Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,264
- 10,535
Tuzo ya nini??-- ni ujinga mtupu huo.
Swala inahitaji mazingatio na ndio maana mtu anaposwali haitakiwi pembeni yake kuwepo na karaha ya aina yoyote, mfano kelele za watoto, radio nk, hiyo yote ni kumfanya anayeswali azingatie swala yake, sasa kwa kitendo cha huyo paka kumrukia huyo Sheikh ni kiraha na hivyo bila shaka katika kipindi hicho kwa tabia na sifa za binadamu huyo sheikh alikosa mazingatio katika hiyo swala, kilichotakiwa ilikuwa ni kumuondoa kwanza na halafu swala iendelee, hicho ndicho kilichotakiwa na si vinginevyo.
Wahenga husema; "ukicheza na mbwa atakufuata hadi msikitini" yawezekana huyo sheikh alipenda kucheza na huyo paka.
Huoni kama angetaka kumuondoa ndio kungemfanya akose umakini na kuharibu swala?
Mtume Muhammad (S.a.w) wakati anaswali wajukuu zake Hassan na Hussein walikua wanamdandia na kumrukia wala hakuwahi kukatisha salaa aliendelea, kumbuka alifuga Paka wengi pia,
Hizi Dini sio ngumu kivile.