Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Imamu aliyerukiwa na paka mabegani akiswalisha apewa tuzo

Hizi sasa ndio Akili za Mtanzania halisi,
Halafu tunataka Mabeberu wasiendelee kutoa misaada eti tunajiweza wenyewe, thubutuuuu
Nime kuelewa kamanda kweli wabongo wanawaza uchawi vichwani wao hata wasomi vipi hiyo tabia aitaondoka akilini mwao
 
Mfugaji yoyote wa Paka atakwambia kwamba hilo sio jambo la ajabu kwa Paka kukurukia au kuzunguka zunguka kwenye miguu....
 
Hapo muujiza uko wapi?
Ukiletewa videos zaidi za Paka au Watoto wakidandia watu wakiwa kwenye sala si utabaki mdomo wazi,

Kilichowafurahisha watu wote duniani ni Paka kuingia msikitini (tunajua huyo mnyama ni mdadisi) na kwenda kumdandia Imam, kilichofurahisha zaidi ni Imam kutokua distract na Paka yule zaidi akamshikilia vizuri hadi Paka akakaa kwenye bega lake, akamlamba uso, akamlamba mdomo (tunasema a kiss from Cat) kisha huyoooo akateremka akaenda zake,

It's all about humanity, usiwe cruel kwa Wanyama pia ujue Paka hua hamfati mwenye roho mbaya na katili hata siku moja.
Tatizo lake huyo ajui nini maana ya mwiujiza
 
Kajisomee mambo ya Walawi: 11:7-8,

7. Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

8. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao, hao ni najisi kwenu.
Mkiristo hakubaliani na andiko hilo hata umfanyeje
 
Angekua Nguruwe [emoji241] kamtulia mabegani je! imamu angepewa tuzo ya kujali wanyama au angeitwa Kafiri?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nyie jamaa wagomvi sana
 
View attachment 2586863

Imamu aliyeteka vichwa vya habari mitandaoni siku za hivi karibuni kupitia video fupi iliyosambaa ikimuonyesha akirukiwa na paka mabegani wakati akiwa anaswalisha swala ya Taraweeh ametunukiwa tuzo.

Tukio hilo ambalo liliibua hisia za watu mbalimbali baada ya kumuonesha Imam huyo kutoonyesha kutetereka na kutomfukuza paka huyo wala kukatisha swala hiyo ambayo huswaliwa kila siku usiku katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa tovuti ya Breaking latest News Imamu huyo aliyetajwa kwa jina la Walid Mahsas kutoka nchini Algeria ametunukiwa tuzo na Ofisi ya masuala ya dini iliyo chini ya serikali ya nchi hiyo kwa kuonyesha kwake taswira ya kwamba uislamu pia unazingatia huruma na upendo kwa wanyama.

Chanzo: Mwananchi


hiyo tuzo anastahili paka
 
Kwa hiyo we ishu yako na kitimoto ni hiyo harufu au kuna kingine?

Ukihakikishiwa kwamba anaweza kupikwa akanukia bila kuacha hiyo harufu usioipenda, utamla?

Basi acha kumdis
Kajisomee mambo ya Walawi: 11:7-8,

7. Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

8. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao, hao ni najisi kwenu.
 
Angerukiwa na kitimoto apo sijui ingekuwaje
Angeingia nguruwe sokomoko lingeanza huku kwa maamuma mpaka imamu mwenyewe angeshtuka.Tungesukumana naye kwa magongo waliombele pamoja na imamu tungewahadithia tu baadae.
 
Tunaisubiri kitimoto naye aende kujichumia mathawabu na yeye kama huyo paka naye apate headline za duniani na peponi, kwani yeye hapendi Jahna tul Firdausi?
Miaka ya nyuma kwenye msikiti wa Manzese Kitimoto aliingia sijui alitokea wapi wakati wa Swala...alikula mikwaju huyo!!
 
Back
Top Bottom