Image ya saini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Image ya saini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

saini-564x272.jpg
Ipi ni saini yake ya kweli ???

Baada ya kufuatilia kwa makini attachment yenye sahihi tofauti za mwalimu zilizowekwa hapa inaonekana kabisa kwamba hizi mbili hapa zimefojiwa. mwandiko ni tofauti kabisa. Kitu kikubwa kinachozitofautisha na sahihi orijino za mwalimu ni hiyo herufi ya mwanzo J. Mwalimu alikuwa anandika J kwa kujiachia na J yenyewe ina mkia mkubwa katika signature zote original lakini hizi nyingine mwandiko sio wa kujiachia na J iko tofauti sana na nyingine.
Cha kujiuliza ni kwamba nani alifoji signature hizi na kwa lengo gani?
 
Nadhani wengi wetu tunakosea sana tunapoa anza kulinganisha maendeleo ya vitu badala ya watu! Enzi za JKN elimu ilikuwa inatolewa bure wakati sasa hivi ni kwa wenye nazo (academia) ... Social GAP ilikuwa almost ZERO wakati sasa hivi tofauti ya kipato ni zaidi ya mbingu na ardhi; Huduma ya Afya ilikuwa inatolewa BURE wakati sasa hivi akina Rev Mwaisapile ndio wanaotiba kwa walalahoi; Uchumi wa nchi wakati ule ulikuwa unategemea kilimo na utalii Revenue ilikuwa inaingia serikalini na faida ya kodi ilikuwa inaonekana WAKATI sasa hivi Fedha za dhahabu, Almasi, Uranium, Gesi, Nickel, Gypsum, Magadi, Utalii na vitalu vya uwindaji vyote vinapelekwa USWIS kwa wajanja wachache! Fedha za walipa kodi walala hoi especially PAYEE inatumika kununulia vitafunwa bungeni na kwenye sherehe za chama... RIP JKN ulie ishi na kuenenda na kauli zako! Nakulilia kwa kuwa ulijali maendeleo ya WATU badala ya MAENDELEO ya vitu kama kumbi za Cinema, Simu za Mikononi nk...
 
Tanzania kila kitu ni kugushi tu,matokeo form 4 feki ARVs feki,naibu waziri wa fedha anatumia jina feki,kifo cha barali kilikuwa feki,rasimu feki,muungano feki hadi sahihi ya nyerere ni feeki!!
Mkuu kunamtu alisema hum JF kuwa IQ ya watanzania ni ndogo, watu wakaponda kwel, lkn ukwel unajidhihilisha wenyewe!tutafika tu!
 
Sasa siye tutajuaje sahihi halisi ya Kambarage? Kwa faida gani?

Kukaa bila kuchangia na kusoma waliyochangia wenzako wanaojua maana ya hitaji la usahihi wa hiyo saini ni AKILI PIA.
 
Baada ya kufuatilia kwa makini attachment yenye sahihi tofauti za mwalimu zilizowekwa hapa inaonekana kabisa kwamba hizi mbili hapa zimefojiwa. mwandiko ni tofauti kabisa. Kitu kikubwa kinachozitofautisha na sahihi orijino za mwalimu ni hiyo herufi ya mwanzo J. Mwalimu alikuwa anandika J kwa kujiachia na J yenyewe ina mkia mkubwa katika signature zote original lakini hizi nyingine mwandiko sio wa kujiachia na J iko tofauti sana na nyingine.
Cha kujiuliza ni kwamba nani alifoji signature hizi na kwa lengo gani?

Maswali ya nyongeza pia ni lini walilifanya tukio hili la kufoji hizo saini? je walifanya haya baada ya tukio la kumuua Mzee wetu Julius Kambarage Nyerere (R.I.P) kukamilika?
 
Mambo ya kisheria hayaendi hivyo. Maana ya kuwekwa sahihi ni kuwa alieweka sahihi anakubali yaliyoandikwa. Sasa kama huna uhakika wa sahihi uhakika wa kilichoandikwa utapatikana vipi?

Kuhusu muda na kubadilika maandishi nakubaliana nawe lakini basi na iletwe document nyengine aliyoisaini kipindi hicho nyuma zilinganishwe!

Je. haiwezekani mtu mmoja akawa na saini zaidi ya moja katika matukio tofauti?
Marehemu Apiyo aliyekuwa Katibu wa Rais angekuwepo angetusaidia.
Mwalimu alikuwa na saini halali zaidi ya moja.
 
Mpendwa kwako si mpendwa kwa wengine. Kama vile ilivyo kwa Kikwete, mpendwa wetu lakini wengine humu wana husda nae za wazi wazi tena ukilinganisha kwa miaka 24 ya Nyerere madarakani hajafanya hata 10% ya aliyoyafanya Kikwete kwa Tanzania kwa miaka 8 tu.

Umedandia tren kwa mbele hujui ukinenacho. Utamfananisha Mwalim na Jk? Amefanya nini kitaifa for individual tanzanian cha kuweza kulinganisha? Umezaliwa jana na uelewa wako ni mdogo sana. Topic ni juu ya forged signature kwenye hati ya muungano na wewe unaleta nyuzi out of topic.
 
Mnahamisha mada
 
FaizaFoxy, wadau wa JF wanakufahamu kuwa wewe ni anti-nyerere kwa 'sababu zako fulani fulani'. Jadili mada, weka itikadi na chuki pembeni. Wote wamekuwa viongozi wa hili taifa kwa vipindi tofauti. Wote wamekuwa na mchango wao kwenye ustawi wa jamii yetu. Uimara wa taifa letu ni kutokana na viongozi waliotangulia na waliopo pamoja na madhaifu yao mbalimbali ya kibinadamu.

Sikukuona ukimwambia hayo niliyemjibu hiyo post.

Jee, ni uongo kuwa ukoo wa Nyerere una mataizo ya akili? nikuwekee ushahidi kutokea humuhumu JF? mtoto wake wa kwanza Nyerere kwa jina Andrew Nyerere anakiri hilo humuhumu JF, wewe ni nani wakuukataa ukweli?

Leo unaongelewa Muungano ambao haukuwahi kuwa mwema na una matatizo toka uanzishwe, na sasa umefikia kuwagawa hata Watanganyika wenyewe kwa wenyewe na Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe, bado unashindwa kusema kuwa huo ulikuwa ni ubovu wa maono ya Nyerere alipoiuwa Tanganyika?

Kwanini kwenye ubovu msiwe wa kweli na kutatua tatizo? Bila kulikubali na kulijuwa tatizo unafikiri utalitatua? hii kumuenzi mtu hata kama alifanya maamuzi mabaya ndiyo maana tunaambiwa Watanzania IQ zetu ndogo sana.

Tuanze kwa kuwa wa kweli na si wanafik. Kumsifia mtu wakati kafanya makosa ni unafik usio na mfano.
 
Last edited by a moderator:
Nikisema humu muungano feki mlikuwa hamnielewi, saa hizi mnahaha, tukiwaambia yule mzee alikuwa majanga hamtuelewi, kaiuwa Tanganyika sasa mnaitafuta kwa udi na uvumba.

Jifunzeni kutoka kwa Wazanzibari, hususan muwatetee wale uamsho, sasa ndio mtawaelewa uamsho walikuwa wanapigania nini.

Upele umepata mkunaji tena mwenye kucha ndefu.........patamu hapo!
 
Hiyo saini ya kwanza mbona ni ya Julius Mamihuri wa pale Mtaa wa Samora? Ni kijana mdogo sana kazaliwa miaka ya 80, anapenda kuvaa mapete ya gold. Sijui saini yake imefikaje Dodoma?!

Ha ha ha jamani noma sana.. eti nini..? kwahiyo ili lijamaa la mapete ndo linajifanya baba wa taifa
 
Hiyo saini ya kwanza mbona ni ya Julius Mamihuri wa pale Mtaa wa Samora? Ni kijana mdogo sana kazaliwa miaka ya 80, anapenda kuvaa mapete ya gold. Sijui saini yake imefikaje Dodoma?!

Ha ha ha jamani noma sana.. eti nini..? kwahiyo ili lijamaa la mapete ndo linajifanya baba wa taifa
 
Je. haiwezekani mtu mmoja akawa na saini zaidi ya moja katika matukio tofauti?
Marehemu Apiyo aliyekuwa Katibu wa Rais angekuwepo angetusaidia.
Mwalimu alikuwa na saini halali zaidi ya moja.

Kunakuwa na sababu gani ya kuwa na saini tofauti, au mzee wetu alikuwa tapeli? Maana matapeli ndio wanaokuwa na saini tofauti!
 
No wonder your not an accountant or a lawyer other wise you could know the alteration of signature what it means!

Kindly enlighten me on the meaning of SIGNATURE! If our president writes "Jakaya M. Kikwete" would you call it a siganature?
 
Kwa hakika kabisa sahihi hizi mbili ni tofauti. Lakini kama binadamu wenye utashi na kufikiri yapaswa kujiuliza nmaswali kadhaa.

1. Sahihi hizi mbili (ya uwongo na ya kweli) zinatoka kwenye document gani?

2. Saini ya juu ukuangalia ni saini iliyoandikwa kwenye kipande cha karatasi, kikabandikwa juu ya eneo la kuweka sasa, ikapigwa photicopy (ndio maana chini kivuri cha mstari ilipoanzia karatasi mpaka kuishia kimeonekana) aliyefanya hivi alifanya kwa malengo gani?

3. Madai ya wajumbe kudai hati itolewe, hati ikaletwa tayari mtu akawa na saini ya pili mfukoni na kuitoa kwa ulinganisho inatia shaka, alijuajeinayokuja itakua feki?

4. Kwa wanaojua maudhui ya mkataba wa awal, je kunamabadiliko?

5. Tunadhani ni kwa nini kiongozi mmoja aliye hai na inadaiwa saini yake ni fake, nae kahojiwa akakanusha kuwa si fake sahihi ni yake, lakini bado tunang'ang'ana ni fake?
 
Hivi Wazanzibari wapo tayari kuishi Tanganyika Kama wageni, wafanye kazi na biashara km wageni, na kwakua mgeni hamiliki ardhi hapa nao waachie majumba yao ya Ilala Msasani Buguruni Kigamboni n.k warudi Unguja na Pemba? Hivi Zanzibar kuna soko la kubeba biashara wanazofanya bara? Hivi wanajua kuwa Watanganyika nao wakitumbukia nyongo hakutakua na kuvumiliana hata kwa kusema sisi tulishajenga na kufungua biashara tuachwe? Hivi wanajua Wazanzibari walio pata Passport bara watalazimika kuzirudisha otherwise waukane Uzanzibar. Na akiirudisha hata pata ya Zanzibar kwa kuwa si mkazi kwa miaka mitano pengine? Tukishiba tufikirie wakati wa njaa pia

hivi wachina,wasouth afrika na wageni wengine munawatizama tu huku wanakuchukulieni rasili mali zenu.wapemba wanalipa kodi wawekezaji kutoka nje kodi zao zinamasharti nafuu.inamaana wewe huependi tanganyika yako kwa sababu tu wapemba wako bara?inamaanisha wapemba wakiondoka bara ndo utaipenda tanganyika?mkataa kwao mtumwa.a u amang the slave
 
Hivi Wazanzibari wapo tayari kuishi Tanganyika Kama wageni, wafanye kazi na biashara km wageni, na kwakua mgeni hamiliki ardhi hapa nao waachie majumba yao ya Ilala Msasani Buguruni Kigamboni n.k warudi Unguja na Pemba? Hivi Zanzibar kuna soko la kubeba biashara wanazofanya bara? Hivi wanajua kuwa Watanganyika nao wakitumbukia nyongo hakutakua na kuvumiliana hata kwa kusema sisi tulishajenga na kufungua biashara tuachwe? Hivi wanajua Wazanzibari walio pata Passport bara watalazimika kuzirudisha otherwise waukane Uzanzibar. Na akiirudisha hata pata ya Zanzibar kwa kuwa si mkazi kwa miaka mitano pengine? Tukishiba tufikirie wakati wa njaa pia

hivi wachina,wasouth afrika na wageni wengine munawatizama tu huku wanakuchukulieni rasili mali zenu.wapemba wanalipa kodi wawekezaji kutoka nje kodi zao zinamasharti nafuu.inamaana wewe huependi tanganyika yako kwa sababu tu wapemba wako bara?inamaanisha wapemba wakiondoka bara ndo utaipenda tanganyika?mkataa kwao mtumwa.a u amang the slave?
 
Back
Top Bottom