Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Hawa ndugu zetu katika imani huwa wanapenda sana petty issues.

Sasa hii nayo ni issue ya kupewa tuzo.?!!
Petty issue iliyoenda Viral Duniani,
Vyombo vikubwa vya Habari Duniani vimeripoti,

It's all about humanity[emoji173], be positive
 
Yaani tunaweza kukaa siku nzima tunamuongelea Paka, hakuna Mnyama ninayempenda kama Paka,
Nimeishi nao tangu mdogo nawajua vema tabia zao na kila kitu chao,

Wewe unasema kochi, anaweza akaenda stoo akanyea kwenye ndoo ya unga halafu anafukia vizuuuri [emoji23]

Ni wewe owner wake unamuelekezaje
Paka nimewahi fuga aisee alikua anafunua chungu anaondoka na Samaki, 😆 namjua Paka vizuri nmefuga sana
 
Paka nimewahi fuga aisee alikua anafunua chungu anaondoka na Samaki, [emoji38] namjua Paka vizuri nmefuga sana
Ulimfuga kienyeji ndio kosa lako,
Paka kama unampa msosi wa uhakika hawezi kuiba, weka ratiba ya chakula sababu Paka anakula hadi mara 5 kwa siku, usimpe nyama mbichi unamfundisha wizi,

Paka wa nyumbani alikua analinda Nyama Kunguru wasidokoe hakuwahi kuiba hata siku moja.
 
View attachment 2586863

Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.

Chanzo: Mwananchi

Sisi tunawaacha paka wanakunya kwenye unga tuzo zetu tunaenda kuzichukua wapi?
 
Ulimfuga kienyeji ndio kosa lako,
Paka kama unampa msosi wa uhakika hawezi kuiba, weka ratiba ya chakula sababu Paka anakula hadi mara 5 kwa siku, usimpe nyama mbichi unamfundisha wizi,

Paka wa nyumbani alikua analinda Nyama Kunguru wasidokoe hakuwahi kuiba hata siku moja.
Sawa Dokta basi yaweza kua nilikosea hio formula yaan alikua anapenda Samaki na akisikia harufu hakai mbali ole wako usimpe atafunua atachukua, 😆
 
Hapo muujiza uko wapi?
Ukiletewa videos zaidi za Paka au Watoto wakidandia watu wakiwa kwenye sala si utabaki mdomo wazi,

Kilichowafurahisha watu wote duniani ni Paka kuingia msikitini (tunajua huyo mnyama ni mdadisi) na kwenda kumdandia Imam, kilichofurahisha zaidi ni Imam kutokua distract na Paka yule zaidi akamshikilia vizuri hadi Paka akakaa kwenye bega lake, akamlamba uso, akamlamba mdomo (tunasema a kiss from Cat) kisha huyoooo akateremka akaenda zake,

It's all about humanity, usiwe cruel kwa Wanyama pia ujue Paka hua hamfati mwenye roho mbaya na katili hata siku moja.
Paka mtu aliemzoea siku zote humfuata na kulala miguuni mwake, yaan hivyo akiona vipi anakupandia anakulalia umpakate ni hivyo yaan wanapenda kustarehe sana 😆 Paka hamfuati mtu ambae hajamzoea au mtu ambae hana mazoea nae kamwe hamfuati na atamkimbia tu na kukaa nae mbali sana
 
Anafunua chungu? Huyo paka itakua alikua anafanya mazoezi ya kunyanyua vyuma kimya kimya 😅😅😅
Si anausukuma mfuniko tu ukianguka anachukua Samaki anaondoka nae anaenda kumla mkija kuangalia mnaona chungu Kiko wazi Paka kaondoka na Samaki, 😆
 
Paka Kajua Ni Wakati wa Sujuud Akashuka Chini,Mashallah Mashallah

Umeona Paka alivyo huyu kamzoea Imam Paka mtu ambae hana mazoea nae hamrukii hivi, ni km ngedere tu ukiondoa wale wanaofuga mbwa Mimi mbwa sipendi, ukimzoea anakuparamia mda wote Ila km hujamzoea anacheza mbali nawe
 
Halafu kinavyotoa harufu!!, Siku moja kitimoto kilitoroka kwao kikaja karibu na nyumbani ilkuwa majira ya saa 11 alfajiri, nipo chumbani nikaaaza kuhisi harufu kali na mbaya nikajiuliza inatoka wapi harufu hiyo, mara nikasika mlio wa "grunting" (mlio anatoa nguruwe anapokula), mara nilipochungulia nje asalaleee!! nikaliona bonge la kitimoto linachakua jalalani kwetu, nililitoa balu, huku njia nzima likiacha harufu mbaya na kali sana, sijui hao wanaokula hilo dudu najisi wanalipendea nini??!🤣🤣
Kwa hiyo we ishu yako na kitimoto ni hiyo harufu au kuna kingine?

Ukihakikishiwa kwamba anaweza kupikwa akanukia bila kuacha hiyo harufu usioipenda, utamla?

Basi acha kumdis
 
View attachment 2586863

Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.

Chanzo: Mwananchi

Wakina msalaba wanasema heti huyo paka ni jini[emoji14][emoji14][emoji14]
 
Naam,
Kwa mujibu wa maandiko na ufafanuzi upo,
Huenda umekwama porini umeishiwa chakula na bado hujajua njia ya kutoka basi kama kuna Nguruwe amekatiza chinja, choma kula kiasi usife kwa njaa ili uendelee na mapambano ya kujinasua, na sio Nguruwe tu hata wanyama wengine ambao walikatazwa unaweza ukala kwa hiyo dharura,

Sio upo zako home umehisi njaa unaagiza nyama yake unakula kwa ugali unashushia na maji baridi halafu useme ni hayo maandiko hapana umekula najisi.
Kwa situation hiyo manake hata Mungu mwenyewe anajiongeza
 
Back
Top Bottom