Imani Kajula CEO Mpya Simba

Imani Kajula CEO Mpya Simba

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Anachukua nafasi ya Barbara Gonzalez

FB_IMG_16747289498482283.jpg
 
Sijui uongozi wa Sasa una haraka gani wakati Kuna uongozi mpya unachaguliwa hivi karibuni Kuna hatari kama uongozi utakuja tofauti wakatofautiana.
Kuna kipindi alikuwa anahusika na jezi za Simba Kuna hatari ya mgongano wa maslahi wakati wa kutangaza tenda za jezi.
 
MRITHI WA BARBARA APATIKANA: Uongozi wa klabu ya Simba umemtangaza Imani Kajula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wake mpya akirithi mikoba ya Barbara Gonzalez ambaye alitangaza kung’atuka katika nafasi hiyo mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa tarrifa ya Simba SC, Kajula ambaye ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira, amepewa mkataba wa miezi sita.

MBALI NA MASWALA YA SOKA, KAJULA PIA NI MBOBEZI KATIKA NYANJA ZIFUATAZO:

Kajula amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika sekta za kibiashara, amewahi kuwa Meneja Mauzo wa Benki ya CRDB kati ya mwaka 1999 hadi 2003 kabla ya kujiunga na Benki ya TPB kama Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara.

Amewahi pia kuhudumu katika Benki ya NMB kama Mkuu wa Masoko na Mawasiliano.

FB_IMG_1674730409420.jpg
 
Sijui uongozi wa Sasa una haraka gani wakati Kuna uongozi mpya unachaguliwa hivi karibuni Kuna hatari kama uongozi utakuja tofauti wakatofautiana.
Kuna kipindi alikuwa anahusika na jezi za Simba Kuna hatari ya mgongano wa maslahi wakati wa kutangaza tenda za jezi.
huyo kateuliwa na tajiri and co,subiri uongozi mpya uingie
 
Back
Top Bottom