Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo.jpg

Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.

Chanzo: Mwananchi

PAKA WA AJABU AINGIA MSIKITINI KUSWALI. Kila akifukuzwa anarudi ndani ya msikiti kutaka na yey...jpg
 
Ile clip niliipenda sana nikaipost whatsapp kila mtu akaiomba na wengine kurepost,

Kibongo bongo yule Paka angeitwa mchawi na hata kusindikizwa na teke la utosi, 🥲

Btw, Surah ambayo Imam alikua anaisoma hadi yule beautiful Paka kumdandia ni Surat al An'am (The Cattle) ayah 148-149
 
Angekua Nguruwe 🐖 kamtulia mabegani je! imamu angepewa tuzo ya kujali wanyama au angeitwa Kafiri?
 
Back
Top Bottom