada kama bangi na mirungi vitachangia zaidi.

Vilevi ni chanzo kikuu cha mapato kwasababu hata kodi ikiongezwa watu wananunua tu maana kuacha ulevi si shughuli ndogo (inelastic demand).

Na ndio maana hata kwenye uhalifu ni wauza madawa ya kulevya ndio wanakinga pesa zaidi.. kina Pablo, El Chapo, n.k.

Kuingia rahisi kutoka ni kitu kingine hicho
Mimi nawaza tu, kwa kuwa serikali haina huruma nasi walevi kutokana na kutuongezea bei kila siku km kutukomoa ili ipate kodi kubwa.Kwa nini sisi walevi tusiungane pamoja nchi nzima tugome angalau mwezi bila kunywa pombe yoyote ile tuone matokeo yake hasa kwa lengo la kushinikiza viwanda vitupunguzie bei.Tuungane tugome ili tuone km patakarika mtaani,tumechoka kuonewa,kutukanwa na kunyanyaswa sana sisi walevi
 
Back
Top Bottom