Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Kajisomee mambo ya Walawi: 11:7-8,

7. Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

8. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao, hao ni najisi kwenu.
Unaambiwa hao Lawi ndio walikua Makuhani wakuu Ila Cha ajabu walikua watenda dhambi wakuu pamoja kutunga sheria km hizo hadi pale Yesu alipotambulika kua yeye ndie Kuhani mkuu asiemtenda dhambi baada ya Pazia la Hekalu lenye urefu wa futi 60 na lenye uzito wa kubebwa na watu zaidi ya 300 kupasikia Kati kwa Kati

Kwa hio walawi nao walikua na mapungufu yao mengi ukiondoa kuwakataza watu wasile kitimoto wenyewe walikua wanakula
 
Asingeitwa Kafiri sababu huyo Nguruwe angekua kamfata yeye na sio kama yeye ndie kamleta Nguruwe na kumuweka begani,

Zaidi angekatisha salaa mwingine angeendeleza na yeye angemtoa nje Nguruwe na kwenda kuoga na kubadili nguo sababu Nguruwe ni najisi kwa Imani yake, na sio tu Nguruwe hata angekua Mbwa bado ni najisi kwake ila Paka sio najisi.
Ila nyama ya Nguruwe 🐖 ukiwa njaa ya kufa kwa mujibu wa Mtume Mohammed S.W.W kwamba Mnyaazi Mungu Subhana wa Tahara ameruhusu ili usife km ipo Nguruwe Basi kula funyango 3/4/5 ili usife na upate kuishi

Sasa je! Mwislamu Kumla Nguruwe 🐖 pindi una njaa ya kufa inaswihi na anakua sio najisi Ila kuguswa nae wakati umeshiba ni najisi na ni haramu ?
 
Hapo muujiza uko wapi?
Ukiletewa videos zaidi za Paka au Watoto wakidandia watu wakiwa kwenye sala si utabaki mdomo wazi,

Kilichowafurahisha watu wote duniani ni Paka kuingia msikitini (tunajua huyo mnyama ni mdadisi) na kwenda kumdandia Imam, kilichofurahisha zaidi ni Imam kutokua distract na Paka yule zaidi akamshikilia vizuri hadi Paka akakaa kwenye bega lake, akamlamba uso, akamlamba mdomo (tunasema a kiss from Cat) kisha huyoooo akateremka akaenda zake,

It's all about humanity, usiwe cruel kwa Wanyama pia ujue Paka hua hamfati mwenye roho mbaya na katili hata siku moja.
Unafiki tu. Unampenda paka unamchukia mkristo. Sasa ndo nini
 
Ile clip niliipenda sana nikaipost whatsapp kila mtu akaiomba na wengine kurepost,

Kibongo bongo yule Paka angeitwa mchawi na hata kusindikizwa na teke la utosi, 🥲

Btw, Surah ambayo Imam alikua anaisoma hadi yule beautiful Paka kumdandia ni Surat al An'am (The Cattle) ayah 148-149
Yule Paka ni wa hapo Msikitini.

Imamu ni wahapohapo Msikitin.

Paka na Imamu washakua Washikaji wa siku nyiiiiiingi.

Ila kwakua mwapenda muonekane, mtaanza sema ni Malaika🤣🤣🤣.

Sasa mlitaka Imamu amfukuze mshikaji wake? Au mlitaka Imamu akatishe swala kisa paka ambaye ni Mshikaji wake??.

DUNIA NZIMA,ITAPIGA MAGOTI KUMUABUDU YESU KRISTO, MWAMBA, ALIYEKUBALI KUTESWA, KUDHALILISHWA NA KUFA, KWA AJILI YA WANADAMU WOTE DUNIANI, YEYE NDIE NJIA NA LANGO PEKEE KUIFIKIA MBINGU.
 
View attachment 2586863

Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.

Chanzo: Mwananchi

Uislamu unazingatia huruma na upendo kwa wanyama, vipi angeingia nguruwe pale angepewa tuzo ya ukimbiaji bora😂😂😂
 
Tunaisubiri kitimoto naye aende kujichumia mathawabu na yeye kama huyo paka naye apate headline za duniani na peponi, kwani yeye hapendi Jahna tul Firdausi?
Firdausi kama firdausi
 
Ila kwakua mwapenda muonekane, mtaanza sema ni Malaika🤣🤣🤣.

Sasa mlitaka Imamu amfukuze mshikaji wake? Au mlitaka Imamu akatishe swala kisa paka ambaye ni Mshikaji wake??.
Daaa we jamaa mkorofi.

Kwema lakini?
 
Tunaisubiri kitimoto naye aende kujichumia mathawabu na yeye kama huyo paka naye apate headline za duniani na peponi, kwani yeye hapendi Jahna tul Firdausi?
Ahahaha kiti moto jahna tul Firdaus ataisikia tu kwenye bomba
 
View attachment 2586863

Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.

Chanzo: Mwananchi

Tuzo ya nini??-- ni ujinga mtupu huo.

Swala inahitaji mazingatio na ndio maana mtu anaposwali haitakiwi pembeni yake kuwepo na karaha ya aina yoyote, mfano kelele za watoto, radio nk, hiyo yote ni kumfanya anayeswali azingatie swala yake, sasa kwa kitendo cha huyo paka kumrukia huyo Sheikh ni kiraha na hivyo bila shaka katika kipindi hicho kwa tabia na sifa za binadamu huyo sheikh alikosa mazingatio katika hiyo swala, kilichotakiwa ilikuwa ni kumuondoa kwanza na halafu swala iendelee, hicho ndicho kilichotakiwa na si vinginevyo.

Wahenga husema; "ukicheza na mbwa atakufuata hadi msikitini" yawezekana huyo sheikh alipenda kucheza na huyo paka.
 
Kitimoto hakina huo mda😂

Kwanza chenyewe hakina uthubutu wa kuingia Msikitini.

Halafu kinavyotoa harufu!!, Siku moja kitimoto kilitoroka kwao kikaja karibu na nyumbani ilkuwa majira ya saa 11 alfajiri, nipo chumbani nikaaaza kuhisi harufu kali na mbaya nikajiuliza inatoka wapi harufu hiyo, mara nikasika mlio wa "grunting" (mlio anatoa nguruwe anapokula), mara nilipochungulia nje asalaleee!! nikaliona bonge la kitimoto linachakua jalalani kwetu, nililitoa balu, huku njia nzima likiacha harufu mbaya na kali sana, sijui hao wanaokula hilo dudu najisi wanalipendea nini??!🤣🤣
 
Back
Top Bottom